Posts

Showing posts with the label kiswahiliadvanceexam

Mtihani wa Kiswahili 2 Kidato cha Sita 2024 NECTA Majibu

Image
Muda: Saa 3 Sehemu A (Alama 40) Jibu maswali yote katika sehemu hii. 1.  Wasanii huongozwa na mbinu mbalimbali katika kutunga kazi za fasihi simulizi. Onesha mbinu zinazotumiwa na wasanii katika kutunga igizo kisha tunga igizo fupi linalohusu madhara ya ukeketaji. Taratibu za kutunga maigizo - Kuchagua tukio la kuigizwa Tukio hilo, liwe na mchango chanya katika jamii , ikiwemo kuelimisha. - Kuchagua mahali pa kutendeka kwa jambo Mahali panaweza kuwa: ofisini, shuleni, kijijini barabarani n.k - Kuamua mtindo wa kuwasilisha jambo la kuigizwa Hapa mwandishi anaweza kutumia fumbo, vichekesho n.k - Kupanga hoja kuu zinazojenga maudhui ya igizo Maudhui hujikita katika migogoro au mivutano. Masuluhisho ya migogoro yanatakiwa kupatikana. Mfano, jambazi kuu hukamatwa mwisho wa igizo. - Kuweka mpangilio wa maonyesho Mtunzi atumie mpangilio mzuri ambao utasaidia wasomaji waweze kuelewa kazi yake. - Kubuni wahusika Mwandishi anashauriwa kubuni wahusika wenye sifa tofauti: wanene, weupe, weusi...

Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2024 NECTA

Image
Muda: Saa 3 Sehemu A (Alama 40) Jibu maswali yote katika sehemu hii. 1.  soma shairi lifuatalo kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata: Majira pia Nipashe , taarifa nazitoa Na redio niwabishe, kama ikiwafikia Majirani niwapashe, jambo nilokusudia Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Ndege nawaelezea, tabia yake murua kucheka yake tabia, kununa hakuzoea Wageni wakiingia, fadhila huwatendea Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Tabia za firauni, hana ninawaapia Na kuranda mitaani, si yake hiyo tabia Marafiki wa Kihuni, hapendi kuwasikia Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Kisa niwaelezeni, tunduni nikamtoa Msusa nambari wani, kisa si kisa alia Hilo kosa namba wani, huzuni imenitia Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Lingine lilochangia, tunduni nikamtoa Kosa sugu nadhania, sijui kama sawia Kufuga ndege Songea, sijui kama sawia Ndege nimemfungua, wafugaji chukueni. Mara aliposikia, mwingine nimechukua Tundu akalibomoa, porini akakimbia Goti nikampigia, katu kanikatalia Ndege ni...

Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2024 1

Image
Muda: Saa 3 Maelekezo 1. karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane. 2. Jibu maswali yote katika sehemu A na maswali matatu kutoka sehemu B. swali la tano ni la lazima. 3. Sehemu A in alama arobaini na sehemu B ina alama sitini. 4. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali. 5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani. 6. Andika namba yako ya mtihani au jina katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia. Sehemu A (Alama 40) Jibu maswali yote. 1.  Soma kifungu cha habari kisha jibu maswali yanayofuata: Utawala bora ni hali ya viongozi kusimamia vyema maslahi ya taifa lao. Ni kitendo cha kutenda haki kwa wote na kuhakikisha maisha mazuri kwa kila mmoja. Kiongozi anaposhindwa kutawala vyema, wananchi hupatwa na kihoro hasa pale ndugu zao wanapoanza kuuawa kwa sababu ya kukosoa serikali. Serikali inayoua watu wake haifai hata kidogo. Ni vyema kama viongozi watasimamia demokrasia kwani demokrasia ni utawala wa watu wote ...

Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2021 2

Image
Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu: 1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu. 2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi. 3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0653 250 566. 4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho. 5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili). Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 895 321 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 250 566 (Daud Mhuli). Pata Majibu ya Mtihani Huu, Gusa Hapa Kuwasiliana Nami. Muda: Saa 3 Maelekezo 1. karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali nane. 2. Jibu maswali yote katika sehemu A na maswali matatu kutoka sehemu B. swali la tano ni la lazima. 3. Sehemu A in alama arobaini na sehemu B ina alama sitini. 4. Zingatia maagizo ya kila sehemu na kila swali. 5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani. 6. Andika namba yako y...

Mtihani wa Kiswahili 2 Kidato cha Sita 2020 2 Fomati Mpya

Image
Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu: 1. Mtu yeyote na popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu. 2. Fanya mtihani huu kwa kutumia aina yoyote ya karatasi. 3. Ukimaliza, piga picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0754 89 53 21. 4. Subiri mtihani wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho. 5. Gharama ya mtihani huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili). Namba za malipo ni: M – Pesa 0754 89 53 21 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 25 05 66 (Daud Mhuli). Muda: Saa Tatu Sehemu A (Alama 40) Jibu maswali yote     1.    Orodhesha dhima nne za tamthiliya ya Kiswahili tangu kupata uhuru mpaka hivi sasa.     2.    Jadili kwa ufupi dhima nne za mhakiki wa kazi za fasihi.    3.    Kwa kutumia mifano, jadili kwa ufupi jinsi uandishi wa riwaya ulivyoisaidia jamii yetu. Toa hoja tano.     4.    Soma kwa makini habari hii ki...