Dhima Tano za Mofimu KI Katika Lugha ya Kiswahili
Siku zote ambazo nilisimamia mitihani ya taifa, nilisimamia wanafunzi waliokuwa shule. Sikuwahi kusimamia wanafunzi wa kujitegemea mpaka ilipowadia mwaka fulani ambapo nilipangwa kwenda kusimamia mtihani wa taifa katika shule fulani ndani ya jiji la Dar es Salaam. Muda ulipowadia, nilifika katika kituo changu, baada ya kufuata taratibu zote, nilisimama pembezoni ya mti ili niweze kuwaona wanafunzi waliokuwa wakifika shuleni hapo tayari kufanya mtihani. Alipita binti mmoja mrembo sana ambaye naye alikuwa miongoni mwa wale wanaofanya mtihani, kwa sababu ya urembo wake, nilikosa nguvu za kusimama na isingekuwa kuushikilia ule mti, ningedondoka! Hata hivyo, nilikaa katika hali ya kuhisi kizunguzungu kwa muda wa dakika tano, hali ilipokuwa shwari, nikaelekea darasani ambako ndipo mtihani ulikuwa ukifanyika. Niliingia darasani, mimi na mwenzangu mmoja tuliyekuwa tunasimamia pamoja, tulitimiza taratibu zote na mtihani ulianza. Katika chumba hiki cha mtihani, yule binti mrembo sana, alik...