Matokeo NECTA Kidato cha Sita 2026

Msichana anatazama matokeo NECTA kidato cha 6 mwaka 2026 katika simu yake.
NECTA Wametangaza matokeo ya kidato cha sita, wapo wanafunzi waliofanya vyema, lakini wapo wanafunzi ambao wameshindwa kufikia malengo yao.

Tazama Hapa Matokeo NECTA Kidato cha Sita 2026

Wanafunzi waliofanya vizuri tunawapongeza na kuwatakia kila la heri katika safari yao ya masomo yanayoendelea.

Wanafunzi waliofanya vibaya, wasikate tamaa, bado wana nafasi yakurudia mitihani yao. Tafsiri ya kufanya vibaya ni kushindwa kufikia malengo. Kwa mfano, mwanafunzi aliyekuwa na malengo ya kwenda chuo kikuu, pale anapopata chini ya D mbili, hujiona kama ambaye hajafikia malengo kwani anatakiwa aongeze D nyingine moja. Huu si muda wa kukata tamaa, bali ni muda wa kurudia tena. Mwanafunzi aliyepata C moja na E, huyo anahesabiwa kuwa na sifa za kwenda chuo kikuu hata kama hajapata D mbili.

Katika kurudia mitihani, wanatakiwa watambue kwamba, mtaala sasa umebadilika, vitabu ni vipya siyo vile ambavyo walisoma zamani.

Hata hivyo, masomo haya yanaeleweka vyema na yeyote anayetemaani kufaulu vyema anaweza kufanikiwa.

Pia, wanafunzi waliofanya vibaya watakapoamua kurudia mitihani yao, wahakikishe kwamba wanatambua makosa yaliyowafanya wakafanya vibaya katika mtihani huu na wasirudie makosa hayo.

Baadhi ya sababu zinazopelekea matokeo mabaya ni pamoja na: kutokusoma mada zote, kutokujipima kwa kufanya mitihani, kusoma peke yako kwa kuzani utaelewa mwenyewe bila mwalimu, wengine hufanya vibaya kwa sababu ya changamoto za kiafya, kukosa vitabu sahihi na sababu nyingine nyingi.

Kwa wanafunzi walifanya vizuri, wanaweza kuendelea mbele na elimu inayofuata kwa mfano vyuo. Madirisha ya kuomba vyuo pamoja na mikopo yamefunguliwa.

Kwa waliofanya vibaya, dirisha la usajili NECTA kwa watahiniwa wa kujitegemea limeshafunguliwa na wanaweza kujisajili.

Wanafunzi waliofanya vibaya au ambao wameshindwa kufikia malengo yao, tunawakaribisha kusoma nasi katika kitu chetu kinachopatikana Kinondoni Mtaa wa Kambangwa, Dar es Salaam. Ambao wapo mbali, wasihofu, tunayo huduma ya masomo  kwa njia ya online na wengi wanafaulu.

Kulingana na matokeo uliyopata, unaweza kujiunga katika group la WhatsApp la wanafunzi wetu wanaorudia mtihani kwa Kugusa Hapa

Popular posts from this blog

SMS 20 za Vichekesho Zinazochekesha Sana

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1

Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe