Mtihani wa Kiswahili NECTA Kidato cha Nne 2025 Maswali na Majibu
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Katika vipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu cha chaguo cha kujibia.
(i) Ni taarifa zipi zinaweza kupatikana katika kamusi kati ya hizi?
A. Neno, maana, matamshi na matumizi ya semi
B. Maana, neno, mazungumzo na matumizi ya semi
C. Matumizi ya semi, matamshi, maana na mazungumzo
D. Matamshi, mazungumzo, maana na kidahizo
E. Kidahizo, matamshi, mazungumzo na semi
Jibu: D
(ii) “Juma anaendesha baiskeli yake polepole.” Kiarifu cha sentensi hii kimejengwa na mfuatano upi wa vipashio?
A. Kiima, chagizo na shamirisho
B. Kitenzi kishirikishi, shamirisho na chagizo
C. Kiarifu, kiima na chagizo
D. Shamirisho, chagizo na kitenzi kikuu
E. Kitenzi kikuu, shamirisho na chagizo
Jibu: E
(iii) “Tutakuja kumpokea kwenye uwanja wa ndege.”
Kazi ya kielezi kinachojitokeza kwenye sentensi hii ni ipi kati ya hizi?
A. Kueleza idadi
B. Kueleza mahali
C. Kueleza namna
D. Kueleza wakati
E. Kueleza nafsi
Jibu: B
(iv) Tamathali ipi ya semi hufananisha mambo kwa kutumia viunganishi?
A. Tashhisi
B. Sitiari
C. Nidaa
D. Tashbiha
E. Tabaini
Jibu: D
(v) Tamathali ipi ya semi inatawala katika wimbo ufuatao?
Ze ndi ndi ndi!
Tolly ndi!
Ndi ndi ndi ndi!
Tolly ndi! ×4
A. Tabaini
B. Taniaba
C. Tashbihi
D. Takriri
E. Tashihisi
Jibu: D
(vi) Neno lipi linadhihirisha kauli ya kutendeka katika kitenzi pika?
A. Pikia
B. Pikiwa
C. Pikika
D. Pikwa
E. Pikisha
Jibu: C
(vii) Yupi kati ya wafuatao anajishughulisha na kusoma, kuchambua na kutoa maoni katika kazi za sanaa?
A. Mdhamini
B. Mtunzi
C. Mhariri
D. Msomaji
E. Mhakiki
Jibu: E
(viii) Hatua mojawapo ya uendelezaji wa lugha ili itumike kitaifa na kimataifa ni kuisanifisha. Jambo lipi kubwa linalofanywa katika hatua hii kati ya yafuatayo?
A. Kupunguza maneno ya kukopa
B. Kuondoa tofauti za kimsamati
C. Kuifanya itumike na jamii ndogo
D. Kuweka tofauti za matamshi
E. Kuidhinisha tofauti za maneno
Jibu: B
(ix) Ni kwa namna gani tungo hutofautiana na sentensi?
A. Tungo zote ni sentensi lakini sentensi zote si tungo
B. Sentensi haitoi taarifa kamili lakini tungo hutoa taarifa kamili
C. Sentensi ni miongoni mwa tungo lakini si kila tungo ni sentensi
D. Tungo sharti ikamilike lakini sentensi si lazima ikamilike
E. Tungo ni ndefu sana lakini sentensi ni fupi sana
Jibu: C
(x) Jambo lipi si muhimu katika uandishi wa kadi ya mwaliko?
A. Jina la mwandishi na mwalikwa
B. Idadi ya waalikwa
C. Tarehe ya tukio
D. Kusudi la tukio
E. Mahali tukio linapofanyika
Jibu: B
2. Oanisha mifano ya tamathali za semi iliyoko katika Orodha A na tamathali husika zilizo katika Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
Orodha A
(i) Kilio cha mama mfiwa kilisikika mithili ya king'ora. E
(ii) Haba na haba hujaza kibaba. H
(iii) Misitu ni uhai. G
(iv) Shangazi amejifungua salama. C
(v) Upepo mkali ulipiga miluzi kila ulipogonga kingo za mti. B
(vi) Binadamu hupanga, Mungu hupangua. D
Orodha B
A. Mjalizo
B. Tashihisi
C. Tafsida
D. Tabaini
E. Tashbiha
F. Onamatopea
G. Sitiari
H. Takriri
Sehemu B (Alama 54)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. (a) Tumia mzizi chez- kuunda vitenzi viwili kwa kila kauli kama zilivyoorodheshwa:
(i) Kauli ya kutendeana
Chezeana,
(ii) Kauli ya kutendana
chezana
(iii) Kauli ya kutendeka
chezeka
(iv) Kauli ya kutendewa
chezewa
(b) Unda nomino moja kwa kila kitenzi.
(i) Zaa
mzazi
(ii) Kimbia
mkimbiaji
(iii) Shikilia
Mshikiliaji
(iv) Elekeza
maelekezo
(v) Penda
mpenzi
4. (a) Fafanua vyanzo vinne vya misimu kwa kutoa mfano mmoja kwa kila chanzo cha misimu husika.
Misimu huzuka kulingana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii husika katika nyakati mbalimbali. Mfano wa misimu iliyotokana na mabadiliko ya kihistoria ni Kupe, katika kipindi cha ujamaa.
Misimu huzuka kutokana na haja ya watu kuelezea hisia zoa juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea katika vipindi fulani kwa mfano, njaa, mafuriko, vita n.k. katika kipindi cha njaa kuliibuka misimu kama unga wa yanga.
(b) Eleza maana mbili kwa kila neno.
(i) Kaka
Ndugu wa mkubwa wa kiume
Ganda tupu la yai au kibiriti
(ii) Kito
Jiwe la thamani
Mchezo wa watoto wa kuficha vitu na kuvitafuta
(iii) Mkaa
Vipande vya mti vilivyochomwa moto na kuzimwa kabla havijawa majivu.
Mti ambao gome lake ni dawa ya kuzuia kuharisha au kukohoa.
(iv) Mkwaju
Mti unaozaa matunda yaitwayo ukwaju.
Fimbo
(v) Babu
Baba mzaa baba au mama
Mshauri wa kiume katika chama cha wanawake.
5. Bainisha viambishi vya o-rejeshi katika kila sentensi kwa kuvipigia mstari kisha taja ngeli husika kwa kila kirejeshi.
(a) Udongo ulioleta umekauka.
O
U-
(b) Kioo kilichovunjika kimetolewa.
Cho
KI-VI
(c) Karatasi zilizokatika zimetumika.
Zo
I-ZI
(d) Mlimokuwa mna joto sana?
Mo
M-
(e) Kijana atakayeshinda atapewa zawadi.
Ye
A-WA
(f) Gazeti lililochapwa limekwisha.
Lo
LI-YA
(g) Barabara iliyofungwa imekamilika.
Yo
I-ZI
(h) Magonjwa yaliyowasumbua yalitokana na athari ya mvua.
Yo
LI-YA
(i) Ng’ombe aliyeanguka shimoni amekolewa.
Ye
A-WA
6. Eleza kwa kifupi maana ya nahau zifuatazo:
(a) Juma ana mkono wa birika
Juma ni mgumu kutoa
(b) Kaka amepata jiko
Ameoa
(c) Mjomba amepiga maji
amelewa
(d) Mwizi amekata mguu
Ameacha kuja
(e) Mtoto amevimba kichwa
Anajiona yeye ni bora, anajidai
(f) Beka ana mkono mrefu
mwizi
(g) Rafiki yangu anakaza kamba
Anafanya bidii katika jambo analotaka
(h) Kijana amepiga kete
amefanikiwa
(i) Huyu ana damu mbichi
Bado mdogo
7. Eleza kwa kifupi sifa sita zilizofanya kiunguja kikachaguliwa kuwa lahaja ya kusanifisha lugha ya kiswahili.
Kilikuwa kimetumika sehemu kubwa
Kiliandikwa vitabu vingi
Kilikuwa na watumiaji wengi
Lahaja ya Kiunguja ilikuwa rahisi kujifunza
8. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
Kwa hakika mwaka ule watu walivuna sana. Haikuwahi kutokea takribani kwa kipindi cha muongo mmoja hivi kuwa na mavuno kiasi hicho. Maghala yalijaa mahindi, mtama, mpunga, uwele, baazi, maharage, njegere na njugumawe. Nyama nyingi ililetwa kutoka porini ambazo wanawake walizitanda na kuzikausha motoni. Aidha, samaki wakubwawakubwa walipatikana kwa wingi, samaki ambao hawakuwahi kupatikana hapo awali. Kila mmoja kijijini hapo alikuwa na furaha.
Mavuno hayo yaliambatana na sherehe za mwisho wa mwaka ambazo zilikuwa ni zenye kufurahisha. Vigelegele vilisikika, ngoma zilipigwa na marimba yakayungwa huku watu wa rika zote wakicheza bila kujali kuwa ni wazee au watoto. Wasichana wa umri wa miaka kumi na mbili walitikisa mili yao kwa mvuto, huku miguu yao ikifuatia mitindo maalum kutoka ardhi ngumu yenye vumbi, wakicheza kwa madoido wakirusharusha shingo zao kama twiga mbugani. Walipeana zamu ya kucheza wengine wawiliwawili na wengine watatuwatatu. Baadaye, wavulana nao walicheza ngoma yao. Kadiri ngoma zilivyodundwa, ndivyo vijana walivyokuwa wakicheza na kuruka juu kama swala. Wazee walitazama na kuridhika huku wanawake wakishangilia kwa vigelegele wakati vijana walipoonyesha pumzi jukwaani.
Wakati wanawake na vijana wakicheza na kuimba, wazee waliketi kando ya moto wakinywa sharubati mpya. Mmoja baada ya mwingine, wazee hao walizungumza na kuanza kucheza. Wakajishikia viuno mara nyingi. Ingawa hawakuwa na kasi kama vijana, lakini walijaribu katika mvuto na ubunifu wa uchezaji wao.
Wapigaji watatu wa marimba walijitokeza na kuonesha umahiri wao. Kila mpigaji alionesha uhodari wake wa kupiga marimba, kuimba na kucheza. Alipoacha, mwingine alijitokeza, akiimba na kujiunga na tungo iliyoanzishwa. Walikuwa kama kundi la muziki wa wapiga marimba ambao kila aliyewasikiliza alivutiwa na upigaji wao uliyotoa mlio wa kumtoa nyoka pangoni. Mdundo wa mziki wa marimba uliingia moja kwa moja hadi ndani ya mioyo yao.
Wakati wa machweo, watu walipumzika na kula chakula. Wapiga marimba waliungana na wapiga ngoma na hivyo uchezaji uliendelea tena hadi usiku wa manane. Kilichowaondoa watu uwanjani pale ni ama uchovu au usingizi.
Maswali
(a) Andika kichwa cha habari uliyoisoma kisichopungua maneno matatu na kisichozidi maneno matano.
SHEREHE ZA MAVUNO
(b) Bainisha shughuli mbili muhimu zilizokuwa zikiwapatia watu riziki kulingana na habari uliyosoma.
Kilimo
Uvuvi
(c) Fafanua kwa kifupi maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari uliyoisoma. (i) Muongo mmoja (ii) Waliwapiku
Miaka kumi
waliwashinda
(d) Fupisha habari hii kwa maneno yasiyopungua mia moja (100) na yasiyozidi mia na tano (105).
Baada ya mavuno mazuri, kijiji kiliamua kufanya sherehe. Watoto, vijana na wazee, wote walicheza ngoma wakisherekea mavuno. Wazee hawakuwa na kasi kama vijana, lakini walicheza. Mabinti walicheza wakifuatisha mdundo na kutimua chini. Wazee walisikiliza, na mara nyingi walisimama kila walipocheza, walishika viuno vyao mara nyingi. Wazee hawa walionekana wakinywa sharubati mpya na walifurahishwa sana na ngoma ile hata waliwaona watu wakitingisha vichwa vyao.
Wapigaji wa marimba waliwafurahisha watu kwa upigaji wao. Walikuwa wapigaji watatu waliopiga marimba kwa ustadi wa hali ya juu. Wapiga ngoma nao walikuwa pembezoni mwa wapiga marimba. Watu walicheza mpaka usiku wa manane. Walioondoka, waliondoka kwa sababu ya usingizi ama uchovu.
Sehemu C (Alama 30)
Jibu maswali mawili kutoka katika sehemu hii. Swali la tisa ni la lazima na kila swali lina alama 15.
9. Jifanye wewe ni mmojawapo wa watoto waliohudhuria kongamano lililohusu haki za watoto, andika beti tano za utenzi kuhusu ‘haki za mtoto.’
HAKI ZA WATOTO
Haki wa watoto wetu,
Elimu siyo upatu,
Walindwe dhidi ya chatu,
Hizo ndiyo hazi zao.
Wapelekwe masomoni,
Waondolewe vitani,
Na nguo nzuri mwilini,
Hizo ndiyo haki zao.
10. lengo kuu la kazi za fasihi ni kuonya na kuiasa jamii. Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.
Takadini
Mwandishi anaionya na kuiasa jamii juu ya suala la kuwaua walemavu. Anawaonya wanajamii kwamba, walemavu hawatakiwi kuuawa kwani kufanya hivyo ni kinyume na haki za binadamu. Mwandishi anaiasa jamii kuwa, walemavu wanaweza kufanya kazi sawa na watu wengine.
Watoto wa mamantilie
Mwandishi anaionya na kuiasa jamii juu ya suala la kuwafukuza watoto shule. Mwandishi anawaonya wanajamii wasiwafukuze watoto shule kwani kwa kufanya hivyo, watoto hawa wataharibika na kuwa wahalifu. Mwandishi anaiasa jamii kuwapa elimu watoto. Elimu hii ndiyo itatumika kama mkombozi wa maisha yao.
11. “uzembe ni jambo linalokwamisha maendeleo ya jamii nchini Tanzania.” tathmini kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.
Kilio chetu
Uzembe wa Mama Suzi unakwamisha maendeleo, Mama Suzi ni mzembe katika suala la kumuelimisha binti yake, anamuacha aende bila elimu yoyote, matokeo yake, anapata mimba na maambukizi ya UKIMWI.
Ngoswe pezi kitovu cha uzembe
Ngoswe ni mzembe kwani anaendekeza mapenzi badala ya kazi. Analeta uzembe katika kazi aliyotumwa kuifanya ambayo ni kuhesabu watu, badala yake anaanzisha kazi mpya ya kumtaka kimapenzi msichana Mazoea. Anapojaribu kutoroka naye, uzembe huu unaleta hasara kubwa ya kuchomwa moto kwa nyaraka.
Jiunge Darasa la Solving Ujipatie Solving Zote na Utabiri wa Mitihani ya NECTA, Gusa Hapa Kujiunga
