Posts

Showing posts from April, 2020

Civics Form Three Notes | Topic One Two and Three

Image
Civics form three has a total of three topics which are:      1.    LifeSkills      2.    Economicand Social Development      3.    Poverty The first topic called 'Life Skills' deals with the various skills one must have in order to live well in his or her community. Among the insights expressed in this topic are: good leadership, self-confidence and teamwork. The purpose of this topic is, of course, to stimulate the student to gain accurate knowledge that will enable them to live well in their community. The second topic called 'Economic and Social Development' concerns economic and social development issues. This topic teaches the student the meaning of development, indicators of development, factors that drive development, government's contribution to development, the contribution of financial institutions to development and the contribution of private sector to development. Also,...

Notes za Civics Form Three | Kidato cha Tatu

Image
Notes za Civics kidato cha tatu, ama kwa Kiswahili sahihi, nukuu za somo la uraia kidato cha tatu zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa kwani, vitabu vya kurejea ni vichache. Somo la Civics kidato cha tatu lina jumla ya mada tatu kama kilivyo kidato chenyewe, mada hizo ni:      1.    Life Skills      2.    Economic and Social Development      3.    Poverty Mada ya kwanza iitwayo ‘Life Skills’ inahusu maarifa mbalimbali anayopaswa kuwa nayo mtu ili aweze kuishi vyema katika jamii yake. Miongoni mwa maarifa yanayoelezwa katika mada hii ni: uongozi bora, kujiamini mwenyewe na kufanya kazi kwa kushirikiana. Bila shaka malengo ya mada hii, ni kumfanya mwanafunzi azidi kupata maarifa sahihi yatakayomwezesha kuishi vyema katika jamii yake. Mada ya pili iitwayo ‘Economic and Social Development’ inahusu masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mada hii inamfundisha mwanafunzi ...

Uandishi | Kiswahili Kidato cha Pili

Image
Insha za hoja Insha za hoja ni insha zinazoelezea jambo fulani katika hali ya kujenga hoja ambazo zinatetea msimamo fulani alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo analolizungumzia. Hoja ni maelezo bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea msimamo wake. Katika uandishi wa insha za aina hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani ambalo analiunga mkono na ni lipi ambalo hakubaliani nalo. Ili hoja zote zipate kueleweka ni sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ulio sahihi kiasi kwamba mtu aisomapo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anaijadili na ana msimamo gani kuhusu mada hiyo. Mambo ya Kuzingatia Katika Uandishi wa Insha za Hoja Unapoandika insha za hoja, au aina zingine za insha, zingatia mambo haya: 1. Kubaini mada ya kuandikia insha na kuielewa vyema. 2. Kupanga mawazo katika mtiririko wenye mantiki. 3. Kutumia mtindo unaoendana na kusudi la insha . Kwa mfano, mtindo wa masimulizi, unafaa kwa hadithi au insha zingine za kisanaa. 4. Kutumia lugha...

Utungaji wa Kazi za Fasihi Simulizi | Kiswahili Kidato cha 2

Image
Kazi za fasihi simulizi hazikutokea tu, kuna mtu alitunga kazi hizo. Mada hii, inaangazia utungaji wa kazi za fasihi simulizi: Utungaji wa mashairi Kanuni za Utungaji wa Mashairi Utungaji wa mashairi una kanuni mbili: 1. Fani 2. Maudhui Katika fani , mshairi azingatie lugha anayotumia kama: tamathali za semi, methali nahau na misemo pamoja na picha na taswira. Pia, mshairi azingatie kama mtindo wa shairi, kama ni shairi la kimapokeo au shairi la kisasa. Pia, mshairi azingatie muundo wa shairi lake, kama atatumia mistari miwili, mmoja, sita ama apendavyo yeye. Katika maudhui, unapotunga shairi zingatia wazo lako.   Mfano: ni lipi lengo la wewe kutunga shairi? Inawezekana unatunga shairi ili kuzungumzia hali ya umasikini unaoikumba nchi yako, au pengine una lengo tofauti. Pia, zingatia ujumbe au mafunzo yanayopatikana katika shairi ulilotunga. Unalenga kufikisha ujumbe gani? Mfano wa shairi lililotungwa kwa kuzingatia kanuni Kubaka Nimekuwa nikipima, najiuli...

Jinsi ya Kuzuia Kusinzia Darasani Mwalimu Anapofundisha

Image
Kabla mwalimu hajaingia darasani, unakuwa na nguvu za kutosha na unazungumza na wanafunzi wenzako. Mwalimu anapoingia, hali inabadilika, kadri anavyoongea na wewe ndiyo usingizi unazidi kukolea. Badala ya kuelewa kipindi, unaishia kusinzia. Sasa mwalimu katoka na usingizi nao haupo. Ni kama umerogwa eeeh? Hapana, hujarogwa hilo ni tatizo la kawaida na karibia kila mwanafunzi hukutana nalo. Tatizo la kusinzia darasani. Kusinzia darasani kunaweza kukufanya uyachukie masomo na mwisho wake upate matokeo mabaya ya darasani kwani kile ulichotakiwa kukielewa hutakielewa kwa sababu ya kukosa usikivu. Tatizo hili linahitaji tiba , na zifuatazo ni njia za kufanya ili kuzuia kusinzia darasani.      1.    Pangilia vizuri muda wako wa kulala Lala muda unaofanana na amka muda unaofanana kila siku hata katika siku za mwisho wa wiki. Kwa mfano, kama unalala saa sita usiku na kuamka saa moja asubuhi, fanya hivyo siku zote. Muda wa kulala ni saa nane, hata hivyo kama rati...

Uhifadhi wa Kazi za Fasihi Simulizi | Kidato cha Pili

Image
Uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi ni kitendo cha kutunza kazi za fasihi simulizi ili zidumu kwa muda mrefu na ziweze kutumiwa na vizazi vingi zaidi. Njia za kuhifadhi kazi za fasihi simulizi Kichwani Hii ndio njia ambayo imekuwa ikitumiwa kuhifadhi kazi za fasihi tangu kale na inaendelea kutumika hadi leo. Kwa kutumia njia hii kazi ya msanii hukaa kwenye ubongo wa msanii, naye huweza kuiwasilisha kazi hiyo, wakati wowote bila gharama yoyote. Ubora wake 1. Uwasilishaji unafanyika wakati wowote Uwasilishaji wa kazi hiyo unaweza kufanyika wakati wowote bila kuhitaji kufanyika maandalizi yoyote, hususani ya kiufundi. 2. Hakuna gharama Msanii hahitaji kugharimia kitu chochote ili aweze kuitoa kazi ya fasihi kichwani, ni uamzi wake tu, anaweza kuimba papo kwa papo. 3. Kazi ya fasihi iliyohifadhiwa kichwani ni hai Hii ni kwa sababu msanii anakuwa ana kwa ana na hadhira yake. Kutokana na matumizi ya mbinu tofauti za kisanaa kama vile kucheza, kubadili sauti, miondoko na men...