Notes za Kiswahili Kidato cha Pili | Form Two


Namba 2

Nukuu za Kiswahili kidato cha pili ni:









Uundaji wa maneno ni mada ambayo inaeleza namna maneno yanavyoundwa kwa kutumia uambishaji. Mofimu nazo zimejadiliwa kwa kina.

Matumizi ya lugha katika miktadha mbalimbali ni mada ambayo inaeleza kuhusu lugha inavyotumika katika mazingira mbalimbali. Ili kuwezesha uelewa, mada hii imejadili kwa kina masuala kama: rejesta, misimu na lugha ya maandishi na ile ya mazungumzo. Mbali na hayo, utata katika mawasiliano umejadiliwa.

Uhakiki wa kazi za fasihi simulizi ni mada ambayo inaangazia kwa kina uhakiki wa mashairi katika ngazi ya kidato cha pili na uhakiki wa maigizo. Vipengele vya fani na maudhui katika ushairi na maigizo navyo vimejadiliwa.

Uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi ni mada ambayo inajadili njia mbalimbali za uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi. Miongoni mwa njia za uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi ni: kichwa, maandishi, vinasa sauti, kanda za video na kompyuta. Faida na hasara za kila njia ya uhifadhi zimejadiliwa.

Utungaji wa kazi za fasihi simulizi ni mada ambayo inaeleza kuhusu utungaji wa mashairi na ngonjera. Mwanafunzi atajipatia mbinu mbalimbali za utungaji na mifano ya mashairi na ngonjera zilizotungwa kwa kuzingatia mbinu hizo.
Uandishi ni mada ambayo inaeleza kuhusu uandishi wa insha za hoja, barua rasmi, simu ya maandishi na dayolojia. Mifano ya insha za hoja, barua rasmi na ngonjera imetolewa.

Usimulizi ni mada ambayo inaeleza kuhusu mambo mbalimbali ya kuzingatia katika usimulizi wa matukio. Mfano wa usimulizi wa tukio umeoneshwa.

Ufahamu ni mada ambayo inaeleza kuhusu ufahamu wa kusikiliza na kusoma. Mbali na hayo, mada hii imeeleza kuhusu ufupisho na matumizi ya kamusi.

Furahia kusoma mada hizo bure. Na endapo utahitaji kitabu cha Kiswahili kidato cha pili katika ‘soft copy’ au ‘hard copy’, tafadhali wasiliana nami kwa namba 0754 89 53 21 | 0653 25 05 66.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne