Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1

Watu wanacheka

1. Kukosa hela ni vibaya sana, unaweza kukutana na ng’ombe ukahisi wanakusema.

2. Kama huna gari, huna nyumba, huna simu na huna hela, tofauti yako na kenge ni mkia.

3. Siyo kila anayeamka saa sita mchana ni tajiri, wengine wanapunguza saa za kuteseka.

4. Mtu mmoja aliota anaendesha gari, ikakwama kwenye matope, akaanza kuisukuma. Alipoamka, akajikuta yupo na kitanda jikoni.

5. Maisha ni ya ajabu sana, unakuta mtu hajaoa lakini chumba anachoishi kuna panya wana familia zao na yeye ndiyo anawalisha.

6. Ukiwa ugenini usinyamaze sana. Wenyeji wanaweza wakadhani unafikiria kuwaua.

7. Kila mtu anauogopa usiku. Kichaa mmoja alisikika akisema, “Usiku umeingia waniroge tena.”

8. Pombe mbaya, nimekutana na mlevi anatafuta wanawake wembamba atengeneze fagio.

9. Niliwahi kupanda basi, dereva analalamika njia nzima, “Nimefanya kazi miaka mingi, mafanikio hakuna. Sasa leo mwisho.” Abiria wakaanza kuomba kushuka mmojammoja.

10. Mchana hupati hela, usiku hupati usingizi. Kwa kifupi hupatikani.

11. Dalili nyingine ya umasikini ni kusafiri na mswaki.

12. Ushawahi kukosa kila kitu, hata ukiombwa msamaha unasema huna?

13. Hata ukienda umevaa suti kwenye harusi, haipotezi lengo kuwa umefuata wali.

14. Msukuma mmoja alikataa kulipa nauli kwa sababu yeye ni birthday Boy.

15.        Usiibiwe tena mchele, kilo moja ina punje 168,370.

16.        Tangu nizaliwe mpaka leo sijui kuogelea. Hata hivyo sijali kwa sababu sijawahi kuona samaki anayetembea.

17.        Dunia imebadilika sana. Siku hizi mtoto kunywa uji mpaka awekewe katuni. Enzi zetu unabanwa pua uchague kufa au kumeza.

18.        Huna hela halafu unajiombea maisha marefu, ukipewa hayo maisha marefu utakula nini?

19.        Mlioenda Dar kutafuta maisha, mkiyaona yangu mniletee.

20.        Sijui nipangishe chumba changu nilichopanga?

21.        Rafiki yangu alikuwa msibani analia. Aliponyamaza, akajisachi mfukoni na kugundua simu haipo. Akaanza kulia tena.

22.        Mwaka mmoja nikiwa katika mwaliko wa chakula, nilisema hii nyama ng’ombe alikua jike. Wakaniuliza kwa nini? Nikawajibu ni tamu sana.


Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024