Jinsi ya Kufahamu Kiingereza cha Kujibia Mitihani
Changamoto
kubwa inayowakumba wanafunzi ni kumudu lugha ya kiingereza. Wapo wanafunzi
ambao wanayaelewa vizuri masomo yao lakini tatizo linakuja katika kueleza
majibu yao ambapo masomo yote isipokuwa Kiswahili hutumia lugha ya kiingereza.
Kushindwa
kumudu lugha ya kiingereza kunachangiwa na matumizi finyu ya lugha hii nchini.
Watanzania wengi hutumia lugha ya Kiswahili katika shughuli zao za kila siku,
hivyo wanafunzi wamekosa nafasi ya kufanya mazoezi ya kuzungumza lugha hii.
Kama
wewe ni miongoni mwa wanafunzi ambao wanashindwa kujibu mitihani na kupata
matokeo mabaya kwa sababu ya kushindwa kuimudu lugha ya kiingereza, fanya mambo
haya:
1.
Sikiliza
lugha ya kiingereza
Sikiliza
mtu yeyote anayeongea lugha ya kiingereza hata kama huelewi. Sikiliza taarifa
ya habari, watu wakizungumza katika televisheni na mwalimu akifundisha
darasani.
2.
Zungumza
lugha ya kiingereza
Kiingereza
kwa Watanzania wengi huambatana na aibu. Kama una aibu kuzungumza lugha ya
kiingereza mbele ya kundi la watu, tafuta marafiki uliowazoea kisha andaeni
ratiba ya kuzungumza lugha ya kiingereza. Siyo lazima mzungumze kiingereza kila
siku na kila mahali, ila mnaweza mkatengeneza ratiba ya kuzungumza kiingereza
hata mara mbili kwa wiki kwa muda wa saa kadhaa.
3.
Andika
kwa lugha ya kiingereza
Fanya
mazoezi ya kuandika vitu mbalimbali. Andika insha za darasani, andika makala na
vingine vingi ilimradi ufanye mazoezi ya kutosha katika kuiandika lugha hii.
4.
Soma
maandishi ya kiingereza
Soma
vitu mbalimbali vilivyoandikwa katika lugha ya kiingereza. Soma magazeti,
vitabu na makala mbalimbali katika lugha ya kiingereza. Wakati unasoma vitu
hivi, hakikisha una kamusi pembeni ili pale utakapokutana na neno usilolifahamu
uweze kutazama maana ya neno hilo. Usisome bila kamusi pembeni. Kamusi ni kifaa
kitakachokusaidia kupata maana ya maneno mbalimbali ya kiingereza na hatimaye
kusaidia kukuza msamiati wako.
5.
Jifunze
lugha ya kiingereza
Zipo
njia mbalimbali utakazotumia kujifunza lugha ya kiingereza. Unaweza kujifunza
lugha hii kwa kusoma vitabu mbalimbali au kutafuta mwalimu ambaye atakufundisha
vyema. Wakati ukifundishwa, usisahau kufanya mazoezi.