VICHEKESHO VILIVYOTUFIKIA WIKI HII

Leo tupo kwenye Taxi tunaelekea Mjini Traffic akasimamisha gari letu, akamuuliza Dereva "Mbona plate namba za nyuma na mbele ni tofauti !?. Dereva akamjibu, 'Kwani ww sura yako na makalio yako vinafanana !?.
Wote tukaanza kucheka ...
Tumepandishwa kwy defender lao nadhani wanatupeleka kupata lunch !
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
XXX
πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€’
IVI KWA MFANO MKEO
AKIWA NA KICHWA KIKUBWA KULIKO WW
BADO TU UTAITWA KICHWA CHA FAMILIA?
🀣🀣🀣🀣🀣
XXX
......... Jaman Hivi hakuna Mtu yeyote Mwenye *Picha* ya *WAHENGA*   Anitumie Mimi Nawaskiaga Tu Cjawahi kuwaona
   πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
XXX
 Ile siku nitaona mwanamke akiskuma
mkokoteni bila shati.....ndio nitaamini
kuwa #what_a_man_can_do_a_woman_can_do_better πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Wacha niende hivi narudi baadae
πŸƒπŸΌπŸƒπŸΌπŸƒπŸΌπŸƒπŸΌ
XXX
 Mdada:- beby nimefukuzwa kwetu
Jamaa:- maskini pole
Mdada:- Hapa Hata sijui ntafanyeje
Jamaa:- panda Gari za mbagala zinazopitia Tazara ulale kwenye FoleniπŸƒπŸΎπŸƒπŸΎ
XXX
 Mwalimu: *Alex, simba akianza kukufukuza utafanya nini?*
Alex: *nitapanda juu ya mti.*
Mwalimu: *je na simba nae akipanda juu ya mti?*
Alex: *nitakimbilia mtoni niogelee.*
Mwalimu: *je simba nae akikufuata mtoni?*
Alex: *mwalimu uko upande wangu au wa simba? Maana* *sikuelewi kabisa, kila ninavyojaribu kumkwepa* *simba we unamwelekeza niliko, kama hunipendi sema tu.*
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
XXX
 *Binti anakula chapati tano na maharage robo harafu ww bado unamuita baby huyo ni brother*
 C & P
XXX
 Kama hujawahi kupata 100% ulipokua Shule ya msingi, na Secondary, basi tambua kuwa 100% pekee ambayo utaweza kuiona maishani mwako ni pale simu yako ikiwa imejaa chaji 100%.😁😁😁😁😁😁😁
XXX
 *BABA*: mwanangu mbona skuizi wapenda niita DAD badala ya BABA
*BINTI* : kuita baba kunamaliza lipstick.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
XXX
 *nahitaji msaada wenu jamanii..*

nipo hapa ubungo nataka kwenda China kumsalimia Jack Chan.., nipande gari za wapi..!!!??
XXX
Nawapenda Sanaa wanawake wa uswahilini kwa ubunifu wao. Hivi ni baadhi ya vicheko walivyo Cheka kwenye miaka tofauti.
2002 to 2004- walikua wanacheka "hehehe haloooo"
2005 to 2007- wakaja Na "hehehe utajiju"
2008 to 2010- wakaleta hii ya "hehehe unalooo"
2010 to 2012- wakaleta "hehehe utajibeba"
2012 to 2014- wakaja Na "hehehe kaoge"
2014 to 2015- SAFARI hii hapa wakacheka "hehehe chezea mie wewe"
2016- hapa sasa ndo wamekuja Na ..... Hehehe kantangazeeeeee
2017- wamekuja Na hii hapa "hehehe warere wapi nyonyoo. 

Jee una hisi 2018 watabuni style gani ya kucheka πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
XXX
 *kumbukumbu ya kusikitisha*😭😭

*Tarehe kama ya leo miaka mitano iliyopita muuza karanga alikimbia na chenchi yangu*
πŸ˜‰πŸ˜‰
XXX
 NIKIWA SHULE MWALIMU WANGU WA KISWAHILI ALINAMBIA "MTU MWENYE MKONO MREFU MAANA YAKE NI MWIZI"
SASA KUNA WAKATI UNASIKIA VIONGOZI WANASEMA..MSICHEZE NA SERIKALI MAANA SERIKALI "INA MKONO MREFU"
*YAANI HAPO NDO NASHINDWAGA KUELEWA NDUGU WATANZANIA*πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
XXX
 Kama hujawahi kuongea Kichina basi hii ni nafasi pekee ya
kufanya mazoezi.....,......rudia kwa haraka haraka ...
"MY SHOE SHALL SOON SHINE"
Tuma audio please angalau tucheke kidogo.....
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
XXX
 *Jamaa yupo kwenye daladala pembeni kuna mrembo mkali kakaaa.Akamlia timing afu akamuuliza*
   jamaa:Samahani dada hivi unaitwa "Google"
    Demu:hapana..kwa nini?!
    jamaa;Una kila kitu ninachokitafuta.
   πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜…πŸ˜€πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›
XXX
 *Maisha yamekaza hadi unamuuliza mkeo kama ana boyfriend awakopeshe hela?  Na stress ni pale anapokujibu kwani ulikuwa unataka kiasi gani  nimuulize?
...napita tu...πŸ™„πŸ™„πŸ™„
XXX
 *Wanyama wangekuwa na WHAT'S UP.*
Status zingekuwa:

MENDE: "nimekoswa na guu la mama mwenye Nyumba, maisha yangu mashakani, why always me???? "

PANYA: "nimekula nguo lenye pafyumu, nasikiaje kiu. uwiiiii"

NGURUWE: Binadamu wabaya jamani, wameshanizushia nasambaza mafua "

MBU: Nina HIV, nimekomaje kunyonyanyonya hovyo.

MBUZI: teh teh teh. thank Good pasaka imepita. ni kula BATA tuu mpaka EID.

KUKU: "friends mkiona kesho kimya mjue nipo mezani maana kuna wageni wamekuja leo hapa home, tuombeane uzima wapendwa, love you all"πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
XXX


*πŸ˜‚Enzi hizo shule  kuna wanafunzi  walikuwa wanaandika topic kwa kalamu nyekundu, sub topic kalamu ya nyeusi,  na notes kalamu ya bluu.πŸ˜‚ Sijui mko wapi siku hizi, au mlipata kazi sadolin?*

πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ
XXX
 *boy* : *baby* *nataka* *niwe* *pirot*
*girl* : *acha* *tu*
*boy*: *kwanini* *unasema* *hivyo*
*girl* : *yani* *umeshindwa* *kulusha* *vocha* *utaweza* *ndege* πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’

*girls* *shikamooo*
XXX
 Bwana alikua ameketi na wake zake wawili sitting room waangalia TV pamoja. Akawa anasikiu kiu lakini akaona ni hishima kumtuma yule bibi mdogo. Alipokua amekwenda kuleta hiyo glassi ya maji, bibi was kwanza akaanza;

"Sasa ndio wanionesha nini! kama ni maji basi sote twajua kuteka. Ama wataka kumwangalia mwendo tu akenda na akirudi kuni dhalilisha mimi. Sawa lakini mungu yuko, dhalimu mkubwa wewe huna uadilifu mwanamume wewe basi tu"😳

Bibi mdogo akirudi na glassi yake ya maji nae akaanza;

"Haya musha zungumza hiyo siri yenu! najua uliku waniondoa ki hikima mupate kunisengenya lakini inshallah mungu atawashinda na dhulma zenu hizo"😳

Heri angebaki na hio kiu yake maskini
πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£
XXX

XXX

```Je, wajua...```?
*Katika maisha yake yote ya _Adolf Hitler_* *hakuwai kusema neno Ahsante na yote hii ni kutokana na kutojua kuongea kiswahili*
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
_Sio lazima tuelewane bhana_
Vichekesho hivi vyote vimechukuliwa kutoka mtandao wa WhatsApp. kwa bahati mbaya watunzi wake wengi hawafahamiki kwa sura wala majina.Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie