JAZA UJAZWE! UPEMBA MWINGI NA TAFSIRI ZA KIMOMBASA
Lugha ya Kiswahili ina maneno lukuki ambayo kama hutakuwa makini katika uchaguzi utaibua sintafahamu na mishangao kwa watu! Hata kabla ya ‘jaza ujazwe,’ neno ‘tigo’ peke yake lina maana nyingine mbali na maana yake! Ama hakika, muhusika wa kitengo cha matangazo kutoka kampuni ya ‘tigo’ atakuwa amefanikiwa sana kuitangaza biashara na ofa hii mpya ya kampuni yake. Lakini mbali na faida hiyo, kuna ukakasi mkubwa ambao umetanda miongoni mwa watu hasa wanaotambaa na maana ya ziada. Wengi hususani wanaume, wanaona neno hili si zuri kutumika na linawadharirisha. Makampuni ya simu yamekuwa na tabia ya kuigana kila inapotokea kampuni mojawapo ikaja na ubunifu wa kuvutia. Lakini katika hili makampuni pinzani bado yako kimya, hakuna aliyejibu mashambulizi haya. Kinacholeta ugumu ni kupata maneno yasiyo na ukakasi. Jekejeke litatokea endapo makampuni mengine yatakuja na misemo hii: CHOMEKA UCHOMEKWE, TIA UTIWE, WEKA UWEKWE, NYONYA UNYONYWE, GEUZA UGEUZWE, LAINISHA ULAINISHWE na mengine mengi y...