Baada ya Mugabe, Waziri wa Fedha Zimbabwe Kukiona cha Mtema Kuni

Baada ya Mugabe, Waziri wa Fedha Zimbabwe Kukiona cha Mtema Kuni
Baada ya jeshi kuchukua mamlaka na kumkabidhi Mnangagwa kwa kile kilichosababishwa na maamuzi magumu ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe kumtimua makamu wake na kutaka kumwachia mamlaka mkewe, purukushani bado zinaendelea.
Aliyekuwa waziri wa fedha wa nchi hiyo, Ignatius Chombo amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya ufisadi na utumiaji mbaya wa mamlaka wakati alipokuwa akishikiria nyadhifa serikalini.
Chombo alikamatwa tangu tarehe 14 Novemba saa chache baada ya Mugabe kuzuiliwa nyumbani kwake.
Kuhusu jeshi kumpora mamlaka Mugabe, mahakama imesema jambo hilo ni halali.
Tayari Mnangangwa ameapishwa na hali nchini Zimbabwe inaonekana kuwa shwari.

Popular posts from this blog

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1

VICHEKESHO HIVI KIBOKO! SOMA KWA UANGALIFU USIVUNJE MBAVU ZAKO!

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu