Masai (Mc Kapalalai) wa Siri za Familia Mapenzini na Mwigizaji Recho
NI kweli, si maigizo tena kama
wafanyavyo siku zote. Masai (Mc Kapalalai), amezama katika dimbwi zito la
mahaba na mwigizaji mwenzake wa Siri za Familia – Recho!
Inasemekana kuwa, Masai kwa sasa
haambiwi lolote juu ya mwigizaji mwenzake Recho. Hajiwezi na sasa yupo tayari
kuchukua jiko.
RECHO AGOMA KUJIBU
Recho alipoulizwa kuhusu taarifa
hizi kama zimesheheni ukweli wowote, alikataa kujibu kwa madai kuwa kwa wakati
huo alikuwa na mambo mengi ya kufanya hivyo atafutwe baadaye. Hata alipotafutwa
baadaye, hakuwa tayari kutoa ushirikiano.
MAJIBU YA MASAI
Alipoulizwa kuhusu tetesi hizi,
Masai (Mc Kapalalai), alisema kwa sasa hayuko tayari kulizungumzia suala hilo,
jambo linaloleta utata na kutufanya tuamini kuwa huenda wawili hao wako
mapenzini.
Recho na Mc Kapalalai (Masai), ni
waigizaji wa tamthiliya ya Siri za Familia. Tamthiliya hii, huzungumzia maisha
halisi na purukushani kedekede zinazotokea katika familia zetu.
Dalili zote zinaonyesha kuwa,
wawili hao ni wapenzi wa kwelikweli na si maigizo tena. Mapenzi hayajifichi,
punde mambo yote yatakuwa hadharani.