Posts

Showing posts with the label riwaya

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya 11

Image
Nilikuwa barabarani natembea, ilikuwa siku ya vurugu kwani vibanda vya wamachinga vilivyokuwa katika hifadhi ya barabara, vilikuwa vinabomolewa na kusababisha vilio vikubwa. Inasemekana mwanzoni serikali iliwaruhusu wafanye biashara, wakajenga vibanda, lakini sasa serikali hiyohiyo iliwataka waondoke kwa madai kuwa ilikuwa ina wapanga vizuri. Hata sikuelewa, nikaendelea na safari zangu. Nilishtuka nilipopita katika nyumba aliyoishi Asi, niligundua kuwepo kwa dalili za mtu kurejea hapo. Kwanza mazingira yalisafishwa na taa ya nje haikuzimwa japo ilikuwa saa tisa mchana. Nikahisi kurejea kwa Babuu. Kisha nikaandaa jambo langu. XX     XX     XX Mlango ulifunguliwa saa saba usiku, mwanamume mwenye kipara akaingia, akabofya swichi iliyokuwa upande wa kushoto, taa ikawaka na hapo akajionea yale asiyoyatarajia. Chumbani palikuwa na mgeni asiyekaribishwa, tena aliikamata vyema bastola yake na alielekeza alipo, hakuonekana kuwa na masihara hata kidogo. Mwan...

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya 10

Image
“ Nkuu wa Nkoa kaja kwa ku shtukiza… patachimbika humu ndani nakwambia, atatumbuliwa ntu baada ya ntu,” alisema bibi mwingine aliyekuwa anamuuguza mjukuu wake. “Unapiga simu wapi?” nilimfokea nesi ambaye alionekana kupiga simu kuwaita wakubwa wake. “Usipige simu, usimuite yeyote, hapa nimekuja kwa kushtukiza na nitaingia kila wodi kwa kushtukiza.” “Sawa mkuu,” walijibu watumishi wale wa afya. Wagonjwa wakatabasamu. “Sasa sikiliza,” niliendelea. “Wagonjwa watibiwe, pesa italipwa baada ya matibabu, tuhakikishe tunaokoa uhai kwa gharama yoyote. Pesa zipo tu na haziwezi kamwe kufanana na thamani ya uhai wa mwanadamu.” “Ndiyo mkuu,” walijibu. “Natoka humu katika ziara yangu hii ya kushtukiza, msipige makelele wala msinifuate, pia msipigiane simu, nakwenda kwenye jengo lile wodi ya wazazi, nawatakia utekelezaji mwema.” Nilitoka katika wodi ile na kuanza kuelekea wodi ya wazazi. Nilikuwa na hofu kwamba, watu wangeongezeka zaidi, lazima ningegundulika kuwa mimi siyo mkuu wa mkoa. ...

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya Tisa

Image
Chafu Tatu alipenda sana kwenda katika danguro lile na alikuwa maarufu sana kwa mtindo wake. Huenda katika danguro akiwa na shilingi elfu kumi. Elfu moja ananunua sigara. Anabakiwa na elfu tisa. Elfu tatu anapata huduma kwa dada wa kwanza. Anamaliza nakutoka nje, anavuta sigara. Anatoa elfu tatu tena kwa dada wa pili, anatoka na kuvuta sigara, halafu anatoa elfu tatu kwa dada wa tatu, akimaliza hapo, anaenda nyumbani kulala. Chafu Tatu ! “Chafu Tatu,” aliita askari. “Naam afande,” aliitika Chafu Tatu kwa adabu. “Hela unatoa au hutoi?” “Afande naomba unielewe, tayari nilikuwa nimeshaingia kwa dada wa pili, sasa nina elfu tatu tu,” alijibu Chafu Tatu, askari wakaangua kicheko, wakachukua ile elfu tatu na kumuachia kwa masharti kwamba, asirudie tena tabia hiyo kwani ni mara ya saba sasa anakamatwa. Chafu Tatu alishuka katika gari lile la polisi. Nikabaki mimi na wao. “Kijana acha kutuchelewesha, leta hera haraka,” alisisitiza askari ambaye kwa sababu ya tumbo lake kuwa kubwa s...

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya Nane

Image
Silaha niliyokuwa nayo, Beretta, iligunduliwa na mtaalamu Bartolomeo Beretta mwaka 1526 huko Gardone Val Trompia nchini Italia. Ni silaha nzuri ya kawaida ambayo imekuwa ikitumiwa na watu binafsi kwa kujilinda. Kama alivyo mtaalamu Bartolomeo Beretta , nami mtaalamu Mako, niligundua silaha kubwa ya maangamizi niliyoipachika jina Mako 29. Ikiwa na maana kwamba, Mako aligundua silaha hiyo akiwa kijana wa miaka 29 tu. Mako 29, ina uwezo wa kupiga risasi 3,000 kwa dakika na inaweza kumdhuru adui akiwa umbali wa hata kilomita mbili. Ukichunguza kwa makini utagundua Mako 29, imeishinda AK 47 ya Warusi na M16 ya Wamarekani karibu mara tatu au tano, pengine hata kumi hesabu zikifanywa vyema. Silaha hiyo tayari ilikuwa mikononi mwa jeshi letu, na walikuwa wanaifanyia mazoezi ili ianze kutumika. Hata hivyo, kwa sababu mimi ndiyo mbunifu wake, nilikuwa nayo moja niliyoificha kwa siri. Na hata ningetaka, ningetengeneza nyingine. Mpishi hafi kwa njaa. Ni kama utani, lakini zilikatika wiki tat...

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya Sita

Image
Siku zote nilikuwa naishia nje nimtafutapo Asi pembezoni mwa nyumba aliyokuwa akiishi. Sasa niliamua, niingie mpaka ndani, huenda Babuu alimkataza kutoka. Nilifika katika nyumba ile, nikagonga mlango kwa dakika nyingi bila kufunguliwa. Mlango ule ulikuwa mkubwa tena wenye pande mbili zilizokutana katikati ambako palikuwa na kitasa. Baada ya gongagonga bila majibu, nilijaribu kuzungusha kitasa, hapo nikagundua palifungwa. Sikuelewa kama mwenye nyumba alikuwa ndani au alitoka, hayo ndiyo matatizo ya vitasa! Hata hivyo nilihisi wenye nyumba hawakuwepo. Niliamua kupeleleza kidogo kuhusu nyumba ile na wakazi wake, kwa kuwa sikutaka kujulikana kama nilikuwa ninapeleleza, niliamua kutafuta watoto wadogo, hawa wasingeweza kunitilia shaka lolote. Niliingia katika chumba kimoja cha biashara kilichokuwa kimeandikwa ‘play station’. Ndani yake mlikuwa na watoto waliokuwa wanacheza michezo mbalimbali ya kompyuta. Nami nilikwenda moja kwa moja mpaka katika sehemu moja iliyokuwa wazi, nikaomba ...

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya Tano

Image
Baada ya siku tatu bila kupita mitaa yake Asi huko Mwananyamala ndanindani, nilipita tena ili niweze kumuona msichana huyu. Hali ilikua tofauti kuliko siku zote, msichana hakuwepo. Nilitazama kama kweli ni nyumba ileile ambayo tangu nianze kupita sijawahi kumkosa akiwa kakaa kibarazani, ilikuwa nyumba ileile na msichana hakuwepo. Hata hivyo sikuwa na wasiwasi, nilihisi huenda alikuwa na kazi humo ndani. Nilipita tena siku iliyofuata, msichana hakuwepo. Nikapita siku nyingine, hakuwepo, nikapita tena na tena mpaka chovya chovya ikamaliza buyu la asali, lakini msichana hakuwepo. Hapo nikapatwa na hofu, hofu ya kupotea kwa mwanamke aliyekula pesa zangu. Shilingi halali za Kitanzania elfu kumi na tisa. Pengine hazikuwa zile pesa, kwani ni pesa kidogo sana zisizotosha hata kununua simu ndogo ya Kichina, pengine nilianza kumpenda Asi, binti mdogo aliyekuwa na tabasamu pana, mwepesi kuzoea watu tena aliyechangamka vyema. Basi baada ya pitapita ya siku nyingi bila kumuona, nikaahidi kumtaf...

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya Nne

Image
Mara kwa mara niliendelea kupita alikoishi Asi, kama kawaida yake, aliomba pesa ndogo, nikampa kisha nikaandika katika kikaratasi changu. Sasa jumla ilifika Shilingi elfu kumi na tisa za Kitanzania. Katika kumbukumbu nzuri, nakumbuka kwenda Coco Beach na Asi, huko tulikula mihogo ya kuchoma, tukaogelea na kuzungumza mengi. “Bwana Mako,” Asi aliniita. “Naam,” niliitika. “Uliwezaje kuwadhibiti wale wezi wa siku ile, tena wakiwa na silaha?” “Unajua…” nilisema nikitafakari namna ya kubadili mazungumzo ili asinichimbe sana. “Katika Jiji hili la Dar es Salaam, kuna watu wanajiona wao ni wababe mno na huwaambii chochote. Achana na huo mkasa, nakumbuka siku moja nikitoka katika matembezi yangu, jamaa mmoja alisimama katikati ya njia na kuniamrisha nitoe pesa. “Jamaa yule wala hakuwa na silaha yoyote na alikuwa peke yake. Nilimuuliza, Unajiamini nini kutaka kuniibia mimi tena ukiwa peke yako? Jamaa akawa mkali na akaanza kusogea nilipokuwa. Alipofika hatua tatu ili aweze kunifikia,...

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya Tatu

Image
Nilinyanyuka huku nazungumza, “Mheshimiwa, huyo dada hana funguo ya kabati la fedha, mimi ni mfanyakazi mwenzake nakuja kukupatieni.” Wakati nazungumza nilikuwa nasogea kuelekea walikosimama, nilitembea mpaka karibu kabisa na yule jamaa mwenye silaha, nikiwa nimeukunja mkono wa kushoto, huku nikichezesha mkono wa kulia wakati ninapozungumza, nilimzubaisha yule jamaa mwenye silaha, nikampiga ngumi kali ya kidevu kwa mkono wangu wa kulia na kabla hajadondoka chini, nikawahi kuikamata silaha yake. Sasa ikawa yangu, yule mwenzake alibabaika, nikamwamuru akae chini haraka. Jamaa wale walifungwa kamba mpaka walipokuja askari kuwakamata. Hakuna aliyeweza kuamini kuwa, mahali pale palitoka kufanyika tukio la uvamizi wa silaha. Mziki uliendelea kama kawaida na watu walicheza kwa nguvu zaidi kuliko mwanzo. Hata hivyo, watu walianza kuniangalia sana, wengine wakinishukuru na kuninunulia vinywaji vya bure kwa ushujaa ambao nilionyesha. Burudani iliendelea kutoka kwa ma Dj ambao nilitambua w...

Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya Kwanza

Image
Nilipita siku ya Jumatatu huko Mwananyamala katika nyumba za ndani sana. Baada ya kuvuka mitaro mitatu, nikaona nyumba iliyokuwa na baraza kubwa. Hapo barazani alikaa binti mrembo sana ambaye kwa uzuri wake angetosha kushtua, kuchanganya na kupunguza ufanisi wa akili ya mwanamume yeyote. Binti huyu aliyekuwa na sura iliyochongeka kwa mfano wa umbo la yai, alivalia dela lililoficha umbo lake. Nilitembea hata nikawa mkabala na mahali alipokaa, nikaporomosha salamu huku nikipunga mkono, “Habari.” “Nzuri,” msichana alijibu akibadili mkao, nami nikaendelea na hamsini zangu. Nilipita siku ya Jumanne huko Mwananyamala katika nyumba za ndani sana. Baada ya kuvuka mitaro mitatu, nikaona nyumba iliyokuwa na baraza kubwa. Kama jana, binti yule alikaa, nami nikaporomosha salamu, “Habari.” “Nzuri,” msichana alijibu akibadili mkao, nami nikaendelea na hamsini zangu. Lakini wakati nikitembea, nilisikia vishindo vikija. Nilipogeuka, niligongana uso kwa uso na msichana niliyemsabahi. “Kaka…” ...

Mfalme Anataka Kuniua | Sehemu ya 10

Image
  Mako alitembea taratibu mpaka aliposimama askari. Umbali wa askari mmoja na mwingine ulikuwa hatua hamsini na tano. Alipomfikia, alimsabahi. “Hujambo Ai.” “Sijambo Mako, pole,” alijibu askari, kisha akaendelea, “umefuata nini hapa, huruhusiwi kuwa eneo hili, nikuchome singe?” “Ni bora kufa kwa kuchomwa singe kuliko kunyongwa bila hatia. Sikiliza Ai, nipo hapa kwa sababu nataka unisaidie. Nisaidie kuchelewa kupiga filimbi.” “Mako, unataka nikusaidie kutoroka?” “Kutoroka nitatoroka mwenyewe, nisaidie kuchelewa kupiga filimbi. Usipige filimbi mpaka nitakapozama mtoni.” Ai ni binti yatima, wazazi wake walifariki kwa ajali ya mtumbwi alipokuwa na umri wa miaka kumi na nne. Hakuzaliwa mjini Kanakantale, alizaliwa kijijini Kanakado, hata hivyo baada ya kupoteza wazazi, alichukuliwa na dada yake mpaka hapo Kanakantale. Alipofika Kanakantale, maisha ya dada yake yalikuwa magumu tena ya ufukara wa kutisha. Yeye na dada yake walifanya kazi ya kuuza matunda kandokando ya barab...

Mfalme Anataka Kuniua | Sehemu ya Tisa

Image
  Wakati dada anasimulia, Mfalme aligonga katika chumba kile na kumtaka Malkia aongozane naye haraka . Basi Malkia akasimama asiyetaka huku akiuliza, “Ikawaje sasa, niambie haraka niende…” “Mako alienda Kwa mfalme…” alijibu dada akiongea haraka, “alipofika kwa mfalme wa majitu akafanya maonyesho kadhaa yaliyokusanya majitu mengi ajabu. Lile jitu lililompokea nalo likapewa cheo nyumbani kwa mfalme hata likasahau habari za umasikini wa awali. Baada ya kuwa amekaa kwa muda wa miaka miwili, Mako akamuomba mfalme huyo amsaidie kurejea Duniani kwa lengo la kuwatoa hofu ndugu na jamaa zake ambao wanaweza kudhani kuwa amekufa. Basi Mfalme wa Majitu alimsaidia Mako kurejea na tangu arejee hajarudi tena huko japo njia anaifahamu. Alimaliza dada kusimulia. Wakati huo mfalme alikwisha fungua mlango na kumkamata mkono Malkia aliyekuwa amesimama kisha akatembea naye haraka kuelekea alikojua yeye. *** Ilikuwa mchana siku ya pili Mako akiwa gerezani. Wenzake watatu hawakuwa na hofu, pengin...

Mfalme Anataka Kuniua | Sehemu ya Nane

Image
  Siku mpya ilifika, Bwana Mako na watoto wa Jitu walikuwa wa kwanza kuamka, na tazama akishirikiana na watoto wa Jitu, alikuwa ametengeneza meza kubwa ambayo ilikuwa na kimo sawa na tumbo la majitu. Baada ya kukamilika kwa meza, akashirikiana na watoto kuipeleka nyuma ya nyumba ambako kulikuwa na ukumbi mkubwa, kisha akawaamuru watoto wakamuite baba yao. “Niliahidi kukufanya tajiri.” alisema Bwana Mako baada ya Jitu kufika. “Na hii meza ndiyo utajiri wenyewe?” Jitu liliuliza. “Ndiyo, meza hii ndiyo utajiri wenyewe, lakini haiwezi kuwa utajiri bila mimi niliyekaa juu yake.” “Sikuelewi unanichanganya!” lililalamika Jitu. “Sikiliza rafiki mwema,” alisisitiza Bwana Mako, “watume wanao waende mjini, wawatangazie watu maneno haya: Nyumbani kwa baba yetu, kuna maonyesho hayajawahi kutokea. Mtu mkubwa kutoka sayari iitwayo Dunia, amemtembelea baba yetu, ajabu ni kwamba, pamoja na ukubwa wake huko Duniani, huku anaonekana kiumbe mdogo. Ama kweli kila mkubwa na mkubwa wake. Njoo ...

Mfalme Anataka Kuniua | Sehemu ya Saba

Image
Akiendelea kushangaa, alishtushwa na sauti ya vishindo, alipotazama mbele, aliona Jitu kubwa refu lipatalo futi hamsini na unene wake ni kama mibuyu miwili. Bwana Mako mwenye futi tano nukta nane, alionekana kiumbe mdogo ilhali Duniani alikotoka yeye ni miongoni mwa watu warefu. Basi kwa kuhofia, alikimbia akajificha nyuma ya mbao mojawapo ya ndege. “Usijifiche,” jitu lilisema kwa upole, “nimekuona tangu unadondoka na chombo chako. Siwezi kukudhuru kiumbe mdogo.” Bwana Mako alisogea karibu na Jitu akizungumza, lakini kwa sababu ya ule urefu wake, Jitu halikuweza kumsikia, hivyo lilimbeba likamweka juu ya bega lake mahali palipo karibu na sikio mazungumzo yakaendelea. “Asante kwa msaada, hapa nipo wapi?” aliuliza Bwana Mako. “Hapa ni Mailanda, nchi ya mfalme Solupa, katika bara la pili kati ya matatu yaliyopo katika sayari yetu isiyo na jina.” Jitu lilijibu. Bwana Mako akagundua kuwa, ndege yake ilimshusha katika sayari nyingine ya watu hao wakubwa. Waliendelea kuzungumza, Bw...

Mfalme Anataka Kuniua | Sehemu ya Sita

Image
“Nini kinakuliza Malkia wangu, ni hii habari ya Mako kuhukumiwa kunyongwa!” aliuliza dada yule aliyemsimulia malkia mkasa wa Mako na Simba mzee. “Ndiyo, mtu asiye na hatia atakufa baada ya mvua mbili kwa sababu yangu.” “Maskini Mako, ni aheri angebaki katika nchi ya majitu kuliko kurudi tena huku!” alijibu Dada. “Una mkasa mwingine wa Mako nisimulie tafadhali,” alisema Malkia akifuta machozi. Dada akakaa sawa kusimulia, nao wenzake wote wakakusanyika na kutengeneza kikao cha watu watano. “Kwa muda mrefu Bwana Mako alitamani kuitembelea Dunia aione yote akiwa juu. Ndipo alipopata wazo la kutengeneza ndege ambayo ingemsaidia kutimiza malengo yake. Umbo la ndege lilitengenezwa kwa mbao za mninga, ndani aliweka furushi kubwa la nyasi ambalo lingetumika kama kiti cha rubani, nyuma ya kiti cha rubani aliweka godoro nene, hili lingetumika kulala pale anapokuwa amechoka na muda huo ndege ingekuwa katika ‘autopilot.’ injini za ndege hii na namna ilivyofanya kazi, ilikuwa siri yake Bwan...