Vunja Mbavu SMS za Vichekesho Utacheka Sana
1. Upo na funguo zake au ukifika unaanza kugonga kama mtu wa taka?
2. Majirani wanashangaa kama hawajawahi kuona mtu anachinja kunguru.
3. Huyo mtu wako ipo siku atakupeleka kwao na mtafukuzwa wote.
4. Umetulia zako huna 'stress' mara ghafla unakumbuka umri wako.
5. Ubaya ulianza pale alipoambiwa, "si kwa ubaya, una kichwa kama mwiko."
6. Leo nimechoka kama mahusiano yako.
7. Sumbua mtu hata kama ana mtu, hakuna mtu wa mtu sisi ni watu wa Mungu.
8. Ukiwa huna hela, ukikunja nne mguu unakufa ganzi.
9. Tunakuzika na suti halafu ndotoni unatutokea na kanzu, ina maana suti yetu umeuza?
10. Mume wako yuko bar, anafungulia demu wake bia na pete yenu ya ndoa.
11. Ukimshitaki mtu polisi malizia hivi, "Alisema hata nikimshitaki hawaogopi polisi."
12. Hili jua litaniulia marafiki zangu waliojichubua.
13. Unapokuwa unaumwa, unapoandika wosia jitahidi basi uwe na uhalisia na uwezekane. Mtu anaumwa halafu anasema nikifa nizikeni ikulu... We unaona inawezekana?
14. Heshimu watu ambao hawatumii pombe, siyo rahisi kuondoa stress na juisi ya miwa.
15. Tafuta mtu anayekupenda hadharani ndugu yangu. Wewe siyo bangi!
16. Mwalimu: Mwanao anatupa wakati mgumu shuleni, tunaomba uje shule tuzungumze.
Mzazi: Mwalimu, hata sisi huyo mtoto anatupa wakati mgumu hapa nyumbani na hatujawahi kukuita.
17. Leo nayo nimechoka kama mahusiano yenu.
18. Kuwa na mpenzi anayejitafuta shida sana. Saa 9 usiku unasikia, "oyaaa... Amka nimepata mteja wa godoro."
19. Nisimame kwenye daladala halafu nisisome meseji za waliokaa! Hamnifahamu vizuri.
20. Mpenzi wako ana kichwa kama mwiko lakini unataka kumwambia ukweli ila hutaki kugombana naye kwa hivyo unamwambia, "una kichwa kama mwiko wa dhahabu."
Pata Kitabu Kilichosheheni Vichekesho Vitakavyokurudishia Furaha Yako na Kukufanya Mwenye Afya Tele, Gusa Hapa Kujipatia Nakala Yako
