Nafasi za Kazi za Udereva | Mwandishi Mwendesha Ofisi
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.
Zimetoka nafasi za kazi mpya zinazohusisha udereva na mwandishi mwendesha ofisi. Unapoomba nafasi hizi zingatia kuwa na CV inayokubalika pamoja na barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa vizuri na iwe imewekwa saini yako. Nakusisitiza kuwa, usitumie akili mnemba (AI) kama Gemini na ChatGPT katika kuandika CV na barua yako. Miundo yake inafanana na kutambulika kwa wepesi, kama huwezi kuandika mwenyewe, ajiri mtu akuandikie na sissi tupo kwa ajili ya kazi hiyo.
Nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu
Nanyumbu wametoa nafasi za kazi za mwendesho ofisi na dereva.
1. Mwandishi mwendesha ofisi daraja la II nafasi 4
2. Dereva daraja la II nafasi 5
Namna ya kuomba na sifa zinazotakiwa, soma hapa.
Nafasi za kazi Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Kigoma wametoa nafasi za kazi za udereva.
1. Dereva daraja la II nafasi 3
Namna ya kuomba na sifa zinazotakiwa, soma hapa.
Nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu
Kasulu wametoa nafasi za kazi za mwandishi mwendesha ofisi na dereva.
1. Mwandishi mwendesha ofisi daraja la II nafasi 12
2. Dereva daraja la II nafasi 3
Namna ya kuomba na sifa zinazotakiwa, soma hapa.
Nafasi za kazi Halmashauri ya Mji wa Babati
Babati wametoa nafasi za kazi za mwandishi mwendesha ofisi na dereva.
1. Mwandishi mwendesha ofisi daraja la II nafasi 3
2. Dereva daraja la II nafasi 4
Namna ya kuomba na sifa zinazotakiwa, soma hapa.
Unapoomba nafasi hizo, zingatia mambo haya:
Uwe raia wa Tanzania.
Umri kuanzia miaka 18 na usizidi miaka 45.
Waombaji wenye ulemavu wanapewa kipaumbele, hivyo wajitokeze kuomba kwa wingi.
Ambatanisha CV: katika cv yako hakikisha umeweka anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na barua pepe, na majina matatu ya wadhamini. Ili kuhakikisha kwamba hukosei, unaweza kuwasiliana nasi tukutengenezee CV yako inayokubalika.
Hakikisha vyeti vyako vyote vya elimu na taaluma vimethibitishwa na mwanasheria/wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha Nne au sita, na vinginevyo.
Waombaji waliostaafishwa katika utumishi wa umma wanaruhusiwa kuomba kwa masharti ya kuwa na kibali kutoka kwa katibu mkuu kiongozi.
Kama tayari upo kazini, huruhusiwi kuomba.
Hakikisha unaandika vizuri barua yako na iwe imesainiwa.
Maombi yote yanatumwa katika mfumo wa kielektroniki.
Kitaalamu Zaidi, Tunaweza Kukuandikia Barua ya Maombi ya Kazi na CV Uitwe Katika Usaili na Upate Kazi. Barua Tsh. 5,000/= na CV Tsh. 9,000/=. Gusa Hapa Kuwasiliana Nasi.