Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.
Tunaandika Mfano wa barua hii ya maombi ya kazi jeshi la magereza kwa sababu tumeshuhudia mifano mingi mtandaoni ambayo siyo sahihi na inawapotosha waombaji. Basi Mwalimu Makoba ili kuweka mambo sawa na ili kuwanusuru waombaji wasishindwe katika hatua za awali tu za barua, anakuja na mfano wa barua hii, ulio sahihi na unaokubalika kote.Jeshi la magereza limetoa nafasi za kazi kwa vijana wenye sifa. Kitu muhimu zaidi katika uombaji wa nafasi hizi ni barua ya maombi ya kazi. Kumbuka kwamba, barua ya maombi ya kazi ndiyo kipaumbele namba moja kitakachotumika katika kuchuja nani anafaa na nani hafai.
Katika barua yako ya maombi ya kazi, hakikisha barua yako inakuwa tofauti na barua za watu wengine. Hakikisha unaandika au anaandika mtu. Epuka kabisa kuandikiwa barua yako na akili mnemba (AI), kwani lugha ya akili mnemba inajulikana na itafanya maombi yako yasifanyiwe kazi.
Pia, endapo utatumia mfano wa barua hii tuliyoonyesha sisi, tambua kwamba, waombaji wengi watatumia mfano huu hivyo barua yako itafanana na watu wengine wengi, kwa hivyo nashauri uboreshe au uwasiliane nasi tukuandikie yako itakayosimama peke yake.
Katika uombaji wa kazi hizi za magereza, hakikisha kwanza una sifa zifuatazo: wewe ni Mtanzania, umri kuanzia miaka 18 na zaidi na uwe angalau na elimu ya kidato cha nne na kuendelea.
Katika barua yako hakikisha unaweka anuani sahihi, siyo namba za simu wala email, weka sanduku la posta, kama huna sanduku la posta, tumia la mtaa. Andika anuani sahihi huko unakoomba kazi, weka kichwa cha barua, na hakikisha barua yako ina aya nne ikifungwa na mwisho unaokubalika.
Zingatia mambo haya:
Unapoandika barua hii, nakushauri utumie lugha ya Kiswahili, kwani tangazo la kazi za magereza limeandikwa kwa Kiswahili.
Hakikisha uanuani unayoweka, ndiyo iliyotajwa kwenye tangazo. Hakiki anuani yangu kama inaendana na iliyopo katika tangazo, kama haiendani, weka inayoonekana katika tangazo.
Sasa tutazame mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Magereza
Serikali ya Mtaa Kambangwa,
S.L.P 98,
13/05/2024.
Kamishina Jenerali wa Magereza,
Makao Makuu ya Magereza
Barabara ya Arusha
Eneo la Msalato,
S.L.P 1176
DODOMA.
Ndugu,
Yah: OMBI LA KUJIUNGA NA JESHI LA MAGEREZA
Mimi ni mwanamume Mtanzania mwenye umri wa miaka 24. Ninaomba kujiunga na Jeshi la Magereza kama ilivyotangazwa katika tovuti ya Jeshi la Magereza na mitandao ya kijamii siku ya tarehe 15/08/2025.
Nina cheti cha elimu ya kidato cha nne, na nimesoma katika Shule ya Sekondari Kishapu na kuhitimu mwaka 2024.
Kutokana na sifa zangu kama: uaminifu, elimu, umri, afya njema ya akili na mwili na urefu unaotakiwa, ninaamini kuwa ninastahili kupata nafasi ya kujiunga na jeshi la magereza. Nipo tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya jeshi la magereza na nipo tayari kufanya kazi mahali popote nitakapopangiwa.
Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi.
Wako mtiifu,
___________
SAMWEL NATA DUNIA
Endapo utaandika katika mfano huu, basi una nafasi kubwa ya kuita katika usaili, hivi ndiyo inavyotakiwa kuandikwa. Tunakukumbusha tena, wengi wataandika kama ilivyo, hivyo basi hakikisha unabadili kidogo ili iwe ya tofauti, ukihitaji kuandikiwa nasi, wasiliana nasi ujipatie kazi iliyo bora, ya peke yako, isiyo fanana na barua ya mtu mwingine na uitwe katika usaili.
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.