Maswali 100 ya Kujiandaa na Usaili Walimu Somo la Kiswahili

Mwanaume na mwanamke katika mitihani ya usaili walimu kiswahili
Katika mitihani ya usaili walimu, maswali haya ni msaada mkubwa. Kwa kuwa muda wa kusoma kila kitu hautoshi, maswali haya hutumika kama njia nzuri zaidi inayomfanya mwalimu apate kila kitu kwa muda mfupi na kumsaidia awe ‘selected’ kwenda ‘oral interview’ katika mitihani hii yenye ushindani mwingi.

1. Katika kompyuta, ukibonyeza alama ctr+A unapata nini?

A. Unafuta maandishi yote yaliyochaguliwa.

B. Unachagua (highlight) maandishi au mafaili yote.

C. Unahifadhi (save) kazi uliyokuwa unafanya.

D. Unafungua faili jipya la kazi.

Jibu: B

2. Juma amewasha kompyuta yake, lakini anagundua kwamba, kila akicheza mziki, sauti haisikiki, afanye nini kama suluhisho?

A. Kununua spika mpya za kisasa zaidi.

B. Kufuta nyimbo zote na kuziweka upya.

C. Kukagua kama sauti imewekwa "Mute" au kama kadi ya sauti ina hitilafu.

D. Kuzima kompyuta na kutofanya kazi yoyote.

Jibu: C

3. Program ya akili mnemba inayohusika na utengenezaji wa picha inayomilikiwa na kampuni ya google inaitwaje?

A. Midjourney

B. Stable Diffusion

C. Imagen (au Gemini)

D. DALL-E

Jibu: C

4. Mshindani mkuu wa Chatgpt ni?

A. Microsoft Word

B. Google Gemini

C. Adobe Photoshop

D. WhatsApp Business

Jibu: B

5.Kuku wangapi wanatakiwa kukamilisha idadi ya miguu 200?

A. Kuku 50

B. Kuku 400

C. Kuku 100

D. Kuku 20

Jibu: C

6. Ni namba gani inayofuata katika mfululizo huu wa namba?

2, 4, 8, 16, 32, ___

A. 40

B. 64

C. 48

D. 50

Jibu: B

7.Taja madhara ya mwalimu kutegemea akili mnemba katika kutengeneza nukuu za kufundishia darasani.

A. Inasaidia mwalimu kuwahi darasani kwa wakati.

B. Inaweza kusababisha kutoa taarifa zisizo sahihi au zenye makosa ya kitaaluma (Hallucinations).

C. Inafanya wanafunzi wapende somo zaidi kuliko mbinu za zamani.

D. Inapunguza gharama za kununua vitabu vya kiada.

Jibu: B

8. Ni kipi kinaifanya akili mnemba iwe kama unaongea na mtu halisi

A. Uwezo wa kompyuta kufanya kazi kwa haraka sana (Processing Speed).

B. Uchakataji wa Lugha Asilia (Natural Language Processing - NLP).

C. Matumizi ya betri kubwa zinazodumu kwa muda mrefu.

D. Kuwepo kwa picha nyingi kwenye mtandao wa internet.

Jibu: B

9. Ni nani baba wa akili mnemba duniani?

A. Bill Gates

B. John McCarthy

C. Elon Musk

D. Mark Zuckerberg

Jibu: B

10. Ikiwa umri wa sasa wa mwalimu ni miaka 25, na umri wa mwanafunzi wake ni nusu ya umri wa mwalimu, mwanafunzi atakuwa na umri gani mwalimu atakapofikisha miaka 40?

A. Miaka 20

B. Miaka 27.5

C. Miaka 30

D. Miaka 32.5

Jibu: B

11. Dai la ushairi wa Kiswahili kutokana na fasihi ya Kiarabu na Uislamu limebainishwa vizuri sana katika andiko la

(a) Harries

(b) Knappert

(c) Mulokozi

(d) Samwel

Jibu: A

12. Fasihi ya ushairi wa Kiswahili imegawanyika katika makundi mawili: fasihi ya kimapokeo na fasihi ya kisasa. Miongoni mwa wafuasi wa usasa nchini Tanzania ni pamoja na:

(a) Euphrase Kezilahabi, Mugyabuso Mulokozi, Kulikoyela Kahigi na Kithaka wa Mberia

(b) Euphrase Kezilahabi, Mugyabuso Mulokozi, Kulikoyela Kahigi na Jumanne Mayoka

(c) Euphrase Kezilahabi, Mugyabuso Mulokozi, Kulikoyela Kahigi na Saadan Kandoro

(d) Euphrase Kezilahabi, Mugyabuso Mulokozi, Kulikoyeyela Kahigi na Tigiti Sengo

Jibu: D

13.  ______________ ni unyume unaotokea pale ambapo leksimu moja huwa ni kinyume cha leksimu nyingine kutegemeana na uelekeo.

a) Unyume kamilishani,

b) Unyume kadilifu,

c) Unyume wa kiutoano,

d) Unyume elekeani

D

14. Mahusiano ya kiwima ni yale yanayohusu neno kubadilishana nafasi na neno jingine bila kupoteza maana. Kwa mfano: Huu ni msimu wa mavuno. Hiki ni kipindi cha kupanda/upandaji. Neno ‘hiki’ na ‘huu’ katika sentensi hizo yamebadilishana nafasi ambapo yote ni:

a) Vivumishi,

b) Viwakilishi,

c) Vielezi,

d) Vihusishi

A

15. Uhusiano wa kimlalo kwa jina jingine hujulikana kama uhusiano wa:

a) kisilisila,

b) Paradigmatic,

c) Sintactic,

d) wima.

A

16. Chimbuko la mihtasari ya Kiswahili Msingi na Sekondari (2005) limetokana na:

a) Sera ya elimu na mafunzo ya 1995

b) Malengo ya elimu Tanzania

c) Malengo ya kufundisha Kiswahili

d) Marekebisho ya mihtasari iliyotangulia

A

17. Dhana mojawapo katika mada ya utungaji ni:

a) Kuandika kwa ufasaha

b) Kuzingatia yaliyomo

c) Kuelewa yaliyomo

d) Kujieleza kwa ufasaha

D

18. Uchaguzi wa mada katika utekelezaji wa muhtasari ni hatua muhimu kwa sababu:

a) Mada zote lazima zichaguliwe

b) Ya upungufu wa vifaa

c) Ya kuthibitisha ufundishaji wake

d) Muhtasari una mada nyingi

D

19. Msingi wa kuwa na hamu ya kujieleza katika utungaji unaweza kutekelezwa kwa:

a) Kuandaa zana husika

b) Kuwa na jambo la kujieleza

c) Kukusanya na kuchagua mawazo

d) Wanafunzi kuwa na mwamko wa utungaji

B

20. Mwalimu Amiri amefundisha uandishi wa Barua Rasmi kwa kuwapa wanafunzi wa Kidato cha Nne Tangazo la Kazi mbalimbali kisha wao waandike barua za kuomba hizo. Mwalimu Amiri alitumia mbinu ya:

a) Vielelezo

b) Kanuni

c) Mawasilisho

d) Mazingira

A

Jipatie Maswali Yote 100, Yakusaidie Katika Kujiandaa na Mtihani Wako, Wasiliana na Mwalimu kwa Kugusa Hapa

Popular posts from this blog

Wanasaikolojia 10 Lazima Kuwasoma Wanatoka Mitihani ya Usaili Walimu

Maswali 100 Usaili Ajira za Walimu | Measurement and Evaluation

SMS 20 za Vichekesho Zinazochekesha Sana