Nafasi za Kazi ya Ualimu Ellen White Pre and Primary School

Gari la Shule ajira za walimu Ellen White School
ELLEN WHITE PRE AND PRIMARY SCHOOL

P. O. Box 3118, Nzuguni Dodoma – Tanzania
Mob: 0769 352 215 / 0673 443 962
Email: info@ews.sc.tz
Web: www.ews.sc.tz

Kumb. Na. EWS/PNA/2026/01 06/07/2026

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Ofisi ya Meneja wa Ellen White School – Dodoma, inapenda kutangaza nafasi za kazi (23) za kada mbalimbali ili kuimarisha utendaji wake. Watu/Watanzania wote wenye sifa na uwezo wanaalikwa kutuma maombi yao ili kujaza nafasi za kazi kama zilivyoainishwa hapa chini:-

1.0 WALIMU WA SHULE YA MSINGI DARAJA LA I A – Nafasi 6

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

(i) Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu aliyokabidhiwa;

(ii) Kutengeneza na Kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia;

(iii) Kufundisha, kufanya tathmini na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi;

(iv) Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;

(v) Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;

(vi) Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;

(vii) Kusimamia utunzaji wa vifaa na mali za Shule;

(ix) Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

1.2 SIFA ZA MWOMBAJI

(i) Wahitimu wa Shahada (Degree) ya Ualimu mwenye kufundisha masomo ya Sayansi au Hisabati.

(ii) Wahitimu wa Shahada (Degree) ya Ualimu mwenye kufundisha masomo ya Kiswahili au Kiingereza.

(iii) Wahitimu wa Shahada (Degree) ya Ualimu mwenye kufundisha masomo ya Historia ya Tanzania na Maadili, Jiografia na Mazingira au Stadi za Kazi.

(iv) Wenye uwezo wa kufundisha masomo kwa kutumia lugha ya Kiingereza kwa ufanisi na mwenye uzoefu wa angalau miaka mitatu (3) ya kufundisha katika shule inayotambulika atapewa kipaumbele.

1.3 NGAZI YA MSHAHARA

EWSS-A KUANZIA TZS 800,000.

2.0 WALIMU WA SHULE YA AWALI NA MSINGI DARAJA LA II B – Nafasi 10

2.1 MAJUKUMU YA KAZI

(x) Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na Mpango wa Kazi wa majukumu aliyokabidhiwa;

(xi) Kutengeneza na Kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia;

(xii) Kufundisha, kufanya tathmini na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi;

(xiii) Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;

(xiv) Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;

(xvi) Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kitaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;

(xvii) Kusimamia utunzaji wa vifaa na mali za Shule;

(xviii) Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule.

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Mwajiriwa anatakiwa awe na Stashahada (Diploma) katika Elimu ya Awali au Msingi kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali. Aidha, mwenye uwezo wa kufundisha masomo kwa kutumia lugha ya Kiingereza kwa ufanisi na mwenye uzoefu wa angalau miaka miwili ya kufundisha katika shule inayotambuliwa atapewa kipaumbele.

2.3 NGAZI YA MSHAHARA

EWSS-B KUANZIA TZS 501,000.

3.0 AFISA USAFIRISHAJI DARAJA LA II B – Nafasi 1

3.1 MAJUKUMU YA KAZI

(i) Kupanga na kuratibu ratiba za magari ya shule kwa ufanisi.

(ii) Kutayarisha gharama za uendeshaji wa usafiri kwa ajili ya kusaidia kutoa maamuzi.

(iii) Kuhakiki kuwa, takwimu na kumbukumbu zinazohusu vyombo vya usafiri zinatunzwa vyema na kwa usahihi.

(iv) Kufanya ukaguzi wa magari na mitambo ya shule kila siku na kutoa taarifa.

(v) Kuandaa taarifa, makisio na mahitaji ya ukarabati wa magari na mitambo.

(vi) Kutekeleza majukumu mengine yatakayoihusu usafirishaji.

(vii) Kusimamia matumizi ya mafuta pamoja na ujazaji wa kitabu cha mafuta (logbook).

(i) Kuweka kumbukumbu vyao vya kushukia.

(ii) Kuwapeleka watumishi nje ya kituo cha kazi kwa kazi za nje.

(iii) Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.

(iv) Kufanya usafi na matengenezo madogo madogo ya gari.

(v) Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.

(vi) Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari "logbook" kwa safari zote.

(vii) Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

5.2 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa mwombaji na awe:-

(i) Amehitimu angalau Elimu ya msingi (Darasa la saba) au kidato cha Nne.

(ii) Awe na leseni halali ya Daraja C, na C1 yenye uzoefu wa angalau miaka miwili bila kusababisha ajali.

(iii) Amehitimu mafunzo ya uendeshaji wa magari ya abiria (PSV) kutoka VETA, NIT au chuo kinachotambuliwa na serikali. Mwombaji mwenye cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la II atapewa kipaumbele.

5.3 NGAZI YA MSHAHARA

EWOS-B KUANZIA TZS 400,000.

6.0 MASHARTI YA JUMLA

(i) Waombaji wote wawasilishe barua za maombi ya kazi zilizoandikwa kwa mkono kwa lugha ya Kiingereza. Wawe ni Raia wa Tanzania umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 50.

(ii) Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detailed Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.

(iii) Waombaji wote waambatanishe nakala za vyeti vya taaluma vinavyohusiana na nafasi husika. Pamoja na nakala ya kitambulisho cha NIDA.

(iv) Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).

(v) Picha moja ya rangi ya pasipoti iliyopigwa hivi karibuni.

Zingatia

Barua zote za maombi zitumwe kupitia EWS Recruitment Portal. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 20/07/2026, katika saa za kazi.

MENEJA WA SHULE,
ELLEN WHITE SCHOOL,
S.L.P 3118, DODOMA.

TANGAZO

Msaada wa Kuandikiwa CV, Barua ya Maombi ya Kazi au Kufanyiwa Maombi Yote, Wasiliana na Mwalimu kwa Kugusa Hapa

Popular posts from this blog

SMS 20 za Vichekesho Zinazochekesha Sana

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1

Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe