Nondo Zote za Kukusaidia Ufaulu Mitihani Usaili Walimu Masomo Yote
Vijana wengi wanaoomba ajira sasa wanaelekea kuamini mfumo hauko sawa, wanahisi kuna mchezo wanachezewa! Wanahisi pengine alama zile siyo zao na huenda matokeo yale yanatungwa sehemu.
Sikuliacha hivihivi jambo hili, niliamua kuingia katika utafiti mimi mwenyewe, kwa kuwa kigezo ni vyeti na umri na wala hawajali sasa unafanya kazi wapi nilijisajili, nikachaguliwa kufanya masomo mawili, mtihani wa kwanza nilipangwa kufanyia chuo cha Kampala International, na mtihani wa pili nilipangwa kufanyia NIT.
Kwa kuwa nilikuwa katika utafiti, nilijibu maswali yale tu ambayo nina uhakika wa asilimia 100 kuwa yalikuwa sahihi, maswali ambayo yalikuwa na utata sikuyajaza. Nilipotoka kwenye mtihani nilitambua kabisa kwamba lazima nipate alama fulani, matokeo yalipotoka, ilikuja alama ileile!
Hata hivyo, mtihani wa pili ulitofautiana kidogo, nilijibu maswali yale tu yaliyo sahihi kama kawaida, kwa kuwa maswali yapo 50, niliamini kwa idadi ya maswali niliyojibu, basi ningeweza kupata alama 88, hata hivyo ilikuja alama inayokaribiana na hiyo, lakini haigawanyiki kwa mbili!
Mtihani wa kwanza ulileta majibu sahihi, mtihani wa pili, ukaleta jibu lenye tofauti ya alama lakini inayokaribiana na alama ileile niliyotarajia, nikawaza kama mtihani una maswali 50, pengine sisi tunadhani kila swali lina alama mbili, nimepataje alama ambayo haigawanyiki kwa mbili? Jibu pekee hapa ni kwamba, huenda maswali yanatofautiana alama… ushauri, wangu ni kwamba, kwa kuwa ni maswali ya kuchagua, nashauri wakati mwingine, maswali yafanane alama!
Kwa utafiti huo, niligundua mitihani inasahihishwa kwa haki, na alama zinaendana na kile ulichojibu. Pia nilipata jibu la swali, kwa nini inaonekana kama hakuna haki? Yote hii ni kwa sababu, waombaji ni wengi na wanaochukuliwa ni wachache kwa hiyo kundi kubwa linabaki kuwa ‘not selected’ kumbe ‘not selected’ siyo kufeli, bali ni ufinyu wa nafasi tu. Kama umepata alama kuanzia 50, wewe ni mshindi!
Baada ya kujiridhisha kwamba mitihani inasahihishwa kwa haki na ukijibu vyema unapata haki yako, nikaandaa mambo ambayo yeyote anayetaka kuwa ‘selected’ lazima ayasome. Na vijana wengi wanaokuwa ‘selected’, wanapitia hatua hizo. Ukweli ni kwamba, wanaokuwa ‘selected’, wanajua wasome nini!
Mambo yatakayokufanya uwe selected
Jambo la kwanza kubali kusoma, tenga walau dakika 40 kila siku za kusoma pale tu usaili unapotangazwa. Usome nini? Ndiyo utata upo hapo, hata hivyo nitakuongoza hatua kwa hatua.
Hatua ya kwanza soma CT 100, hakikisha unakumbushia somo hili linalohusu utangulizi wa taaluma ya ualimu.
Hatua ya Pili jipime kwa kufanya maswali 50 yanayohusu hiyohiyo CT 100.
Soma Hapa Maswali ya CT 100 na Majibu Yake
Hatua ya Tatu soma maeneo 27 yanayoleta alama nyingi katika mitihani ya usaili walimu.
Soma Hapa Maeneo 27 Yanayoleta Alama Nyingi
Hatua ya Nne, soma EP, hata hivyo wekeza nguvu kubwa kuwasoma wanasaikolojia 10 wa lazima ambao wanatoka sana katika mitihani.
Soma Hapa Wanasaikolojia 10 wa Lazima Wanaotoka Katika Mitihani
Hatua ya Tano, measurement and evaluation ni sehemu muhimu mno kwa mwalimu kuifahamu, hapa, jipime kwa maswali 100 yanayohusu mada hiyo.
Soma Hapa Maswali 100 Measurement and Evaluation
Hatua ya sita, sasa soma mtihani halisi ulivyo. Mtihani halisi unatoa maswali yanayohusu taaluma ya ualimu, kompyuta, akili mnemba na hesabu nyepesi.
Soma Hapa Maswali 100 Kujiandaa na Mtihani Masomo Yote
Mpaka hapo utakuwa upo vizuri kabisa, kwa wale wa Kiswahili, mtihani unatoka kwa lugha ya Kiswahili hivyo hakikisha pia kama unasomo hilo tazama mfumo wa mtihani wako.
Soma Hapa Maswali 100 ya Kujiandaa na Usaili Somo la Kiswahili
Hivyo ndivyo walimu wanaofaulu mitihani hii ya usaili wanavyosoma mpaka wakafaulu. Wanaofaulu, wanabahati ya kufahamu wasome vitu gani, ukisoma mambo ambayo yanafanana na yanayotoka, unakuwa na nafasi nzuri ya kupita katika mitihani yako.
Ili Kujipatia Nondo Zote za Kukusaidia Ufaulu Mitihani ya Usaili Hatua kwa Hatua Wasiliana Nami kwa Kugusa Hapa
