Jinsi ya Kuandika Tangazo| O level na Advance

Matangazo ya gazetini huandikwa kwa lengo la kutangaza biashara. Kwa kuwa magazeti yana wasomaji lukuki, hivyo njia hii hudhaniwa kuwa miongoni mwa njia rahisi zaidi za kuwafikia watu wengi ambao hapo baadaye hugeuka wanunuzi wa bidhaa inayotangazwa. Uandishi mzuri zaidi wa matangazo ndiyo utakaofanya bidhaa yako inunuliwe. Uandishi mbovu hugeuka kero kwa watu. Mambo Muhimu ya Kuzingatia 1. Kichwa cha habari. Kiandikwe kwa herufi kubwa. 2. Taja aina ya biashara. 3. Taja bidhaa unazouza na bei zake. 4. Taja mahali inapopatikana bidhaa yako. 5. Taja mawasiliano yako. Mawasiliano yanaweza kuwa ya simu, barua n.k. hata hivyo, simu ni bora zaidi, kwa sababu mawasiliano yake ni ya haraka. Mfano wa Kwanza MASOMO KWA WANAFUNZI WOTE Kituo cha Mwalimu Makoba kinatoa huduma ya kufundisha wanafunzi wanaorudia mitihani na walio shuleni kwa masomo ya sayansi, sanaa na biashara. Gharama zetu ni shil...