Utungaji wa Kazi za Fasihi Simulizi | Kiswahili Kidato cha 2
Kazi
za fasihi simulizi hazikutokea tu, kuna mtu alitunga kazi hizo. Mada hii,
inaangazia utungaji wa kazi za fasihi simulizi:
Utungaji wa mashairi
Kanuni za Utungaji wa Mashairi
Utungaji
wa mashairi una kanuni mbili:
1. Fani
2. Maudhui
Katika
fani, mshairi azingatie lugha anayotumia kama: tamathali za semi, methali nahau
na misemo pamoja na picha na taswira.
Pia,
mshairi azingatie kama mtindo wa shairi, kama ni shairi la kimapokeo au shairi
la kisasa.
Pia,
mshairi azingatie muundo wa shairi lake, kama atatumia mistari miwili, mmoja,
sita ama apendavyo yeye.
Katika
maudhui, unapotunga shairi zingatia wazo lako.
Mfano: ni lipi lengo la wewe kutunga shairi? Inawezekana unatunga shairi
ili kuzungumzia hali ya umasikini unaoikumba nchi yako, au pengine una lengo
tofauti.
Pia,
zingatia ujumbe au mafunzo yanayopatikana katika shairi ulilotunga. Unalenga
kufikisha ujumbe gani?
Mfano wa shairi lililotungwa kwa kuzingatia kanuni
Kubaka
Nimekuwa nikipima, najiuliza kichwani,
Watu kugeuka kima, asili yake nini,
Si busara si hekima, wala halina
utani,
Kubaka huo unyama, chanzo chake
kutamani.
Ninaanza kuwasema, tuchungue kwa
makini,
Midume iso heshima, inavuruga amani,
Hawana hata huruma, utadhani hayawani,
Kubaka kama mnyama, chanzo chake
kutamani.
(HRT
Muzale)
Ngonjera
Ngonjera
ni aina ya igizo linalotungwa kwa kufuata kanuni za ushairi wa kimapokeo.
Katika ngonjera, kuna wahusika wawili au zaidi wanaojibishana. Mara nyingi
mwishoni mwa ngonjera wale wanaobishana hukubaliana na hapo ngojera huwa
imekwisha.
Kanuni za kutunga ngonjera
1. Kuteua mada
Mada
inaweza kuwa, mjini au kijijini, ukosefu wa lishe kwa watoto n.k
2. Kuweka dhamira
Ni
lipi wazo kuu la mtunzi wa ngonjera? Wazo kuu linaweza kuwa, maendeleo, uhalifu
na amani.
Mfano wa ngonjera
MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2020
Mzee
Uchaguzi
umefika, viongozi kuchagua,
Hakuna kubabaika, kama moto wa mabua,
Rushwa hiyo kwangu taka, busara kuibagua,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Hakuna kubabaika, kama moto wa mabua,
Rushwa hiyo kwangu taka, busara kuibagua,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Kijana
Wala
Sitapiga kura, kupoteza muda wangu,
Chagua wauza sura, wasioona uchungu,
Kiona vyao vipara, ni vyeusi kama vyungu,
Nasema kura sipigi, uchaguzi ukifika.
Chagua wauza sura, wasioona uchungu,
Kiona vyao vipara, ni vyeusi kama vyungu,
Nasema kura sipigi, uchaguzi ukifika.
Mzee
Kijana
elewa sasa, faida za kuchagua,
Tena si vyema kususa, taja angukia pua,
Na usitoe ruksa, serikali kuiua,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Tena si vyema kususa, taja angukia pua,
Na usitoe ruksa, serikali kuiua,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Wote
Kushiriki
uchaguzi, ni bora si kulalama,
Hatuachi uchokozi, kwa uchaguzi salama,
Hakuna kumwaga chozi, kwako we baba na mama,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Hatuachi uchokozi, kwa uchaguzi salama,
Hakuna kumwaga chozi, kwako we baba na mama,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Maigizo
Maigizo
ni tendo la kuiga sura, tabia, matendo na mazungumzo ya watu au viumbe wengine.
Taratibu za kutunga maigizo
1. Kuchagua tukio la kuigizwa
Tukio
hilo, liwe na mchango changa katika jamii, ikiwemo kuelimisha.
2. Kuchagua mahali pa kutendeka kwa jambo
Mahali
panaweza kuwa: ofisini, shuleni, kijijini barabarani n.k
3. Kuamua mtindo wa kuwasilisha jambo la
kuigizwa
Hapa
mwandishi anaweza kutumia fumbo, vichekesho n.k
4. Kupanga hoja kuu zinazojenga maudhui
ya igizo
Maudhui
hujikita katika migogoro au mivutano. Masuluhisho ya migogoro yanatakiwa
kupatikana. Mfano, jambazi kuu hukamatwa mwisho wa igizo.
5. Kuweka mpangilio wa maonyesho
Mtunzi
atumie mpangilio mzuri ambao utasaidia wasomaji waweze kuelewa kazi yake.
6. Kubuni wahusika
Mwandishi
anashauriwa kubuni wahusika wenye sifa tofauti: wanene, weupe, weusi, warefu, wafupi
n.k pia, wahusika hawa wawe na uhalisia na wahusika halisi waliopo katika
jamii.
Mfano wa igizo
Bodaboda:
Habari yako dada. (Akisimamisha pikipiki yake.)
Msichana:
Nzuri, shikamoo!
Bodaboda:
Aaaah, usinizeeshe binti, vipi, panda nikupeleke, mtoto mzuri kama malaika,
haifai kutembea kwa mguu.
Msichana:
Sitaki, niache nisome, ukiendelea kunifuata nakupigia kelele za mwizi.
Bodaboda:
tobaa! Yamekuwa hayo tena. (Anawasha pikipiki yake na kuondoka.)
Maswali
1. Eleza kanuni muhimu za kutunga
mashairi.
2. Tunga shairi la kimapokeo lenye beti
nne kuhusu mada isemayo, ‘Siku ya mnada.’
3. Ngonjera ni nini?
4. Fafanua kanuni za kutunga ngonjera.
5. Tunga ngonjera juu ya mada yoyote.
6. Ni mambo gani anapaswa kuyazingatia
mtunzi wa maigizo?
7. Tunga mchezo wa kuigiza kuhusu simba
aliyevamia kijiji chako.