Posts

Showing posts with the label makala

Matokeo NECTA Kidato cha Sita 2026

Image
NECTA Wametangaza matokeo ya kidato cha sita, wapo wanafunzi waliofanya vyema, lakini wapo wanafunzi ambao wameshindwa kufikia malengo yao. Tazama Hapa Matokeo NECTA Kidato cha Sita 2026 Wanafunzi waliofanya vizuri tunawapongeza na kuwatakia kila la heri katika safari yao ya masomo yanayoendelea. Wanafunzi waliofanya vibaya, wasikate tamaa, bado wana nafasi yakurudia mitihani yao. Tafsiri ya kufanya vibaya ni kushindwa kufikia malengo. Kwa mfano, mwanafunzi aliyekuwa na malengo ya kwenda chuo kikuu, pale anapopata chini ya D mbili, hujiona kama ambaye hajafikia malengo kwani anatakiwa aongeze D nyingine moja. Huu si muda wa kukata tamaa, bali ni muda wa kurudia tena. Mwanafunzi aliyepata C moja na E, huyo anahesabiwa kuwa na sifa za kwenda chuo kikuu hata kama hajapata D mbili. Katika kurudia mitihani, wanatakiwa watambue kwamba, mtaala sasa umebadilika, vitabu ni vipya siyo vile ambavyo walisoma zamani. Hata hivyo, masomo haya yanaeleweka vyema na yeyote anayetemaani kufaulu vyema ana...

Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Jeshi la Wananchi JWTZ

Image
Jeshi la wananchi Tanzania limetangaza nafasi za kuandikishwa na jeshi hilo kwa vijana wenye baadhi ya sifa hizi: raia wa Tanzania, umri kuanzia miaka 18 mpaka 25 kwa kidato cha nne na sita na miaka isiyozidi 28 kwa wanaotoka vyuoni au elimu ya juu na awe na cheti cha jeshi la kujenga taifa kilichopatikana kwa kujitolea au kwa mujibu wa sheria. kuandika barua inayokubalika , kutakufanya uitwe katika usaili huu wa nafasi hizi ambazo zina waombaji wengi. Unapotuma maombi, anza na barua yako, Weka nakala ya kitambulisho chako cha NIDA ikifuatiwa na nakala ya cheti cha kuzaliwa, na vyeti vya shule, nakala ya cheti cha JKT, karatasi moja iliyoandikwa namba yako ya simu, kichwa cha habari kiwe, NAMBA YA SIMU YA MKONONI, halafu nenda posta kayatume maombi hayo katika anuani yao iliyoandikwa hapo kwenye mfano wa barua ya maombi JWTZ. Huu hapa mfano wa barua ya kuomba kuandikishwa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ): Mtaa wa Kambangwa, S.L.P 1248, KINONDONI, DAR ES SALAAM. 1...

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi TAKUKURU Ajira Mpya

Image
TAKUKURU  wametangaza nafasi za kazi kwa vijana wenye sifa mbalimbali. Nafasi mpya za kazi zilizotangawa na TAKUKURU zinayahusu makundi mawili: Kundi la kwanza, Muombaji awe na angalau elimu ya shahada ya kwanza iliyotolewa na chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika moja ya fani zifuatazo: Uhasibu, Usanifu Majengo, Usimamizi wa Biashara, Usanifu wa Majengo, Ukadiriji wa Majengo (Quantity Surveying), Uhandisi wa Usindikaji wa Kemikali, Maendeleo ya Jamii, Sayansi ya Kompyuta/TEHAMA, Uhandisi wa Ujenzi, Uchumi na Mipango, Uhandisi wa Umeme. Lishe na Sayansi ya Chakula, Usimamizi wa Rasilimali Watu, Usimamizi na Tathmini ya Ardhi, Sheria, Uhandisi wa Mitambo, Uhandisi wa Mafuta na Gesi, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Miradi, Ushauri Nasaha, Utawala wa Umma, Mahusiano ya Umma/Mawasiliano ya Umma, Usimamizi wa Kumbukumbu, Sayansi ya Michezo/Elimu ya Viungo, Takwimu, na Uhandisi wa Maji. Soma: Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi JWTZ Kundi la pili: u...

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza

Image
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=.  Gusa Hapa  Kuwasiliana Nasi. Tunaandika Mfano wa barua hii ya maombi ya kazi jeshi la magereza kwa sababu tumeshuhudia mifano mingi mtandaoni ambayo siyo sahihi na inawapotosha waombaji. Basi Mwalimu Makoba ili kuweka mambo sawa na ili kuwanusuru waombaji wasishindwe katika hatua za awali tu za barua, anakuja na mfano wa barua hii, ulio sahihi na unaokubalika kote. Jeshi la magereza limetoa nafasi za kazi kwa vijana wenye sifa. Kitu muhimu zaidi katika uombaji wa nafasi hizi ni barua ya maombi ya kazi. Kumbuka kwamba, barua ya maombi ya kazi ndiyo kipaumbele namba moja kitakachotumika katika kuchuja nani anafaa na nani hafai. Katika barua yako ya maombi ya kazi, hakikisha barua yako inakuwa tofauti na barua za watu wengine. Hakikisha unaandika au anaandika mtu. Epuka kabisa kuandikiwa barua yako na akili mnemba ( AI ), kwani lugha ya ...

SMS 20 za Mahaba Makali Kumtumia Mpenzi Wako

Image
Makala hii imeandikwa na wadhamini wetu: Tunakuletea meseji kali za mahaba unazoweza kumtumia mpenzi wako na kumfanya awe na furaha muda wote. Meseji hizi za mahaba unaweza kuzituma kwa mpenzi wako muda wowote, unaweza kumtumia asubuhi, mchana, jioni na hata usiku. Meseji hizi, zitalifanya penzi lenu lizidi kuwa imara siku zote. Meseji hizi za mapenzi unaweza kuzituma kwa njia ya meseji za kawaida, WhatsApp , na njia nyinginezo. Unaweza kutuma meseji moja kila siku. Kwa kipindi cha siku 20 tu, penzi lako litabadilika na kuwa bora mno. 1.  Nimekuchagua wewe, ninafuraha kwamba na wewe umenichagua mimi. 2.  Ninashukuru kuwa nawe , ninatabasamu, ninacheka na mara chache ninalia. 3.  Mpenzi ninayejivunia , asante kwa kuwa bora kwangu siku zote. 4.  Nina bahati kubwa kuwa katika mapenzi na wewe rafiki yangu. Nakupenda sana mpenzi. 5.  Hakuna ninachotaka zaidi ya kukufanya wewe mpenzi wangu mwenye furaha siku zote. 6.  Uzuri wako, akili zako na utu , vinanifanya...

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi ya Mauzo | Kiswahili

Image
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=.  Gusa Hapa  Kuwasiliana Nasi. Huu ni mfano wa barua ya mtu anayeomba kazi ya mauzo katika kiwanda fulani. Mwombaji kazi huyu ana elimu ya shahada na anajieleza vyema. Katika barua yake, amendika vyema anuani yake. Kwa kuwa hana sanduku la posta , ameanza na namba ya simu ikifuatiwa na barua pepe. Katika kiini ametumia aya nne: Aya ya kwanza ameeleza jinsi yake, umri pamoja na kazi anayoomba. Ameeleza alipoona tangazo la kazi, lakini hajaeleza ni tarehe gani tangazo hilo liliwekwa. Pengine hakuwa na uhakika ndiyo sababu ya kuacha kipengele hicho. Aya ya pili anaeleza elimu yake. Katika kipengele hiki hatuoni uzoefu wa kazi. Tunarejea katika hoja kuwa, pengine mwombaji kazi huyu hakuwa na uzoefu wowote wa kuweka. Aya ya tatu anaeleza kwa nini apewe kazi hii yeye na si mtu mwingine. Anafafanua kutokana na uzoefu wake, lakini uzoefu huu hak...

Uandishi wa CV au Wasifu | Maswali na Majibu

Image
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=.  Gusa Hapa   Kuwasiliana Nasi. Nimekuwa nikiulizwa maswali mengi na watu mbalimbali kuhusiana na CV au Wasifu. Hapa nimeweka maswali ninayoulizwa sana pamoja na majibu yake. 1.  CV au Wasifu ni nini? CV au wasifu ni maelezo kuhusu mtu fulani ambapo maelezo hayo huangazia historia ya elimu pamoja na uzoefu wa kazi. Waajiri huhitaji CV yako ili iwarahisishie kukufahamu na kupata mawasiliano yako. 2.  CV bora ina kurasa ngapi? CV bora ina kurasa mbili hadi tatu. CV ya ukurasa mmoja haifai na CV yenye zaidi ya kurasa tatu haina vigezo. Jifunze: Jinsi ya Kuandika Barua ya maombi ya Kazi 3.  Wadhamini katika CV ni watu gani? Wadhamini katika CV ni mtu yeyote anayekufahamu ambaye endapo atapigiwa simu na waajiri ataweza utoa maelezo kukuhusu. Mdhamini anaweza kuwa rafiki yako uliyesoma naye na sasa anafanya kazi fulani. Anaweza...

Mfumo wa Maombi ya Ajira za Serikali Unavyoweza Kukupa Kazi

Image
Katika zama hizi za maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia , mfumo wa maombi ya ajira za serikali umebadilika kutoka kuchaguliwa moja kwa moja mpaka kuomba mwenyewe tena kwa njia za kidigiti. Waombaji wengi kwa sababu ya elimu ndogo ya matumizi ya vifaa vya kiteknolojia , wamekuwa wakifanya makosa makubwa waombapo nafasi za kazi . Ajira za serikali zimekuwa zikiombwa kwa njia nyingi lakini njia maarufu ni: Mfumo wa maombi ya ajira TAMISEMI  na Recruitment Portal-Ajira. Katika mfumo wa Recrutment Portal, wengi wakiuita Ajira Portal, kazi nyingi hutangazwa kutoka waajiri mbalimbali. Ni jukumu la mwombaji kuandika barua ya kazi na kutengeneza wasifu pamoja na kutuma vyeti vyake tayari kwa maombi yake kufanyiwa kazi. Katika Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI, nyingi ya kazi ziombwazo ni Ajira za Walimu na Ajira za Kada ya Afya. Serikali inapotoa ajira hizi hutangaza na waombaji huruhusiwa kuanza kutuma maombi yao. Katika mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI, waombaji wengi wamekuw...

Uhakiki wa Wimbo Nipeni Maua Yangu wa Roma Mkatoliki

Image
Roma Mkatoliki  ni mwanamuziki machachari anayefanya mziki wa kufokafoka  maarufu kama ‘Hiphop.’ kibao cha Mr President  kilimtambulisha vyema. Katika wimbo huo, msanii huyu anamsema waziwazi rais kuwa kashindwa kutimiza ahadi yake ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Baada ya kibao hicho, alijipatia umaarufu mkubwa na alitoa vibao vingine vikali na kama kawaida aliendelea kusema mambo mazito bila kificho. Roma Mkatoliki hakuishia kuwasema wanasiasa tu, aliwasema hata wachungaji katika wimbo wake wa Pastor . Roma siyo malaika, kuna wakati anakosea. Katika wimbo uitwao Tanzania  anasikika akisema, “Kimbilio la waliofeli ni ualimu na upolisi” (Roma, 2008). Hapo msanii alikosea pengine ni kwa kukosa taarifa muhimu juu ya sekta nyeti ya ualimu na ile ya upolisi. Kuna hatari ya kubeba kila kinachosemwa na watu na kukitangaza zaidi na Roma hajaiepuka hatari hii. Mwalimu Julius Nyerere  aliyeleta uhuru wa Tanzania hakufeli, Mwalimu Mahatma Gandhi aliyewapatia uhuru India...