PROFESA MUHONGO ANAVYOTESWA NA NAMBA 24
January 24, 2015, Profesa huyu mwenye bahati
mbaya, alijiuzuru wazifa wake kutokana na sakata la Tegeta Escrow.
May 24, 2017, Muhongo analeta utata. Kwanza
naiona barua ya Mheshimiwa Rais ikisema kuwa, uteuzi wake umetenguliwa ama kama
wasemavyo watoto wa mjini, barua ile ilibeba tamko la kumtumbua mzito huyu. Lakini
baadaye naiona barua ya Profesa Muhongo mwenyewe akitangaza kujiuzuru huku akiwa
tayari amekwisha tumbuliwa! Kama sikuchanganya mambo, basi hii ni ajabu.
(KICHEKO).
Cha kushangaza ni kwamba katika mara zote
alizoondoka madarakani kwa zahama, aliondoka tarehe 24. Kuna nini katika hii
tarehe 24?
Kwa imani aliyonayo Muhongo, namba 24 ina maana
kubwa. Namba hii ina uhusiano na masuala ya kumtumikia Mungu hususani katika
hekalu. Hivyo rafiki yangu Profesa huyu achague kilinge chochote kinachomfaa
katika shughuli za utumishi wa Bwana, kama ataamua kulihubiri neno kwa imani ya
Kirastafari, Budha, Hindu, Dini ya Afrika ya Jadi n.k, basi afanye hima kabla
hajachelewa. Kwa wakristo, hekalu lilihudumiwa na watumishi wa Bwana 24, ambao
ni, 1) Jehoiarib; 2) Jedaiah; 3) Harim; 4) Seorim; 5) Malchijah; 6)
Mijamin; 7) Hakkoz; 8) Abijah; 9) Jeshua; 10) Shecaniah; 11) Eliashib; 12)
Jakim; 13) Huppah; 14) Jeshebeab; 15) Bilgah; 16) Immer; 17) Hezir; 18)
Happizzez; 19) Pethahiah; 20) Jehezkel; 21) Jachin; 22) Gamul; 23) Delaiah; 24)
Maaziah. Pia kitabu cha Mtakatifu Luka, kina jumla ya sura 24. Namba hii haiko
katika siasa. HAIKO.
Profesa Muhongo alidondoka, akajizoazoa! Kadondoka tena, hawezi
nyanyuka, labda awe mhubiri.