Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta | Sehemu ya 11

Nilikuwa barabarani natembea, ilikuwa siku ya vurugu kwani vibanda vya wamachinga vilivyokuwa katika hifadhi ya barabara, vilikuwa vinabomolewa na kusababisha vilio vikubwa. Inasemekana mwanzoni serikali iliwaruhusu wafanye biashara, wakajenga vibanda, lakini sasa serikali hiyohiyo iliwataka waondoke kwa madai kuwa ilikuwa ina wapanga vizuri. Hata sikuelewa, nikaendelea na safari zangu. Nilishtuka nilipopita katika nyumba aliyoishi Asi, niligundua kuwepo kwa dalili za mtu kurejea hapo. Kwanza mazingira yalisafishwa na taa ya nje haikuzimwa japo ilikuwa saa tisa mchana. Nikahisi kurejea kwa Babuu. Kisha nikaandaa jambo langu. XX XX XX Mlango ulifunguliwa saa saba usiku, mwanamume mwenye kipara akaingia, akabofya swichi iliyokuwa upande wa kushoto, taa ikawaka na hapo akajionea yale asiyoyatarajia. Chumbani palikuwa na mgeni asiyekaribishwa, tena aliikamata vyema bastola yake na alielekeza alipo, hakuonekana kuwa na masihara hata kidogo. Mwanamume mwenye bastola ni mimi