Sitasahau Nilipolala na Mwanamke Juu ya Kaburi (27)| Riwaya
Nilishtuka nikaamka. Shingo iliuma lakini nilijikaza. Nilikuwa mahali nisipopafahamu, nazo fahamu zikazidi kunirejea taratibu hata nikagundua palikuwa pangoni. “Umetumwa kuja kuniokoa! Lakini nimekudondosha kwa kofi moja tu.” Mtoto alizungumza, bila shaka ni Chimota. “Sijabobea katika ulozi!” nilijibu. “Nani kabobea?” “Wewe, inasemekana ulizaliwa nao.” “Ulishuhudia wakati nazaliwa?” “Hapana. Niliambiwa tu.” “Ujinga ni kukubali kila unachoambiwa!” alinijibu. Nikakaa kimya. Nilizungumza na Chimota mpaka tukazoeana. Nilipomuuliza aliwezaje kuishi pangoni badala ya kuishi katika falme ya Matumbawe, alinijibu kuwa, aliutoroka utawala huo baada ya kugundua walitaka kumtumia katika mambo ya kunyanyasa watu wengine. Pia aligundua siri kuwa, yeye hakuwa mzaliwa wa Matumbawe, bali aliibwa kichawi na kufikishwa huko. Alipogundua nguvu zake za ziada, hakusita kukimbia. Hata hivyo, hakujua hasa ni kwa namna gani angerudi tena nyumbani, ujio wangu mahali pale ulimpa faraja na ...