BONDIA MSOMI KUTOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, ASEMA YUKO TAYARI KWA PAMBANO.


Goodluck Elisaria, bondia machachari wa uzito wa 'featherweight', mwanafunzi wa mwaka wa tatu kutoka ndaki ya COHU anayekiwakilisha Chuo Kikuu Cha Dar es salaam katika ulimwengu wa ngumi, sasa amethibitisha rasmi kupanda tena ulingoni kukipiga na mpinzani wake Vasco Maklin.
Maamuzi haya yanakuja baada ya Saria kupona jeraha lake alilolipata siku ya tarehe 07/05 mara baada ya kutokea ajali ya kugongana vichwa akiwa ulingoni hali iliyopelekea pambano hilo lihesabike kama suruhu 'technical draw'.
Bondia huyu ambaye hajawahi kupigwa, kule Congo alifanya mambo makubwa wakampa jina la 'SariaMundende'. Hapa Tanzania tunamwita  'SariaZege'.
"Nitampiga Maklin katika raundi ya kwanza, kisha nitakwenda chuo kufanya test nikiwa ninatabasamu kwa ushindi!" Alisema SariaZege.
 KILA LA KHERI SARIA. WAPIGE!!
Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Kirafiki

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie