Jinsi ya Kuomba Chuo kwa Usahihi

Jengo la Nkrumah Hall Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kama umehitimu kidato cha sita au umehitimu chuo kwa ngazi ya stashahada (diploma) na una sifa za kuomba chuo, maelekezo haya yatakusaidia uombapo chuo.

Kwanza tufahamu ni mtu gani mwenye sifa za kuomba chuo?

Kwa mujibu wa mwongozo wa TCU kuhusu sifa za kuomba chuo, wamegawanya waombaji katika makundi kadhaa. Miongoni mwa makundi hayo ni wale wanaoomba kutoka kidato cha sita, na waombaji wanaotoka vyuo vya kati.

Sifa za mwombaji Kutoka kidato cha sita

Aliyemaliza kidato cha sita kabla ya mwaka 2014 anatakiwa awe na ‘principle passes mbili zinazoleta jumla ya alama 4.

Mgawanyo wa alama umekaa katika mfumo huu: (A=5; B=4; C=3; D=2; E=1; S=0.5)

Aliyemaliza kidato cha sita mwaka 2014 na 2015 anatakiwa awe na ‘principle passes’ mbili (C na kuendelea) akiwa na jumla ya alama 4 katika masomo mawili.

Mgawanyo wa alama umekaa katika mfumo huu: (A=5; B+=4 B=3; C=2; D=1; E=0.5)

Aliyemaliza kidato cha sita mwaka 2016 na kuendelea anatakiwa awe na ‘Principle passes’ mbili yenye jumla ya alama 4 katika masomo mawili.

Mgawanyo wa alama umekaa katika mfumo huu: (A=5; B=4; C=3; D=2; E=1; S=0.5)

Mwanafunzi mwenye C na E anaweza kupata chuo?

Ndiyo, anaweza kupata chuo. Kwa sababu C ina alama tatu na E ina alama moja, hivyo anakuwa amefikisha jumla ya alama nne zinazotakiwa.

Sifa hizo, zinaelezwa katika jedwali hili:

Jedwali likionyesha alama stahili kidato cha sita

Kwa wanafunzi wanaoomba kozi za afya, wanatakiwa angalau wawe na D tatu katika masomo yao na wawe na jumla ya alama 6.

Sifa za Kuomba Chuo kwa Wenye Diploma

Awe amefaulu masomo manne kutoka kidato cha nne. Masomo hayo, yasiwe ya dini. Kufaulu maana yake awe amepata angalau alama D.

Pia, awe amepata wastani wa GPA ya 3.0 katika matokeo yake ya diploma.

Sifa hizo kwa ujumla, zinaonyeshwa katika jedwali hili:

Jedwali la alama kwa waombaji wa diploma


Kwa mwanafunzi mwenye sifa, anatakiwa kuomba chuo kupitia njia ya mtandao. Maombi yanaombwa moja kwa moja katika chuo husika na kwa kila ombi utakalofanya, gharama yake ni tsh. 10,000/=.

Inashauriwa mwanafunzi aombe angalau vyuo vitatu, endapo ataomba vyuo vingi zaidi, basi visizidi vitano. Kwa mfano, kwa mwanafunzi anayetaka kusomea fani ya Ualimu, anaweza kuomba Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, DUCE na Mkwawa.

Baada ya maombi yako ya kwanza, endelea kufuatilia majibu ya dirisha la kwanza. Katika dirisha la kwanza, unaweza kupata chuo ulichotaka au unaweza kukosa kwa sababu ya ushindani. Usiwe na wasiwasi, dirisha la pili litafunguliwa na utaelekezwa vyuo vyenye nafasi ambazo unaweza kutuma maombi yako.

Hivyo basi, wanafunzi wanashauriwa kabla ya kuomba vyuo, wasome mwongozo kutoka ‘TCU guide book’ ili wafanye maombi sahihi na wasipoteze pesa zao kwa kufanya maombi ambayo hayaendani na sifa zao.

Soma: Jinsi ya Kuomba Mkopo

Kwa wanafunzi wanaohitaji usaidizi wa kuombewa vyuo, tunatoa huduma hiyo kwa punguzo la bei. kwa wale wanaoomba vyuo vitatu, gharama yetu ni tsh. 50,000/= tu, mgawanyo wa malipo ni, 30,000/= itatumika kama malipo kwa vyuo husika, na tsh. 20,000/= itatumika kama gharama ya kufanyiwa maombi, Gusa Hapa kuwasiliana na Mwalimu na kuanza kufanyiwa maombi yako.

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Hotuba