Posts

Showing posts with the label kiswahiliformfive

Uhakiki wa Riwaya ya Ua la Faraja

Image
Wasiliana na Mwalimu ili Kujiunga Darasa la Uhakiki wa Vitabu vyote vya Fasihi Mtaala Mpya kwa Kugusa Hapa Mwandishi: W.E. Mkufya Mwaka: 2004 Mhakiki: Mwalimu Makoba Utangulizi Profesa Madumla akiizungumzia riwaya ya Ua la Faraja alisikika akisema, “Mkufya anajua kuitumia lugha ya Kiswahili vilivyo… ni fundi wa ujenzi wa taharuki.” Huwa sipendi kubishana na Profesa Madumla, lakini katika hili alidanganya. Haifahamiki kwa nini Madumla alidanganya, ila moja kati ya hoja hizi huenda ikawa kweli: pengine hakukisoma kitabu , na kama alikisoma, huenda kuna manufaa fulani aliyapata, kama hakuna kabisa manufaa yoyote, basi Madumla uzee umeanza kumwingia! Mkufya ni Mwanasayansi aliyeivamia sanaa, sanaa ikamgaragaza vilivyo, Ua la Faraja ni Riwaya ndefu kama andiko la tafiti za Kisayansi, ina kurasa 423! Ni kama riwaya yake mwenyewe ilikuwa ikimdhihaki na kumweleza, “Sanaa ina wenyewe!” Riwaya hii imekosa ujenzi wa taharuki, kila tukio linalofuata linatabirika na matukio mengine wala hayakupasw...

Uhakiki wa Riwaya ya Mirathi ya Hatari

Image
Wasiliana na Mwalimu ili Kujiunga Darasa la Uhakiki wa Vitabu vyote vya Fasihi Mtaala Mpya kwa Kugusa Hapa Mwandishi: C. G. Mung’ong’o Mwaka: 1977 Mhakiki: Mwalimu Makoba Utangulizi Mirathi ya hatari kisomwe kwa tahadhari. Yale yanayojadiliwa humo, ni mambo ya kufikirika ambayo katika dunia hii iliyojaa uhalisia hayana nafasi. Kitabu hiki kisiposomwa kwa tahadhari, kinaweza kusababisha changamoto tatu: Kwanza, wanafunzi wataamini habari za uchawi kuwa ni za kweli. Wataanza kuiona dunia kama sehemu ya miujiza na si uhalisia wa bidii ya kufanya mambo. Pili, wanafunzi watapatwa na hofu, watakapougua, watahisi pengine wamechezewa ilhali kuugua ni hali ya kawaida katika maisha na vipo visababishi mbalimbali wakiwamo mbu waenezao malaria. Changamoto ya tatu bado haijajulikana na inaninyima usingizi! Kwa hivyo unaposoma kitabu hiki, na unapohakiki riwaya hii, tambua jambo moja, yanayosemwa humu hayawezi kutokea katika ulimwengu wa kawaida. Dunia yetu inaongozwa na kanuni nayo sayansi imethi...