SMS 20 za Vichekesho Zinazochekesha Sana
1. Huu mwezi mwenye nyumba aje atoe nyumba yake kwenye vitu vyangu, sina kodi.
2. Nimetoa vyombo nje nifanye usafi, kurudi naambiwa gari la taka limebeba.
3. Kwa jinsi maisha yalivyo magumu siku hizi unajikuta wewe ndiyo unamuamsha jogoo.
4. Chakula chenyewe unakipata kwa mateso halafu bado unakiwekea pilipili, una tatizo gani mkuu?
5. Mtu anakuja kuniomba elfu 20 kweli! Unaniombaje nusu ya utajiri wangu?
6. Daktari: Bia inatanua moyo.
Walevi: imeshindwa kutanua chupa itatanua moyo?
7. Nimeota nakula tambi, kuamka sizioni "earphone" zangu.
8. Taja faida kwa nini unaishi peke yako. Hakuna wa kuniuliza kwa nini pazia nafutia sahani.
9. Leo mwizi kapigwa mpaka kasema, "mawe yanauma, nipigeni makofi.”
10. Hasira mnatoa wapi wakuu, fikiria mtu anaua kipepeo.
11. Bongo movie imenishinda. Malaika katoka mbinguni kavaa jezi ya Yanga!
12. Siku hizi sijali, ukiniita mbwa nabweka naondoka zangu.
13. Sitasahau ile siku nilikabwa na vibaka nikawaambia mimi sina kitu, wakaniambia basi toa ziwa tunyonye!
14. Mnaosema fundi mkweli kinyozi fikirie i mara mbili: jana nimenyoa kipara, kinyozi kachovya kitambaa kwenye maji ya moto kikamshinda kukishika akakirushia kwenye kichwa changu.
15. Maombi ya mtu ambaye mahusiano yake ya kumi yamevunjika utasikia, "Baba ni mimi tena mbele yako."
16. Nipo nawaza tu hapa. Au nishinde bila nguo kikulacho kife na njaa.
17. Unajitahidi usichepuke, kumbe wewe ndiyo mchepuko.
18. Sitasahau Christmass mzee alinunua utumbo kilo 20, aisee tulikula mpaka mwingine tukavaa shingoni kama cheni.
19. Acha nijitume watoto wangu wasinitoe kafara, hiki kizazi kinachokuja siyo kizuri hata kidogo.
20. Hata leo hakutoi 'out' mahusiano yako magumu sana.
Ni matumaini yetu kuwa, vichekesho hivi 20, vimekuchekesha na kukufanya mwenye furaha. Vichekesho hivi huwekwa mara kwa mara, hivyo hakikisha unatembelea mahali hapa kila unapotaka kucheka.
Sms za vichekesho, vichekesho vunja mbavu, meseji za kuchekesha na vichekesho vya kila aina, hapa ndiyo nyumbani kwake. Pia, tunavyo vitabu vya vichekesho vinavyouzwa kwa bei nzuri kabisa. Kama lengo ni kufurahi, basi mahali hapa ndiyo penyewe.
Kucheka ni Afya, Nunua Kitabu cha Vichekesho vya Kiswahili kwa Tsh. 5,000/= tu, Ucheke Siku Nzima, Ili Kununua, Gusa Hapa
