TATHMINI YA WAGOMBEA NAFASI YA URAIS-DARUSO (UDSM)

Anaandika Makoba Daud

Japokuwa Wagombea wote wamepitishwa na kamati ya wapiga ramli, tena wagombea hawana mvuto kuanzia sera mpaka majina yao, hatuwezi kususa kabisa kuutazama uchaguzi na mwenendo wa kampeni zao.

RICHARD
Anatilia mkazo suala la kusoma mapato na matumizi ya DARUSO.

Pia anahoji uhalali wa kulipa nauli katika mabasi ya CRDB.

Amekopa hoja ya Charles William ya kuwalipa posho ma CR.

CHANGAMOTO
Wakati wa uzinduzi wa kampeni, hakupata kusikilizwa na watu wengi japo alijieleza vizuri. Kuna mpinzani wake alicheza mchezo mchafu wa kuwatoa watu nje ili kupunguza upinzani.

Pia Hatajwi sana katika mitandao ya kijamii.

*Siku hii ya mwisho, anaonekana kuanza kukubalika na watu wengi. Hivyo ashone suti nyeusi, huenda akawa raisi.

EMANNUEL
Anataka kuirudisha DARUSO kwa wana DARUSO. Anadai yeye sio kiongozi wa kujikombakomba na kujipendekeza.

Amekopa hoja ya Shamira Mshangama inayotaka Dean afanye kazi ya kushauri wanafunzi na si vinginevyo.

CHANGAMOTO
Watu hawana imani naye kwa sababu ni kada wa waziwazi wa CCM, tena aliyegombea cheo kidogo akashindwa.

Pia, Kamati yake ya kampeni inalaumiwa kuendesha sera za ukoleji.

*Hata hivyo anazungumzwa sana katika mitandao ya kijamii. Hii ni faida kwani watu wengi watamfahamu. Bila shaka yoyote, ang'arishe viatu vyake, huenda akawa rais.

JEREMIAH
Anasema, serikali yake itawapa wanafunzi uhuru wa kuhoji mambo mbalimbali bila kuingiliwa wala kufukuzwa. Anasisitiza kwamba, endapo atashindwa kutimiza yale aliyowaahidi wanaDARUSO, yuko tayari kuondolewa.

CHANGAMOTO
Tamaduni za ndaki ya COET zisizoruhusu mtu yeyote asiyemhandisi kupanda katika kimbweta ili kuhutubia, huenda zikaamsha hasira kwa watu wa ndaki zingine kwa kujihisi wamedharauliwa na hivyo kumnyima kura.

Pia, Inasemekana ni kada mwaminifu wa CCM, lakini anaonekana kuwahadaa wanaDARUSO kuwa yeye ni mpinzani. Uongo kama huu, ukishindwa kumfaidisha, utamwangusha.

Pia, Anaungwa mkono na viongozi wengi wa serikali dhaifu iliyopita. Huenda watu wakadhani hana jipya kwani naye alikuwa mmoja wa serikali hiyo.

*Nguvu kubwa inayotumiwa na wafuasi wake, mabango mengi yaliyotapakaa kila mahali, na utekaji mkubwa wa mitandao ya kijamii, unafaida kubwa kwake. Hivyo basi, apige pasi suti yake, huenda akawa rais

#Makoba


Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2023

Uhakiki wa Riwaya ya Watoto wa Maman’tilie