Jinsi ya kuandaa Somo na Kuwasilisha Oral Interview Ajira za Walimu

Mwalimu anawasilisha somo oral interview ajira za walimu
Nililia kwa uchungu, sikuamini kwamba, yote niliyomfanyia Ashura, mchepuko niliyekuwa na malengo naye, aliyaona hayafai. Ni mimi ndiye niliyempa mbinu zote za kufaulu usaili ajira za walimu, bidii yote na uwekezaji niliofanya, Ashura kaniacha!

Niliisoma upya meseji yake ya mwisho, “Mwalimu Makoba, asante kwa msaada wako, ni wewe uliyenisaidia mpaka nimepata ajira ya ualimu mkoani Dodoma, hata hivyo, siwezi tena kuendelea na wewe kwa sababu mbili: kwanza, una mke na mimi sipo tayari kuwa mchepuko, ninahitaji maisha yangu; pili, nimepata mume mkulima wa zabibu tena anayeijua dini vizuri, wewe hueleweki dini yako; japo umesoma, lakini elimu imeshindwa kukubadilisha, bado unafuata tamaduni za Kisukuma ikiwemo kuabudu mizimu!”

Nilipomaliza kuisoma, nililia upya, mke akaamka na kuniuliza shida nini? Nilidanganya, “Nimemkumbuka marehemu bibi!”

Nilikumbuka jambo moja muhimu, msafara wa Rais ungepita karibu na mtaa wetu, na rais angesimama kusikiliza kero za wanachi. Nilitembea haraka nami nikaeleze kero yangu, aliyonifanyia Ashura lazima Rais ayajue. Sijawahi kuvuta sigara, lakini njiani nilinunua moja, nikavuta pafu moja nikakohoa kama mbwa nikaitupa na kuikanyanga kwa hasira.

Nilipofika nilikuta rais amekwisha simama akisikiliza kero za wananchi, nami nikaunyoosha mkono, baada ya bibi mmoja kusikilizwa kero yake, nikapewa kipaza sauti, nimwage ya rohoni!

Nikiwa nimeshika kipaza sauti nilikumbuka mimi ni mwalimu ninayeheshimika, kamera zote zilimulika mahali nilipo na pengine nchi nzima ilikuwa ikitazama, nikawaza kuhusu wanafunzi wangu, nikasema hapana, nikabadili mada.

“Jamani mitano tenaaa!” nilisema kwa sauti yenye uchangamfu wa kuigiza, watu wakashangilia. Kipaza sauti kikachukuliwa na kupewa mtu mwingine.

Mahali hapo hapakunifaa, niliondoka na kuelekea ofisini, nilifungua droo kwa nguvu na kutoa bastola yangu pendwa aina ya Bereta 92 X, kisha nikainyanyua juu na kutamka kwa sauti, “Kwa heri Dunia, Kwa heri ya kuonana!”

Lakini ghafla sauti ya kike ilibisha hodi, nikairejesha bastola katika droo kisha nikaruhusu, “Ingia!”

Aliingia binti mrembo, rangi yake maji ya kunde, mbele ntinti, nyuma ntinti, umbo namba nane, midomo minene tena mwenye ‘thigh gape’ na alitembea kwa madaha akajibwaga katika kiti mbele yangu.

“Binti unalo jina?” Niliuliza nikimeza mate.

“Ninaitwa Ramona,” alijibu.

“Karibu Ramona, leta maneno!”

“Mimi hapa…” alizungumza Ramona akiibenjua midomo yake, damu yangu ikaanza kwenda mbio nami nikazidi kumsikiliza, “Nimechaguliwa kwenda oral interview somo la Kiswahili, nimefaulu ‘writen’ baada ya kusoma nondo zote za kufanya nifaulu mtihani katika mtandao wako, sasa nimeona nije unielekeze namna ya kuandaa somo na kuliwasilisha.”

Nilinyanyuka katika kiti, nikampeleka mahali palipokuwa na meza na ‘benchi’, nikaanza kumfundisha.

Jinsi ya Kuandaa Somo

Utakapofika katika usaili huu wa mazungumzo, kitu cha kwanza kupewa itakuwa karatasi, katika karatasi hiyo utatakiwa kuandika somo lako. Nenda ukiwa umejiandaa kwani utaandika somo hilo kutoka kichwani.

Kama utapewa karatasi ambayo baada ya kuandika ilibaki nafasi, tunashauri uandike na  ‘lesson plan’ baada ya hilo somo lako.

Unapoandika somo, chagua mada utakayofundisha, siku hizi wanaita umahiri.

Huu ni mfano wa somo lililoandaliwa kutoka mada ya kwanza kiswahili kidato cha kwanza muhtasari mpya:

UMAHIRI MKUU: KUMUDU MISINGI YA KISWAHILI

UMAHIRI MAHSUSI: Kutambua Kiswahili Kama Kielelezo Cha Utaifa Na Utambulisho Wa Mtanzania

Lugha ni mfumo maalumu wa sauti za nasibu wenye kuleta maana, uliokubalika kutumika katika kuwasiliana miongoni mwa wanajamii wenye utamaduni mmoja.

Mfumo wa lugha huhusisha sauti, silabi, maneno, sentensi na maana.

Lugha ya Kiswahili nikieleleozo cha utaifa na utambulisho wa Mtanzania. Kokote aliko Mtanzania, hutambulishwa na lugha ya Kiswahili.

Watanzania wanapokuwa katika mijadala mbalimbali, huzungumza kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.

Watanzania wanapozungumza, ili kulinda utamaduni wao, huzingatia: matumizi ya tafsida, na uteuzi wa maneno kulingana na mila na desturi zao.

Matumizi ya Tafsida

Tafsida ni tamathali za semi ambazo hutumika kupunguza ukali wa maneno.

Utamaduni wa Mtanzania hauruhusu kutaja maneno ya matusi, hivyo hutafutwa maneno mbadala ilikupunguza ukali wa maneno. Kwa mfano, badala ya kusema ninakwenda chooni, Watanzania husema, ninakwenda uani.

Watanzania huteua maneno yao kwa uangalifu mkubwa, wao huzingatia mila na desturi zao katika uteuzi huo.

Jinsi ya Kuwasilisha Somo

Wapo wanaosema unapowasilisha, wasilisha kama upo katika semina, Ashura alipata ajira kwa kuwasilisha kama yupo katika semina za chuo. Hata hivyo, sishauri tena matumizi ya njia hii, badala yake nashauri uwe kama unayefundisha darasani tena ukitumia mbinu zaidi ya moja. Zingatia kwamba, unapofundisha, epuka kuwafanya wale wanaokusaili kama watoto wadogo!

Anza Namna Hii

Wasalimie kama unayesalimia wanafunzi. Chukua chaki, gawa ubao mara tatu, katikati ya ubao andika KUMUDU MISINGI YA KISWAHILI, halafu andika tena,  Kutambua Kiswahili Kama Kielelezo Cha Utaifa Na Utambulisho Wa Mtanzania, kulia andika tarehe, Kisha zungumza hivi:

Wanafunzi wangu mkiwa katika vikundi, leo nitawaongoza kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utamaduni wa Mtanzania katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Mkiwa katika vikundi sikilizeni habari hii kuhusu kijiji cha Safina.

Halafu simulia hivi:

Kijiji cha Safina kilikuwa na wakazi wenye makabila anuai. Wakazi wa kijiji hicho hawakuweza kuwasiliana kwa sababu walitumia lugha tofauti. Mwaka fulani kulitokea ukame katika kijiji hicho, hali iliyodumu kwa muda mrefu. Kutokana na hali hiyo, iliwalazimu wananchi hao kuhamia karibu na chanzo cha maji ili waweze kupata huduma ya maji. Wanakijiji hao waliinua kwa pamoja kwa kipindi chote cha ukame, hali iliyofanya kuwa na msamati unaofanana kutokana na baadhi ya maneno kutumika mara kwa mara miongoni mwao.

Baada ya muda kupita, wanakijiji hao walijikuta wana mfumo mmoja wa mawasiliano ambao uliweka miongoni mwa wanakijiji wote. Kuanza hapo, watu wa Kijiji cha Safina wakakubaliana kutumia mfumo huo wa mawasiliano. Muda ulivyozidi kuendelea, walijikuta wanaujua na kuutumia mfumo huo bila mafundzo rasmi. Mfumo huo uliobuka kinasibu ulikuwa na mpangilio maalumu wa sauti, silabi, maneno na sentensi ambao unaleta maana. Walielelea kuongeza maneno katika lugha hiyo kadiri walivyokutana na dhana mpya katika mazingira yao kwa kutumia mfumo wa lugha hiyo. Majina yao na ya maeneo yao yaliendelea na maana na dhana kama zilivyokubalika katika jamii yao. Hivyo, maana za maneno yao ziliitambulisha jamii yao kupitia mfumo wao wa mawasiliano.

Aidha, mfumo huo uliwafanya wanakijiji hao waanze kuelewana katika mazungumzo yao na kufanya shughuli mbalimbali kwa pamoja. Walianza kuwasiliana kwa kutumia mfumo wao kwa kuzungumza kisha wakajifunza kuandika.

Wakazi wa kijiji hicho waliinua maisha yao kupitia mfumo huo wa mawasiliano kwani ulitumia na watu wote. Hivyo, jamii ya Safina haikuwa na namna nyingine ya kueleza masuala yake pasipo kutumia mfumo huo wa mawasiliano. Kwa hakika, wakazi wa Kijiji cha Safina walijenga uhusiano mzuri miongoni mwao kama wanajamii moja. Sanjari na hayo, mfumo wa mawasiliano wa Kijiji cha Safina uliwawezesha wanakijiji hao kufikiri, kuhifadhi na kutiririsha maarifa na amali zao kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Vilevile, kupitia mfumo huo wa mawasiliano, watu wa kijiji cha Safina waliweza kutambua kila walipokuwapo kwani walijitofautisha na wazungumzaji wa mahali pengine kutokana na uzungumzaji wao.

Pia, waliweza kuendeleza utamaduni wao na kuongeza maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia mfumo wa mawasiliano walioutumia. Hivyo, Kijiji cha Safina kilifanikiwa kukua na kuwa na maendeleo makubwa sana.

Ukimaliza kusimulia, waulize maswali haya, wasipoyajibu, toa majibu mwenyewe, tena ukiwa unajiamini.

Maswali

1. Unafikiri mfumo uliotumiwa na wanakijiji wa Safina katika kuwasiliana unaitwaje?

2. Umejifunza nini kuhusu dhana ya lugha kutokana na habari uliyoisoma?

3. Vipengele gani vya lugha hujenga mpangilio wa mfumo wa mawasiliano kwa mujibu wa habari uliyoisoma?

4. Kuna uhusiano gani kati ya lugha na jamii kulingana na habari uliyoisoma?

5. Kutokana na habari uliyoisoma, lugha ina dhima zipi?

Utakapomaliza kuwasilisha hapa, utaelekea hatua ya pili, hatua ya kuulizwa maswali. Hatua hii nimeieleza vyema katika kiunganisha hapa chini.

Soma: Mbinu 4 na Maswali 50 Kusaidia Ufaulu Oral Interview Ajira za Walimu

Baada ya maelekezo hayo Ramona aliniahidi kunipa ‘zawadi ya ushindi’ endapo mbinu nilizompa zingemfanya afanikiwe kupata kazi, niliagana naye.

Sikuchukua namba yake ya simu, hivyo kilipita kimya cha wiki mbili bila kusikia habari zake. Lakini siku moja nikiwa ofisini, Ramona aliingia akiwa mwenye furaha, nilimsikia akisema, “Asante Mwalimu, nimeajiriwa… nimepelekwa kufundisha mkoani Shinyanga… nilikuahidi zawadi ya ushindi, mimi sasa ni wako, ukitaka nitafune, ukitaka nimeze mzimamzima!”

Sikuwa na maneno mengi, niliukamata mkono wa Ramona, nikampeleka upande wa pili wa ofisi yangu ambako haruhusiwi mtu mwingine kuingia bila ruhusa.

Angalizo

Kwa kuwa mtandao wetu husomwa na watu wengi, tunashauri uandae somo jipya kwani kutumia somo hilo lililotumiwa kama mfano huenda ukarudia alichofanya mwenzako na kukunyima nafasi ya kusonga mbele. Endapo unahitaji Kusaidiwa Kuandaa Somo Kama hilo Gharama yake Ni Tsh. 9,000/= tu. Kuandaliwa, Wasiliana na Mwalimu kwa Kugusa Hapa

Popular posts from this blog

SMS 20 za Vichekesho Zinazochekesha Sana

Nondo Zote za Kukusaidia Kufaulu Mitihani Usaili Walimu Masomo Yote

Maswali 100 Kujiandaa na Mtihani Usaili Walimu Masomo Yote