Mada za History Zinazotoka Zaidi Katika Mtihani Kidato cha 4

Sanamu udongoni.
Nimekuwa nikiulizwa swali hili na wanafunzi wangu wengi. “Mwalimu ni mada gani zinapenda kutoka katika mtihani wa History kidato cha nne?” wanaouliza swali hili wamegawanyika katika makundi matatu:

Kundi la kwanza ni wanafunzi wavivu, wanataka wajue mada zinazotoka katika mtihani ili wasome hizo tu na wasihangaike kusoma mada zingine.

Kundi la pili ni wanafunzi wanaotaka kufahamu waweke msisitizo wa kusoma mada gani zaidi.

Na kundi la mwisho, huuliza bila kuwa na sababu maalumu, wao huuliza tu.
Nasisitiza kuwa, siyo kosa kutaka kufahamu mada zinazotoka zaidi katika mtihani wa History kidato cha nne.

Ni mada gani hutoka zaidi katika mtihani wa History kidato cha nne?

Mada zote hutoka katika mtihani wa kidato cha nne. Ili uweze kufaulu mtihani wako wa History, unashauriwa usome mada zote za kidato cha kwanza, pili, tatu na nne, utaweza kufaulu vizuri mtihani wako.

Pia, lengo la somo la History siyo kufanya mtihani pekee, lengo kuu ni kukupa maarifa ya Historia yako ili utambue ulipotoka, ulipo na unapokwenda.

Baada ya kuwa umesoma mada zote, sasa tambua ya kwamba, kuna mada zina alama nyingi zaidi katika mtihani kwani mada hizi hupenda kutoka katika maswali ya maelezo. Mada hizo ni:

Establishment of colonialism, Colonial administration, Colonial Economy, Colonial social services, Crises na nationalism and decolonization.

Wakati mada zote hutoka katika mtihani wako, inawezekana mada tajwa hapo juu zikawa na alama nyingi zaidi kuliko mada zingine.

Zingatia kwamba hayo ni maoni yangu tu, kwani inawezekana maswali mengi ya kujieleza yakatoka kidato cha kwanza au cha pili.

Sasa nakuomba ufuate kile ambacho nimekuwa nikiwaeleza wanafunzi wangu ambao siku zote hufaulu mitihani yao ya History kwa alama zenye kuacha tabasamu:

“Hakuna mada zinazopenda kutoka katika mtihani wa History, mada zote hutoka na jambo la msingi ni kusoma mada zote yaani, mada nne kidato cha kwanza, mada nne kidato cha pili, mada nne kidato cha tatu na mada nne kidato cha nne.”

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne