Vita ya Bwana Makani na Utamu Korea itakavyokuwa

Kwanza hakuna anayeombea mpambano huu utokee, kwani vita hivi vitakuwa na madhara kwa dunia nzima. Makala haya yanalengo la kuchochea amani. Wengi wetu tunaomba yaendelee kuwa ni maneno kama siku zote! Ila kama wataamua kupigana basi pambano litakuwa hivi.
Bwana Makani atarusha kombora kali kwa kutumia kifaru cha aina yake kitwacho ‘Karl Great’. Kombola hilo lisilo na macho litaipiga ‘Utamu Korea’, Kimung’unya mzee wa kiduku kitengo mawe, ataliamsha dude, kwa kutupa kombora hatari linalotembea katika kifaru ambacho hupita katika reli yake, sio kingine ni ‘Schwerer Gustav and Dora’.
Hapo sasa vita vitakuwa vimenoga, wanajeshi wa pande zote kutokana na uzito wa makombora hayo hawatatumia silaha ndogo, watabeba ‘RPG-71’ silaha hii kwa urefu wake inaitwa (Ruchnoy Protivotankovyy Granatomyot), sisi wataalamu wa mambo haya huwa tunaiita ‘ant – armor’ yaani huwa inasambaza chochote. Ikikohoa hii haina kusema ‘gari lile la fulani huwa halipitishi risasi wala mabomu’, hii huwa inabomoa tu.
Kama kawaida Utamu Korea atatishia kutumia kombora la nyuklia ‘B53’, kitisho hiki kitasababisha Bwana Makani ashambulie haraka kwa kutumia dhana ya hatari sana iitwayo ‘MOAB/GBU-43/B Massive Ordinance Air Blast’… mimi huwa naiita ‘fukufuku zamisha’ kwani ikiachiwa inauwezo wa kuharibu majiji tisa kwa kipimo cha radius ya 137.61 m.
Vita vikifikia hapo, Utamu Korea atajibu kwa kumrusha ‘king of bombs’ Tsar Bomba. Hatua hii itafungulia matumizi ya nyukilia kwa pande zote mbili. Madhara yake yatakuwa ni makubwa sana kuwahi kushuhudiwa na dunia hii.
Wito wangu, lazima tuombe kila mtu kwa dua yake – BALAA HILI LISITOKEE.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu