Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Nne 2024 NECTA Majibu
Sehemu A (Alama 16)
1. Katika kipengele I hadi X chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu kwenye kijitabu chako cha kujibia.
(i) Vifuatavyo ni vyanzo vya misimu, isipokuwa:
A Tanakali sauti au milio A
B Sayansi na Teknolojia
C Shughuli maalumu
D Utani katika jamii
E Mabadiliko ya historia
(ii) Neno lenye mofu ya mtendwa ni lipi kati ya haya?
A Aliyetembea
B Alimkimbilia B
C Alivyotembea
D Atakayetembea
E Ametembea
(iii) Msaada wako umenifaa sana. Asante! Neno "Asante!" ni aina gani ya neno?
A Nomino
B Kivumishi
C Kielezi
D Kitenzi
E Kihisishi E
(iv) Tamathali ipi ya semi hukipa kitu kisicho binadamu sifa ya ubinadamu?
A Taniaba
B Tashihisi B
C Tashibiha
D Takriri
E Tabaini
(v) "Wanafunzi wa Kidato cha Pili wamepigiwa ngoma." Kauli hii inaonesha hali gani?
A Kutendana
B Kutendeka
C Kutendewa C
D Kutendwa
E Kutendea
(v) "Wanafunzi wa Kidato cha Pili wamepigwa ngoma." Kauli hii inaonesha hali gani?
A Kutendana
B Kutendeka
C Kutendewa
D Kutendwa D
E Kutendea
(vi) Tanzu sahihi za Fasihi simulizi ni zipi kati ya zifuatazo?
A Ngonjera, mashairi, nyimbo na tenzi
B Historia, ngano, visasili na soga
C Semi, hadithi, maigizo na ushairi C
D Methali, misemo, nahau na vitendawili
E Michezo, vichekesho, majigambo na ngonjera
(vii) Mpangilio mzuri wa muundo wa insha ni upi?
A Kichwa, mwanzo, wazo na kiini
B Mwanzo, kiini, hitimisho na wazo
C Kichwa, wazo, hitimisho na kiini
D Kichwa, mwanzo, wazo na hitimisho
E Kichwa, mwanzo, kiini na hitimisho E
(viii) Kwa nini lugha ya mazungumzo ni halisi zaidi?
A Wahusika huwasiliana kwa simu
B Wahusika huwasiliana kwa ana kwa ana B
C Wahusika huwasiliana kwa mtandao
D Wahusika huwasiliana kwa barua
E Wahusika huwasiliana kwa barua pepe
(ix) Methali isiyosisitiza uvumilivu na jitihada katika kazi ni ipi?
A Afiriti hafichiki A
B Mvumilivu hula mbivu
C Acha koko uangue koma
D Aali hupatikana kwa ghali
E Abadi abadi kamba hukata jiwe
(x) Tungo ipi ina kiambishi rejeshi kati ya hizi?
A Anaondoka
B Ameondoka
C Aliondoshwa C
D Amejiondoa
E Ameondokewa
2. Oanisha fasili za vipera vya semi zilizopo katika Orodha A na vipera husika kutoka Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
Orodha A | Orodha B |
i. Semi fupi zinazoeleza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na uzoefu wa jamii. G ii. Semi fupi za mafumbo zinazotumia lugha ya picha na zinazotolewa kwa hadhira zikieleza jambo lenye kuhitaji jibu. E iii. Semi zilizojengwa kwa picha kwa kutumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti na maneno yaliyotumika. F iv. Semi zenye maonyo au mawaidha ambazo maana zake za ndani zimefichika. A v. Semi zenye picha za mafumbo zinazoonesha ukinzani wa fikra au matukio. B vi. Semi zinatumia picha, ishara na tamathali kueleza kitu au wazo kwa ufupi. H | A. Mafumbo B. Nahau C. Misemo D. Lakabu E. Vitendawili F. Mizungu G. Methali H. Misimu
|
Sehemu B (Alama 54)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. A. Kwa kutumia mifano, eleza jinsi vipengele vifuatavyo vinavyoweza kupotosha lengo la msemaji katika mazungumzo ya kila siku.
i. Matumizi ya msamiati usio sahihi.
Msamiati usio sahihi unaweza kupotosha lengo la msemaji, kwa mfano, msemaji anaposema ‘danga langu limelala’ anasababisha upotoshaji.
ii. Matumizi ya miundo isiyo sahihi
Miundo isiyo sahihi inapotosha lengo la mseamaji katika mazungumzo kwa mfano, ‘sokoni cheza baba ana,’ hapa miundo haijakaa sawa na inaleta upotoshaji, ilitakiwa iwe, ‘baba anacheza sokoni.’
iii. Matumizi ya matamshi yasiyo sahihi
Matamshi yasiyo sahihi nayo yanasababisha upotoshaji, kwa mfano, mtu anapotamka, ‘kula’ ilhali anamaanisha kura, inafanya iwe ngumu kueleweka hivyo kupotosha.
iv. Kukosekana kwa mantiki katika tungo
Kukosekana mantiki katika tungo nako kunasababisha upotoshaji, kwa mfano, mtu anaposema, ‘usimwange kuku kwenye mchele mwingi, anapotosha, ‘ilitakiwa aseme usimwage mchele kwenye kuku wengi.
B. Fasili kwa kifupi istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika lugha ya Kiswahili.
i. Irabu
Irabu ni sauti ambazo hutamkuwa bila kuwekwa kikwazo. Kwa mfano, a, e, i, o, u.
ii. Kiimbo
Kiimbo ni kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti wakati wa kutamka.
iii. Konsonanti
Sauti ambazo hutamkwa kwa kuweka kikwazo, kwa mfano, z, b, s.
iv. Lafudhi
Lafudhi ni namna ambavyo mtu anatamka lugha, namna hii inatokana na kuathiriwa na lugha mama. Kwa mfano, lafudhi ya Kisukuma.
v. Mkazo
Mkazo ni sauti ambazo hutamkwa kwa nguvu na kusikika kuliko sauti zingine katika neno. Katika lugha ya Kiswahili, mara nyingi mkazo hutokea katika silabi ya pili.
4. Ujio wa Waarabu, Wajerumani na Waingereza ulikuwa ni mchango mkubwa katika kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili nchini Tanzania kabla ya uhuru. Eleza umuhimu wao kwa hoja mbili kwa kila taifa.
Umuhimu wa Waarabu katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili
Waarabu walitumia lugha ya Kiswahili katika biashara zao hivyo kufanya Kiswahili kienee.
Katika kufundisha dini, waarabu walitumia lugha ya Kiswahili hivyo kuwafanya Waislamu wengi wakifahamu Kiswahili.
Umuhimu wa Wajerumani katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili
Kutoa mafunzo ya lazima ya lugha ya Kiswahili kwa wafanyakazi wa serikali: Wajerumani waliweka sheria kwamba, lazima kila mfanyakazi wa serikali ajue lugha ya Kiswahili. Hivyo, wafanyakazi wote wa serikali ya kijerumani wakiwemo maakida, walijifunza lugha ya Kiswahili ili wapate kigezo cha kuajiriwa au kubaki na ajira zao. Hata Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza kiswahili ili waweze kuwasiliana na wenyeji kwa urahisi na hivyo kurahisisha shuguli zao za kiutawala.
Ujenzi wa shule: Shule zilifunguliwa kufundisha watu weusi ili waje wawe wasidizi wao katika utawala wa wajerumani, na lugha iliyokuwa ikitumika kufundisha masomo ilikuwa ni lugha ya Kiswahili.
Umuhimu wa Waingereza katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili
Waingereza waliruhusu Kiswahili kifundishwe mashuleni hivyo wanafunzi wengi wakapata nafasi ya kuifahamu lugha.
Mikutano ya kisiasa katika enzi za utawala wa Waingereza ilifanyika kwa lugha ya Kiswahili hivyo Kiswahili kikapata nafasi ya kukua na kuenea.
5. a. Kwa kutoa mfano mmoja kwa kila neno, fafanua istilahi zifuatazo kama zinavyotumika katika kamusi ya Kiswahili Sanifu.
i. Homonimu
Homonimu ni maneno ya kiswahili yenye kufanana lakini yenye maana tofauti! Kwa mfano, barabara, inaweza kumaanisha jambo limefanyika vizuri au inaweza kumaanisha njia.
ii. Sinonimu
Sinonimu ni neno lililo na maana sawa na neno jingine kwa mfano, 'mwandani' ni sinonimu ya 'mpenzi'.
iii. Kategoria
Kategoria ni tabaka au kundi la vitu, watu n.k, lenye ubora au sifa zinazofanana.
iv. Kisawe
Kisawe ni neno lenye maana ileile ya neno lingine; kwa mfano jogoo kisawe chake ni kikwara.
b. Bainisha aina za maneno yaliyopigiwa msitari katika sentensi zifuatazo:
i. Nguo yoyote fupi ni marufuku.
Kivumishi
ii. Amina ndiye mwanangu.
Kivumishi
iii. Alisoma kwa bidii japokuwa alifeli.
Kiunganishi
v. Afadhali! Mwalimu amerudi nyumbani.
Kihisishi
vi. Walianguka kizembe.
Kielezi
Pata Majibu ya Maswali yaliyobaki kwa Tsh. 1,000/= tu, Wasiliana na Mwalimu Hapa
6. Kwa kutumia hoja sita, fafanua mafanikio sita ya Kamati ya Lugha ya afrika Mashariki ya mwaka 1930 katika kusimamia usanifishaji wa lugha ya Kiswahili.
7. Fafanua mambo tisa ya muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa dayolojia.
8. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Kulikukwa na kiongozi mmoja maarufu aliyekuwa amebobea na kusifika sana katika ukanda wenye misitu minene. Siku zote alikuwa anasisitiza umuhimu wa kupanda miti kabla ya kukata miti. Aidha, kila mara alikuwa anawahamasisha watu juu ya umuhimu wa kupanda miti kuzunguka maeneo yao yote kwa kuamini kuwa akiba haiozi.
Siku moja alialikwa katika shule ya Sekondari Twaweza kuhudhuria mahafali ya kuhitimu Kidato cha Nne. Kabla ya shamrashamra kuanza, alihakikisha kwanza miti inapandwa katika eneo lote la kuzunguka shule. Katika wosia wake, aliwashawishi wanafunzi kuwa mabalozi wa upandaji miti, utunzaji miti na usafi. Aliwasisitiza kuwa safi kwani usafi ndiyo njia pekee ya kulinda afya zao kwa kuwa afya njema ni mtaji wa mafanikio yao. Vilevile, alikemea vikali tabia ya kutiririsha maji machafu, kutupa takataka ovyo na kujisaidia sehemu zisizostahili.
Aliwasihi wahitimu kuwa, miongoni mwao watapatikana viongozi ambao watakuwa na moyo wa kuendeleza kazi ambayo viongozi waliokuwepo waliithamini sana. Hii itasaidia kuinusuru nchi yetu isije ikavamiwa na madhara ya jangwa baada ya kipindi si kifupi. Ukataji wa miti holela huathiri uwoto wa asili, kufukuza mvua na kukaribisha ukame.
Aliendelea kueleza kuwa, hatuna budi kuelewa kwamba ukosefu wa mvua siku zote ndicho chanzo kikuu cha maradhi ya binadamu, wanyama wa mwituni, wanyama wafugwao na hata wadudu na mimea pia. Kila mmoja akikariri kauli mbiu panda mti kata mti tutakwepa ukame. Hivyo, kila mwanajamii anapwaswa kuienzi kwa dhati kabisa kauli mbiu hii kwani mchelea mwana kulia, hulia yeye.
Maswali
A. Andika kichwa cha habari hii kwa maneno matatu.
B. Eleza maana ya methali zifuatazo kama zilivyotumika katika habari uliyosoma.
i. Akiba haiozi.
ii. Mchelea mwana kulia, hulia yeye.
C. Kutokana na habari uliyosoma, taja athari mbili za kukosa mvua kwa binadamu, wanyama, wadudu na mimea.
D. Fupisha habari uliyosoma kwa maneno yasiyopungua sitini na yasiyozidi sabini.
Sehemu C (Alama 30)
JIbu mawali mawili kutoka sehemu hii. Swali la 9 ni lazima na kila swali lina alama 15.
9. Kwa kutoa hoja mbili na mifano, eleza namna jina la kitabu linavyosaidifu yaliyomo katika diwani mbili ulizosoma.
10. “Mapenzi ya dhati huleta faraja miongoni mwa wanajamii.” Thibitisha kauli hii kwa kuoa hoja tatu kuotka katika kila riwaya kati ya riwaya mbili ulizosoma.
11. Kwa kutumia hoja tatu kwa kila kitabu katika tamthiliya mbili ulizosoma, eleza namna walivyotumia dhamira mbalimbali ili kuakisi jamii ya leo.
Pata Majibu ya Maswali yaliyobaki kwa Tsh. 1,000/= tu, Wasiliana na Mwalimu Hapa