SMS 20 za Mahaba Makali Kumtumia Mpenzi Wako

Wapenzi wakitazama picha za mapenzi katika kamera.
Makala hii imeandikwa na wadhamini wetu:

Tunakuletea meseji kali za mahaba unazoweza kumtumia mpenzi wako na kumfanya awe na furaha muda wote. Meseji hizi za mahaba unaweza kuzituma kwa mpenzi wako muda wowote, unaweza kumtumia asubuhi, mchana, jioni na hata usiku. Meseji hizi, zitalifanya penzi lenu lizidi kuwa imara siku zote.

Meseji hizi za mapenzi unaweza kuzituma kwa njia ya meseji za kawaida, WhatsApp, na njia nyinginezo. Unaweza kutuma meseji moja kila siku. Kwa kipindi cha siku 20 tu, penzi lako litabadilika na kuwa bora mno.

1. Nimekuchagua wewe, ninafuraha kwamba na wewe umenichagua mimi.

2. Ninashukuru kuwa nawe, ninatabasamu, ninacheka na mara chache ninalia.

3. Mpenzi ninayejivunia, asante kwa kuwa bora kwangu siku zote.

4. Nina bahati kubwa kuwa katika mapenzi na wewe rafiki yangu. Nakupenda sana mpenzi.

5. Hakuna ninachotaka zaidi ya kukufanya wewe mpenzi wangu mwenye furaha siku zote.

6. Uzuri wako, akili zako na utu, vinanifanya nikupende kila siku.

7. Nakusalimia mpenzi wangu, siwezi kuacha kukufikiria muda wote mpaka nitakapokuona.

8. Kila siku ninapokuwa na wewe, najiona mwenye bahati.

9. Wewe ni mpenzi aliyekamilika kwangu, wewe ni kila kitu kwangu. Nakupenda.

10. Hakuna mwingine anayeweza kukupenda kwa viwango ninavyokupenda.

11. Ninahesabu kila siku ambazo niko mbali nawe, sitaacha kuzihesabu mpaka nilale tena mikononi mwako. Nakupenda.

12. Ni bahati kubwa sana kulala pembeni yako mpenzi wangu. Najivunia.

13. Nina furaha kuwa mimi ni wako.

14. Siku zinavyozidi kwenda, ndivyo ninavyozidi kukupenda.

15. Kuwa na wewe ni maamuzi ya busara sana kuwahi kuyafanya. Najivunia kuwa wako.

16. Upendo wako, msaada, ushauri na kila kitu, vimebadili maisha yangu. Asante kwa kuwa nami.

17. Hakuna anayenipa furaha zaidi yako. Nakupenda mpenzi wangu.

18. Kwako mpenzi wangu wa maisha, upendo wangu kwako hauishi daima.

19. Hakuna hisia za furaha kama kukukumbatia. Nakupenda mpenzi.

20. Sikuwahi kufikiria kama ingetokea siku nikapenda kama ninavyokupenda wewe. Ninakupenda sana mpenzi.

Ni matumaini yetu kuwa, SMS hizo, zitazidi kuliimarisha penzi lenu. Mapenzi ni kitu cha thamani sana tulichopewa sisi binadamu.

Dawa Kumfanya Mpenzi Akupende, Wasiliana na Mganga (Mdhamini) Wetu kwa Kugusa Hapa

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe