SAFARI YA KUUSAKA MWEZI (sehemu ya nane)
Looh! Sikuamini, niliiona Mapandagila 214 ikiwa imeegeshwa mbali kidogo, niliruka kwa furaha nikamkumbatia Chokusi, akanikwaruza ubavuni kwa vile vyuma vyake, sikuhisi maumivu. Lakini tena nikakumbuka jambo, nikauliza. “Lakini nilipodondoka iliharibika kabisa… nitawezaje kupaa tena?” “Niliitengeneza… kwa sasa iko vizuri na itakufikisha salama huko uendako.” Nilimkumbatia tena kwa furaha, lakini kabla sijamwachia, akanipiga mweleka, wote tukalala chini. “Askari wanakuja na makombora, wamekwishagundua kuwa umetoroka, tambaa mpaka katika ndege yako, usinyanyue kichwa wala kugeuka nyuma, kwa heri. Chokusi alirudi katika shimo haraka, mimi nilitambaa kama nyoka kuelekea ilipokuwa Mapandagila 214, nikayasikia makombora mazito yakirushwa, nikakaza mwendo. Kombora ...