Uundaji wa Maneno | Kiswahili Kidato cha Pili

Konsonanti na irabu.

Uundaji wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji, ujasiriamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.

Uambishaji ni nini?

Uambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno. Uambishaji hutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.
Mofimu zinazopachikwa katika mizizi huitwa Viambishi.

Aina za uambishi

Kuna aina mbili za viambishi;
Viambishi awali: Hivi ni viambishi vinavyo pachikwa kabla ya kiini/mzizi wa kitenzi. Kwa mfano anaimba, viambishi awali vya kitenzi anaimba -imba- ni a- na-
Viambishi tamati: Hivi ni viambishi vinavyopachikwa baada ya kiini/mzizi wa kitenzi. Kwa mfano kitenzi anacheza, kiambishi tamati ni a- inayotokea baada ya z-

Dhima za Mofimu

Mofimu ni neno au sehemu ya neno inayobeba maana maalumu ambayo ikigawanywa katika vipande zaidi hupoteza maana. Maneno haya ni mofimu: mama, punda, wali, bunge, huru, na, ta, li, na kalamu.
Aina za mofimu

1. Mofimu huru

Ni aina ya mofimu ambayo herufi zinazoiunda huleta maana kamili. Mfano: baba, mama, shangazi, amini, imani, wewe, redio na bendera.
Mofimu tegemezi
Ni aina ya mofimu ambayo herufi zinazoiunda hazileti maana kamili. Mfano: li, na, pik.

Zifuatazo ni dhima za mofimu:

1. Huonesha nafsi

Mfano: katika neno ninacheza, mofimu ‘ni’ inaonesha nafsi ya kwanza umoja.

2. Huonesha njeo (muda)

Mfano: katika neno alikuja, mofimu ‘li’ inaonesha wakati uliopita.

3. Huonesha urejeshi

Mfano: waliolala, mofimu ‘o’ inaonesha urejeshi wa watenda.

4. Huonesha ukanushi

Mfano: sikucheza, mofimu ‘si’ inaonesha ukanushi.

Mnyambuliko

Mnyambuliko ni namna ya kuunda neno jipya kwa kutumia neno la awali kwa njia ya kulirefusha zaidi.
Mifano:
Habari - habarisha
Sasa - sasisha
Piga - pigisha

Mazingira yanayosababisha mahitaji ya maneno mapya

Yapo mazingira yanayosababisha kuwe na uhitaji wa kupata maneno mapya. Mazingira hayo ni:

1. Sayansi na teknolojia

Kukua kwa sayansi na teknolojia ni sababu ya uhitaji wa maneno mapya. Hivyo mpaka sasa tuna maneno mapya ya sayansi na teknolojia. Maneno hayo ni kama: tarakilishi, luninga n.k

2. Elimu

Katika elimu kunahitajika maneno mapya kila siku. Kwa mfano, katika taaluma kuna tafiti na gunduzi mbalimbali hivyo, maneno mapya kwa ajili ya vitu vilivyogunduliwa huhitajika.

3. Uandishi wa habari

Waandishi wa habari wanahitaji maneno mapya ili waweze kuendana na kazi yao. Neno mubashara, limepatikana katika mazingira haya.

Dhima ya mnyambuliko wa maneno

1. Kurefusha maneno

Mfano: piga, pigia, pigiwa, pigika
Cheza, chezewa, chezeka.

2. Kuongeza maneno

Mfano: bora, boresha, boreshewa.

3. Kupanua maana ya maneno

Mfano:
Piga - kukutanisha vitu kwa nguvu.
Pigia - piga kwa sababu fulani.

4. Huzalisha kauli mbalimbali

Mfano:
Piga - kauli ya kutenda.
Pigiwa - kauli ya kutendewa.

Maswali

1. Eleza maana ya viambishi awali huku ukitoa mifano.
2. Eleza kazi tano za viambishi awali huku ukitoa mifano.
3. Onyesha viambishi awali vilivyomo katika maneno yafuatayo, kisha ueleze shina la kila kimoja:
A. Mlezi B. Tuliompinga C. Wanajivisha D. Hajasoma E. Umeshiba F. Amefika
4. Eleza maana ya uambishaji.
5. Fafanua dhima ya uambishaji katika lugha.
6. Nini maana ya viambishi?
7. Onyesha namna uambishaji unavyotokea katika aina mbalimbali za maneno.
8. Eleza kazi nne za mnyambuliko katika lugha ya Kiswahili.
9. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kaul nne kila moja:
A. Omba B. Shawishi C. danganya D. Unga
10. Eleza maana ya jozi za maneno yafuatayo:
A. Enea, eneza B. Changanya, Changanyikiwa C. Angua, angusha D. Someka, somesha E. Tengewa, tengana
11. Geuza kauli zifuatazo katika kauli tendana:
A. Mwalimu alimsaidia mzazi kubeba mzigo.
B. Amani itatokea tu ikiwa wanachi watawaamini viongozi.
C. Mwanachama ameamua kumshika mkono mwenzake baada ya ushindi.
D. Ni kweli kwamba, Ria atamshinda Ari kesho.
E. Mshtaki ameafiki mshitakiwa alipe faini.
F. Tunga sentensi yenye vitenzi vifuatavyo:
A. Gombana B. Rudiana C. Andikiana D. Tabiriana E. Ridhiana F. peana

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie