Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Jeshi la Wananchi JWTZ

Askari JWTZ
Jeshi la wananchi Tanzania limetangaza nafasi za kuandikishwa na jeshi hilo kwa vijana wenye baadhi ya sifa hizi: raia wa Tanzania, umri kuanzia miaka 18 mpaka 25 kwa kidato cha nne na sita na miaka isiyozidi 28 kwa wanaotoka vyuoni au elimu ya juu na awe na cheti cha jeshi la kujenga taifa kilichopatikana kwa kujitolea au kwa mujibu wa sheria.

kuandika barua inayokubalika, kutakufanya uitwe katika usaili huu wa nafasi hizi ambazo zina waombaji wengi.

Unapotuma maombi, anza na barua yako, Weka nakala ya kitambulisho chako cha NIDA ikifuatiwa na nakala ya cheti cha kuzaliwa, na vyeti vya shule, nakala ya cheti cha JKT, karatasi moja iliyoandikwa namba yako ya simu, kichwa cha habari kiwe, NAMBA YA SIMU YA MKONONI, halafu nenda posta kayatume maombi hayo katika anuani yao iliyoandikwa hapo kwenye mfano wa barua ya maombi JWTZ.

Huu hapa mfano wa barua ya kuomba kuandikishwa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ):

Mtaa wa Kambangwa,
S.L.P 1248,
KINONDONI, DAR ES SALAAM.
15/04/2026.

Mkuu wa Utumishi Jeshini,
Makao Makuu ya Jeshi,
S.L.P 194,
DODOMA, TANZANIA.

Yah: OMBI LA NAFASI YA KUANDIKISHWA JESHINI

Mimi ni mwanamke Mtanzania mwenye umri wa miaka 21. Ninaomba nafasi ya Kuandikishwa Jeshini kama ilivyotangazwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) siku ya tarehe 14/04/2026 katika tovuti na mitandao mbalimbali ya kijamii.

Nina elimu ya Kidato cha nne, nimetunukiwa cheti na ‘NECTA’ na nimesoma katika shule ya Sekondari Kishapu na kuhitimu mwaka 2025.

Kutokana na kuwa na elimu inayotakiwa, afya nzuri na akili timamu, tabia njema na nidhamu nzuri, ninaamini kwamba, ninastahili kuandikishwa Jeshini.

Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi.

Wako,

______________

MAGE KINYAUNYAU PUSIKATI

Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi ya Kuandikishwa JWTZ Itakayokufanya Uitwe Katika Usaili Ambayo Haitafanana na ya Mtu Yeyote, Kuwasiliana na Mwalimu, Gusa Hapa

Popular posts from this blog

SMS 20 za Vichekesho Zinazochekesha Sana

Jinsi ya kuandaa Somo na Kuwasilisha Oral Interview Ajira za Walimu

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi TAKUKURU Ajira Mpya