Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi

Mtu akiandika barua ya maombi ya kazi

Kitaalamu Zaidi, Naweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi Kwa Tsh. 8,000/= tu. Barua Tsh. 3,000/= na CV Tsh. 5,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nami.
Umewekeza katika elimu yako, una kila sifa ya kupata kazi fulani lakini hupati kazi hiyo, inawezekana kabisa sababu mojawapo inayokufanya usipate kazi unayoitaka ni kutokujua kuandika barua ya maombi ya kazi.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiulizwa na wanafunzi na wasomaji wa mtandao wangu kuhusu jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi kwa kiswahili, na wengine huuliza kuhusu jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi kwa kiingereza. Wengine huomba kazi serikalini, wengine kazi za udereva, ualimu, udaktari na wengine kazi za uhudumu wa baa. Kazi zote siku hizi zinahitaji kuandika barua, hata kama unataka kujitolea, lazima utaandika barua!
Bahati mbaya ni kuwa, hata mtandaoni mifano inayooneshwa kuwa ni ya barua za maombi ya kazi mingi yake siyo sahihi, kila mmoja ana njia zake. Ni kama mashetani kila mmoja na mbuyu wake.
Barua ya maombi ya kazi huandikwa kwa malengo ya kuomba kazi. Kujifunza namna sahihi ya uandishi wa barua ya maombi ya kazi si kwamba utakusaidia katika kujibu maswali pekee, bali ujuzi huu utakufanya upate kazi halisi wakati utakapo hitaji kufanya hivyo.
Nakumbuka niliwahi kuitwa kufanya kazi katika kampuni ya global publishers kwa sababu tu, niliandika vyema barua yangu ya maombi ya kazi. Sasa nitakuelekeza yale unayotakiwa kuyafanya unapoandika barua ya maombi ya kazi. Jifunze taratibu ili baadaye uweze kuandika barua unayotaka na uweze kupata kazi.
Muundo wa Barua ya Maombi ya Kazi
i. Anuani ya mwandishi. Yaani anuani yako wewe unayeandika barua hiyo.
ii. Tarehe.
iii. Anuani ya anayeandikiwa.
iv. Salamu.
v. Kichwa cha habari.
vi. Kiini cha barua. Hii ni roho ya barua yako, ukikosea mahali hapa, kama unajibu swali katika mtihani, utapoteza alama. Na kama unaomba kazi halisi, utaikosa. Kiini kina aya nne:
Katika aya ya kwanza, eleza kazi unayoomba na mahali ulipoona tangazo la kazi hiyo. Ni katika sehemu hii unaweza kutaja umri wako.
Katika aya ya pili, eleza ujuzi wako kwa ufupi. Usieleze sana. Barua hii haipaswi kuwa ndefu kupindukia.
Aya ya tatu eleza kwa nini upewe kazi hii wewe na si mtu mwingine. Epuka kueleza shida zako binafsi ili upewe kazi. Maneno kama, ninaomba kazi hii ili niweze kumtibia mama yangu mgonjwa kitandani, hayana msaada.
Aya ya nne eleza uko tayari kwa usahili siku gani?
vii. Mwisho wa barua. Mwisho wa barua yako uwe na:
Neno la kufungia. Wako mtiifu. Wako katika ujenzi wa taifa n.k
Sahihi yako.
Jina lako
Wengine hujifunza kuandika barua ya maombi ya kazi ili waweze kujibu maswali katika mtihani, na wengine hujifunza ili waweze kuandika barua hizo, waweze kuomba kazi halisi. Vyovyote vile, mfano huu halisi wa barua, ni sahihi kwa watu wote, wanafunzi na wale wanaotafuta kazi.

Mfano huu wa barua ni wa barua ya maombi ya kazi ya ualimu. Hata hivyo, muundo huu unaweza kutumika katika kuomba kazi yoyote.

Pia, barua ya maombi ya kazi, huambatana na CV, hivyo utakapomaliza kujifunza jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi, tafadhali jifunze hapa jinsi ya kuandika CV.

Mtaa wa Kigogo
S.L.P 109,
DAR ES SALAAM.
0754895321.
18/10/2017.


Mkuu wa shule,
Shule ya sekondari Kigogo,
S.L.P 21494,
Dar es Salaam.

Ndugu,
YAH: OMBI LA KAZI YA UALIMU WA KISWAHILI NA HISTORIA
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24. Ninaomba kazi ya ualimu katika shule yako kama ilivyotangazwa katika gazeti la Raia Mwema siku ya Alhamisi tarehe, 23-10-2017.

Nimehitimu shahada yangu ya ualimu kwa masomo ya Historia na Kiswahili mwaka 2016 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia nimefanya kazi ya kufundisha kwa miezi saba katika shule ya wasichana Kandambili iliyoko Mbagala. Mbali na hayo, nina uwezo mkubwa wa kutumia kompyuta.

Uzoefu wangu wa kazi na elimu niliyonayo, vinanishawishi niamini kuwa, ninafaa kufanya kazi katika shule yako. Pia, ninaahidi kufanya kazi kwa bidii ili niweze kufikia malengo ya shule ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaofaulu na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaofeli mitihani yao.

Ninategemea majibu mazuri kutoka kwako na nipo tayari kwa usahili siku yoyote nitakayohitajika. Kwa uthibitisho zaidi, nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu.

Wako mtiifu,
Sahihi
Kilaza Pondaponda

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi kwa Lugha ya Kiingereza

Kassim Bingwe Somoye,

bingwe@gmail.com,

Tel: 0754 895 321,

IRINGA.

04/11/2020.                            

General Manager,

Barrick Mining Company,

P.O. Box 322,

MARA.

Dear Sir/madam,

 

APPLICATION FOR COMMUNITY RELATIONS OFFICER VACANCY

I am Tanzanian male aged 36 years old. I am applying for Community Relations Manager Vacancy as advertised by Barrick North Mara in November 8, 2020.

I have Bachelor Degree in Regional Development Planning, awarded from Institute of Rural Development Planning (IRDP) in 2012. Also, I have experience of working with: Christian Council of Tanzania and Africa Inland Church Diocese of Geita (AICT).

I believe that I possess the temperament and experience to excel in this position. Not only I am well organized but I have a passion for creating positive and productive work environments. As a Community Relations Officer I will: ensure implementation of the quick fix projects in a timely manner and according to the North Mara Gold Mine (NMGM) principles of engagement, establish appropriate partnerships with research institutions, government agencies, NGOs, specialists and others to implement this strategy, also I will envelop, in line with the NMGM principles as well as in collaboration with the community, a medium term (2 – 5 years) development plan and and all other duties relating to my rank.

I am ready for an interview any day you will need me. Also, I am enthusiastically looking forward to receiving a positive response from you. Enclosed are copies of my certificates.

Yours faithfully,

K. Somoye 

Kassimu Bingwe Somoye

Sasa nadhani umeona jinsi barua ya maombi ya kazi inavyoandikwa. Unaweza kuandika barua yako kwa mfumo huo niliotoa, hata kama ni kwa kiingereza, muundo unabaki kama huo hapo juu, tofauti ni lugha tu.

Kama umeona mifano wa barua hizo, lakini hutaki kuandika barua wewe mwenyewe, pengine hutaki kufanya kosa hata moja litakalosababisha ukaikosa kazi uitakayo, au labda inatakiwa barua ya kiingereza na wewe hutaki kuhangaika kuanza kutafuta maneno ya kiingereza, naweza kukuandikia barua. Bei ni ndogo na haifanani na bei zingine, barua peke yake ni sh. 3,000/= (elfu tatu tu), na cv peke yake ni sh. 5,000/=  (elfu tano tu).

Kitaalamu Zaidi, Naweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi Kwa Tsh. 8,000/= tu. Barua Tsh. 3,000/= na CV Tsh. 5,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nami.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Uhakiki wa Riwaya ya Takadini