Fasihi ya Watoto na Vijana | KF 203

Mwezi mzima ukionekana wakati wa usiku.

Fasihi ni Sanaa ambayo hutumia lugha kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa.

Fasihi ya watoto na vijana ni aina ya sanaa ambayo inatumia lugha kufikisha ujumbe kwa watoto na vijana.

Mtoto ni nani?

Linaweza kutafsiriwa kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kimuktadha:

Kiimani

Kibaiolojia na Kiumri

Wafura (2011) amegawanya watu katika makundi manne:

i. 0-17 watoto

ii. 18-34 vijana

iii. 35-52 utu uzima

iv. 53 na kuendelea, wazee

Mamlaka za kiserikali na mashirika mbalimbali yanamtambua mtoto kuwa mtu yeyote ambaye ana umri wa chini ya miaka 18.

Kuna watoto wadogo na watoto wakubwa (vijaluka). Vijaluka ni watoto wakubwa ambao wako katika umri wa kujitambua.

Mtazamo mwingine kuhusu fasihi ya watoto:

Wamitila (2008) anasema suala la ufafanuzi wa fasihi ya watoto linaweza kueleweka kwa kutumia mitazamo miwili:

i. Kuwalenga watoto kama hadhira.

ii. Ni ile ambayo maudhui na dhamira zilizopo zinawarejelea watoto.

Mtazamo mwingine:

Ni aina ya sanaa ambayo watumizi wake ni watoto.

Ili kuweza kutambua fasihi ya watoto, zipo nduni (sifa) mbalimbali.

i. matumizi ya picha, vielelezo na michoro.

Lengo la kutumia hivyo ni:

-      Picha yaweza tumika kama simulizi hata kama mtoto hajaweza kusoma.

-      Wahusika wake wakuu, nguli au shujaa lazima wawe watoto. Hata hivyo, hii haimzuii mwandishi kutumia wahusika watu wazima.

-      Hutumia lugha rahisi.

-      Huwa na visa vichache.

-      Hujengwa katika msuko sahili wa matukio. Muundo mwepesi.

-      Hutumia sana fantasia. Fantasia ni matumizi ya mambo ambayo hayapo katika ulimwengu wa kawaida.

Kwa nini mwandishi hutumia fantasia?

-      Huburudisha

-      Humjengea mtoto au hadhira taswira mbalimbali.

-      Huhusisha milango mingi ya fahamu. Mtunzi hutumia viungo vya mwili, picha na maelezo yanayomwezesha kuhisi harufu fulani na vitu fulani ambavyo humjengea picha kichwani mwake. Watoto hupenda kusikia, kuona, kunusa na kugusa badala ya maneno matupu.

-      Maisha ya wahusika huanzia na kuishia nyumbani. Sababu ni kuwa, mtoto hana uwezo wa kujitegemea hivyo wahusika lazima waishie nyumbani hata kama akiondoka lazima atarudi. Mfano, kitabu cha Bahati na Mwewe.

-      Mambo mema ndiyo matarajio. Lengo ni kuwajengea watoto mtazamo chanya.

-      Hutumia mbinu ya kurudiarudia. Mfano, marudio ya sentensi au neno. Lengo ni kuwawezesha walengwa waelewe kinachowasilishwa.

-      Kazi za watoto hujikita katika motifu ya safari na motifu ya msako. Motifu ni kipengele kinachojirudiarudia ambacho huweza kuwa cha kijamii au kimaudhui, kinachotokea katika kazi za fasihi. Mfano, motifu ya majambazi matatu, saba n.k

Vitabu vingi vina motifu ya Bibi Kizee Mchawi.

Motifu ya safari na msako.

Msako wa kitu kilichopotea.

-      Fasihi ya watoto inajali saikolojia ya mtoto. Inazingatia mtoto anapenda nini na hapendi nini?

Dhima ya fasihi ya watoto na vijana

i. Kuburudisha, Hii ni dhima kuu, mtoto anaweza kuburudika kwa kuangalia picha, jinsi lugha inavyotumika kumfuatilia mhusika fulani n.k

ii. Kumuondoa mtoto katika hali aliyonayo mpaka katika hali bora zaidi. Usomaji wa hadithi husaidia mtoto kuongeza ufahamu.

iii. Kuchachawisha ubunifu (kuhamasisha). Kazi nyingi za fasihi zinamfanya mtoto aweze kufikiria kuhusu mazingira fulani.

iv. Humsaidia mtoto kujielewa na kuwaelewa wengine.

v. kupata uzoefu na kuelewa umbo la lugha.

vi. husaidia katika kujifunza masomo na mada mbalimbali.

Aina za fasihi

Fasihi simulizi za watoto na fasihi andishi za watoto.

Bunilizi (fiction), si bunilizi (nonfiction)

Bunilizi ni ubunifu.

Kazi zinazopatikana katika bunilizi ni:

Ngano, visasili, visakale, visafuli, hadithi fupi, novela, riwaya, tamthiliya, ushairi, semi, michezo ya watoto…

Visasili hueleza sababu ya matukio fulani, mfano, kwa nini sungura ana mkia mfupi.

Novela haina uchangamani wa visa na matukio kama riwaya.

Aina za bunilizi

Zinatokana na kuangalia bunilizi imetawaliwa na nini, imetokana na nini, ikoje?

i. Bunilizi ya kifantasia

hii imetawaliwa na mambo ya ajabu ajabu. Mamboya njozi. Mara nyingi hutawaliwa na wanyama, huwa katika ulimwengu dhahania, hutawaliwa na nguvu za ajabu, vikaragosi…

ii. Bunilizi ya kisayansi (saifa)

Ni kazi ya sanaa ambayo imetungwa kwa kuegemea kwenye sayansi yaani matukio ambayo yanaweza kuthibitishwa kisayansi.

iii. Bunilizi ya kihistoria

Hii imeegemea katika mambo ambayo yamekwishatokea.

iv. Bunilizi ya kihalisia

Katika bunilizi hii, kuna mhusika wa kweli ambao wanapatikana katika ulimwengu halisi.

Si bunilizi

Ni kazi ya sanaa ambayo mambo au matukio ya kweli hutawala zaidi kuliko iliyo katika bunilizi.

Si bunilizi huwa na taarifa za watu za kweli katika dunia halisi. Hulenga kutoa taarifa au kuonyesha.

Aina zake:

Tawasifu

Kumbukumbu

Hadithi

Ni masimulizi au kisa kinachohusu suala fulani kwa muhtasari na mara nyingi huwa na mhusika mmoja aliyejitokeza sana ingawa hakuzwi kwa mapana yake kama ilivyo katika riwaya.

Matei (2011) anaeleza hadithi kama masimulizi yanayowasilishwa kwa lugha ya kinathari kuhusu watu, matukio na mahali mbalimbali.

Hadithi huwa haina upana wa kimaudhui au uchangamano wa visa au matukio kama ilivyo katika riwaya.

Katika hadithi, huwa kuna fanani na hadhira, pia, huweza kuwa ya ukweli au kubuni lakini ikiwa na maadili fulani.

Sifa zinazobainisha hadithi

I.        Haitumii wahusika wengi.

II.        Inahusu jambo moja kubwa lililowekwa katika utamaduni wa hadhira husika.

III.        Ni masimulizi ya kubuni.

IV.        Haina uchangamano wa visa au inatakiwa iwe na muundo sahili.

V.        Inaeleza matukio kwa mpangilio wa moja kwa moja. Kuanzia tukio la mwanzo au la mwisho.

VI.        Huwa na mgogoro au tukio la kuelezea.

Riwaya

Wataalamu mbalimbali wanajadili kwa kutumia vigezo na sifa tofautitofauti. Mphahlele (1976) riwaya ni masimulizi ya kinathari yenye maneno kati ya 35,000 mpaka 75,000. Riwaya fupi inaanzia maneno 35,000 mpaka 50,000 na ndefu inafika mpaka maneno 75,000.

Mhando na balisidya (1976) wanakubaliana na Mpahlele kuhusiana na kigezo cha urefu.

Senkoro (2011) tukitumia kigezo cha urefu tutapata riwaya chache sana katika fasihi ya Kiswahili.

Senkoro anasema, riwaya ni kisa mchangamano ambacho huweza kuchambuliwa na kupimwa mapana na marefu, kifani na kimaudhui.

Riwaya ni kisa au mkusanyiko wa visa.

Riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye visa vingi, wahusika wengi na inayoangalia mambo muhimu katika jamii.

Vipengele muhimu katika kueleza maana ya riwaya:

        Uchangamano wa visa. Huwa na wahusika wengi na dhamira nyingi.

    ii.        Kufungamana na wakati. Ili kuweza kueleza na kufafanua.

  iii.        Mawanda mapana.

  iv.        Mpangilio, msuko wa matukio. Msuko changamano wa matukio.

Hivyo, suala la urefu si kigezo muhimu katika kufafanua riwaya.

Ngano

Senkoro (1982) ngano ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu ili kuelezea au kuonya watu kuhusu maisha.

Wamitila (2004) anasema ngano ni hadithi za kimapokeo ambazo hutumia wahusika wa aina mbalimbali kama miti, majitu, watu ili kuweza kusimulia tukio au kisa fulani chenye mafunzo.

Matei (2011) anasema ngano ni hadithi za kimapokeo ambazo hutumia wahusika kama vitu, mizimu, uchawi…

Hurafa ni aina ya ngano ambayo wahusika wake ni wanyama lakini hutumika kuwakilisha tabia za kibinadamu.

Hekaya ni aina ya ngano ambayo wahusika wake ni binadamu ili kuwakilisha tabia fulani.

Sifa za ngano

i.        Huanza na muundo maalumu au fomula maalumu. Mfano, hadithi hadithi… paukwa…

ii.        Huwa na kimalizio maalumu. Miisho ya kifomula. Mfano, wakaishi raha msitarehe.

iii.        Husimuliwa kwa njia ya kinathari tena kwa mdomo.

iv.        Huwa na funzo fulani kulingana na maadili ya jamii.

v.        Huwa na muingiliano na tanzu zingine kama nyimbo.

vi.        Wahusika wake mara nyingi ni bapa.

vii.        Mandhari hayapewi nafasi kubwa na wakati mwingine hayaoneshwi.

viii.        Dhamira za kingano zinahusu mapambano kati ya wema na ubaya.

ix.        Muundo wake ni sahili.

x.        Zinahusu kufichua hadhira iliyofichika.

xi.        Kuwa na ujirudiaji.

Tamthiliya

Ni andiko ambalo lengo lake ni kwa ajili ya maonyesho.

Ushairi

Ni utungo ambao unaonyesha jinsi wazo, hali, kitu au tukio fulani kwa kutumia lugha ya mkato, mpangilio maalumu wa maneno yenye kugusa moyo.

Shairi ni utungo ambao unagawanyika katika beti.

Nyimbo

Utungo wenye mahadhi ya sauti ya kupanda na kushuka. Kuna aina nyingi za nyimbo:

Tendi ni aina ya wimbo inayohusu mashujaa.

Fasihi ya watoto kwa ujumla

Nadharia:

Fasihi chimbuko lake ni Mungu (Plato).

Udhaifu

Inachanganya imani na taaluma. Huwezi kuthibitisha kisayansi.

Sihiri

Nguvu ama uwezo wa kimiujiza.

Mwigo wa uigaji

Wananadharia hii wanaamini kwamba, mambo yote yaliyopo katika dunia hii yanaigwa toka kwa Mungu.

Nadharia ya kiyakinifu

Waasisi ni Karl Max na Engels.

Mwanadamu ni zao la maumbile ambayo yalitokana na mabadiliko. Waamini kuwa, mwanadamu alianza kama sokwe.

Fasihi ya Watoto

Ilitokana na simulizi au hadithi ambazo zilikuwa zikitolewa katika jamii kwa njia yam domo kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Simulizi hizo zilikuwa na lengo la kuburudisha jamii.

Tunaweza kugawa fasihi ya watoto katika vipindi vifuatavyo:

Zama za mwanzo 400

Hakukuwa na fasihi ya mtoto kama ilivyo sasa. Kulikuwa na fasihi ya jumla.

Zama za kati 476-1400

Kulikuwa na simulizi za kidini, hususani simulizi za kibiblia. Mfano, kulikuwa na habari za mtoto Yesu na zilihusu sala mbalimbali. zilikuwa zinahusu zaidi maadili. Hakukuwa na michoro. Simulizi hizi zilikuwa na mchanganyiko wa fantasia na uhalisi.

Kipindi cha elimu na maarifa 1400-1700

Dhana ya utoto ilianza kuwaingia watu.

Uhamasishaji wa elimu.

Vitabu vilianza kuchapishwa.

Kitabu cha kwanza cha watoto cha picha kilichapishwa na kilitungwa na John Comenius.

Vitabu vingine viliendelea kutungwa.

Watoto walikuwa angalau wengi, hata hivyo hawakupewa taswira ya utoto.

1700-1830

Dhana ya utoto ilianza kuchukuliwa kwa upekee.

Vitabu vingi vya watoto vilianza kuchapishwa.

John Newberry aliweza kutunga kitabu kidogo zaidi ambacho kingeweza hata kuwekwe mfukoni.

Wazazi walikuwa wanasomea watoto vitabu.

1830-1900

Kazi za watoto za kifantasia zenye ubunifu wa kisasa. Vitabu hivi vilihusu: maadili, kufundisha, kuburudisha n.k

Lakini pia, kulitokea hadithi za kweli.

Kuanzia karne ya 20

Hapa ndipo tunapata kazi zenye ubunifu wa hali ya juu zinazowahusu watoto. Hii yote ni kutokana na watu kupata elimu.

Fasihi ya watoto nchini Tanzania

Hii inajumuisha kazi za riwaya, hadithi, ushairi ambazo zinaandikwa. Fasihi andishi ya watoto ni change kwa sababu haikupewa kipaumbele. Kazi nyingi ziliwahusu watu wazima.

Mulokozi anasema fasihi andishi ni changa kuliko fasihi simulizi kwa  kuwa uandishi hutugemea fasihi simulizi na ili iwepo ni lazima kuwe na maandishi. Vilevile fasihi andishi ya watoto ilichelewa zaidi.

Hadithi fupi zilizoonekana za kwanza zilionekana zilianza kuchapwa miaka ya 1960.

Kupatikana kwa vitabu vya watoto kuliwezeshwa na mradi wa vitabu vya watoto.

Mulokozi alitunga Ngome ya Mianzi na Moto wa Mianzi.

Watu mbalimbali walihamasika kutunga fasihi ya watoto.

Mradi huendesha mashindano ya usomaji na uandishi.

Kitabu cha kazi ya kwanza lazima kiwe na picha nyingi zaidi kuliko ngazi ya pili na tatu.

Hivi sasa Tanzania ina vitabu vingi vya fasihi ya watoto.

Maendeleo ya fasihi ya watoto nchini Tanzania

Fasihi ya watoto si kongwe. Kabla ya mwambao wa pwani kuingiliwa na wageni, fasihi ya Kiswahili ilikuwa ni ya kusimuliwa. Maendeleo ya fasihi hususani ya Kiswahili ni suala lisilojadilika bila kuangalia historia ya Tanzania.

Kipindi kabla ya uvamizi kulikuwa na simulizi tu. Kipindi cha ujamaa jamii ilikuwa na itikadi ya umoja na ushirikiano. Hivyo fasihi ilikuwa ya wote. Fasihi haikutofautiana kati ya ile ya watoto na watu wazima.

Baada ya wageni, mambo yalianza kubadilika. Mfano kuingia kwa waarabu walioleta hati ya kiarabu na uislamu.

Fasihi ilikuwa inafundishwa kupitia mafundisho ya mtume. Hati ya kiarabu ilisaidia katika fasihi.

Kipindi cha Waarabu kilikuwa na shujaa wa kijadi maarufu mfano Fumo Lyongo.

Mulokozi 1996.

Tungo mbalimbali zilitungwa ikiwemo Tumsifu Yangu.

Baada ya Waarabu walikuja Wareno. Walisaidia kueneza Kiswahili. Walipofika kulitokea mgogoro kati ya wenyeji na Wareno. Waarabu walisaidiana na wenyeji kupambana na Wareno.

Kipindi hiki kazi zilitungwa kuonyesha hali ya kuwapinga Wareno, mfano: Mzungu Migeli, Portuguese Afala. Bado fasihi ili dumisha watoto.

Kipindi cha Waarabu baada ya kuondoka kwa Wareno. Tenzi mbalimbali ziliibuka. Mfano, utenzi wa Mwanakupona.

Kipindi cha wageni kutoka magharibi walileta hati ya Kirumi na dini ya Kikristo.

Kuletwa kwa hati za kirumi zilisaidia  baadhi ya simulizi kuwekwa katika maandishi, kazi zikaanza kutafsiriwa mfano: Machimbo ya Mfalme Selemani, Hekaya za Abunuwasi.

Mzungu alionekana bora kuliko mwenyeji.

Kipindi hiki kulianzishwa shirika la Uchapishaji K.A.M 1948...

Notes Hazijafika Mwisho, Gusa Hapa Kupata Notes Zote kwa Tsh. 2,000/= Tu.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024