Pre Form One Course 2025 | Pre Form One Notes

Wanafunzi wa Pre form One wakiwa wamekaa darasani.

Mwalimu Makoba Open School inawatangazia Masomo ya Pre Form One. Masomo haya yanawahusu wanafunzi wote ambao wamemaliza darasa la saba.

Gharama zetu ni Tsh. 50,000/= (elfu hamsini tu) kwa kozi yote ya miezi mitatu.

Tunapatikana Dar es Salaam, Kinondoni, Mtaa wa Kambangwa karibu na De Mag Hotel.

Wanafunzi wa pre form one watafundishwa masomo (Pre form one subjects) haya:

English course (Pre form One English Course) ili kuwafanya wafahamu lugha ya kiingereza. Masomo mengine ni: Physics, Chemistry, Mathematics, Biology, Geography na History.

Katika kituo chetu tuna notes nzuri za pre form one (pre form one notes) ambazo zimeandaliwa vyema kueleweka kwa wanafunzi wetu.

Faida za Masomo ya Pre Form One

Masomo ya pre form one yanamsaidia mtoto aliyemaliza darasa la saba, awe tayari na masomo yake ya kidato cha kwanza pindi atakapoanza elimu yake ya sekondari.

Kumbuka kwamba, wanafunzi wengi husoma masomo yao kwa lugha ya Kiswahili, wanapoanza sekondari, lugha hubadilika ghafla na kuwa Kiingereza, hapa ndipo hitaji la pre form one linapokuja ambapo mwanafunzi huweza kuandaliwa kwa ajili ya kuyamudu masomo yake.

Kwa hivyo basi lengo kuu hasa la pre form one ni kumsaidia mwanafunzi kufahamu lugha ya kiingereza ambayo ndiyo lugha kuu inayotumika kufundishia katika shule za sekondari. Kumbuka kuwa, mwanafunzi anapoanza kidato cha kwanza, hasubiliwi, bali masomo huendelea bila kujali kuwa anaelewa lugha au la.

Kwa kuongezea, masomo ya pre form one huwaondolea hofu wanafunzi juu ya kile watakachokutana nacho sekondari. Huwaandaa kiasi kwamba, wanapoanza masomo yao huwa tayari wamefahamu nini kinachohusika.

Pre form one inaokoa muda. Mwanafunzi anafahamu mapema kinachohusika huko na kumfanya aweze kufaulu vyema masomo yako aanzapo kwani huwa mbele ya wenzake ambao huwa hawajasoma pre form one.

Karibu sana, mlete mwanao asome nasi. Silabasi mpya imezingatiwa katika ufundishaji wetu.

Unaweza kuwasilina nasi kwa simu namba: 0653 250 566.

Karibuni sana.

Popular posts from this blog

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe