Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi TAKUKURU Ajira Mpya
Kundi la pili: ulinzi, ufundi wa magari, ujuzi wa udereva, huduma kwa wateja, msaidizi wa uhasibu, masomo ya ukatibu, fundi wa kompyuta na fundi wa mashine za ofisi.
Katika maombi haya, ni lazima uandike wasifu (CV) inayokubalika tena yenye wadhamini watatu, na ni lazima, uandike barua ya maombi ya kazi.
Hapa tunakupa mfano wa barua ya maombi ya kazi katika nafasi mpya za kazi TAKUKURU. Kwa sababu nafasi hizi ni chache na waombaji ni wengi, wengi watachujwa kwa kukosea kuandika barua pekee, hivyo, utakapoandika barua sahihi kama inayotolewa katika mfano huu, utakuwa katika nafasi nzuri ya kupata kazi hii.
Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
Mtaa wa Jamhuri,
S.L.P 1291,
1101 DODOMA.
Yah: OMBI LA KAZI YA MCHUNGUZI MSAIDIZI
Mimi ni mwanamume Mtanzania mwenye umri wa miaka 21. Ninaomba Kazi ya Mchunguzi Msaidizi kama ilivyotangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) siku ya tarehe 11/04/2026 katika tovuti ya TAKUKURU.
Nina ujuzi wa Udereva (Dereva Daraja C), ujuzi huu nimejifunza katika chuo cha VETA Shinyanga na kuhitimu mwaka 2025. leseni yangu ni halali nikiwa na rekodi safi ya udereva pamoja na uzoefu wa mwaka mmoja. Zaidi ya hayo, nina elimu ya kidato cha Nne niliyoipata katika Shule ya Sekondari Kishapu mwaka 2023.
Kutokana na elimu yangu, uwezo wa kufanya kazi nilionao pamoja na kuwa na sifa zinazotakiwa, ninaamini kuwa ninastahili kupata kazi hii. Endapo nitapata kazi ya Mchunguzi Msaidizi, nitafanya kazi kwa bidii na kutimiza majukumu yangu yote. Pia nipo tayari kufanya kazi wilaya yoyote ya Tanzania Bara.
Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi.
Wako,
______________
JUNIOR KINYAUNYAU PUSIKATI
Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi, Wasifu (CV), pamoja na Kukusaidia Kufanya Maombi ya Kazi Hizi Katika Akaunti Yako, Ili Kuwasiliana na Mwalimu, Gusa Hapa
