Notes za Civics Form Three | Kidato cha Tatu


Namba 3

Notes za Civics kidato cha tatu, ama kwa Kiswahili sahihi, nukuu za somo la uraia kidato cha tatu zinahitaji umakini mkubwa katika kuziandaa kwani, vitabu vya kurejea ni vichache.

Somo la Civics kidato cha tatu lina jumla ya mada tatu kama kilivyo kidato chenyewe, mada hizo ni:




Mada ya kwanza iitwayo ‘Life Skills’ inahusu maarifa mbalimbali anayopaswa kuwa nayo mtu ili aweze kuishi vyema katika jamii yake. Miongoni mwa maarifa yanayoelezwa katika mada hii ni: uongozi bora, kujiamini mwenyewe na kufanya kazi kwa kushirikiana.

Bila shaka malengo ya mada hii, ni kumfanya mwanafunzi azidi kupata maarifa sahihi yatakayomwezesha kuishi vyema katika jamii yake.

Mada ya pili iitwayo ‘Economic and Social Development’ inahusu masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Mada hii inamfundisha mwanafunzi maana ya maendeleo, viashiria vya maendeleo, mambo yanayosababisha maendeleo, mchango wa serikali katika kuleta maendeleo, mchango wa taasisi za fedha katika kuleta maendeleo na mchango wa taasisi binafsi katika kuleta maendeleo. Pia, mada hii inaisha kwa kuonesha mipango mbalimbali ya kujiletea maendeleo pamoja na mafanikio yake.

Mada hii itamfanya mwanafunzi atamani kupata maendeleo yake na jamii na hatimaye kuondokana na adha ya ukosefu wa maendeleo katika jamii yetu.

Mada ya tatu ambayo ndiyo mada ya mwisho kwa kidato cha tatu inaitwa ‘Poverty’. Mada hii inahusu umasikini. Katika mada hii, mwanafunzi atajifunza maana ya umasikini, mambo yanayosababisha umasikini na jinsi ya kufanya ili kuondokana na umasikini.

Mada hii itawafanya wanafunzi wabadili mtazamo wao kuhusu umasikini na kuwafanya waongeze mapambano dhidi ya umasikini na hatimaye kuiletea maendeleo jamii yetu ya Tanzania.

Notes hizi za Civics kidato cha tatu, zimeandaliwa kwa weledi mkubwa na Mwalimu Makoba, zimezingatia lugha rahisi inayoeleweka kwa wasomaji Watanzania ambao kiingereza siyo lugha yao ya kwanza.

Mwanafunzi anaweza kusoma ‘notes’ hizi bure katika mtandao huu, lakini hata hivyo, atatakiwa kuunga kifurushi kila atakapo kusoma. Endapo mwanafunzi angetaka awe na ‘notes’ zake mwenyewe na asome muda wowote bila kuhitajika kuunga kifurushi cha intaneti, anashauriwa kununua na atatumiwa katika mfumo wa PDF kokote alipo.

Nawatakia usomaji mwema.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1