Mtihani wa Kiswahili Kidato cha Nne 2022 1
Endapo Unahitaji Kufanya Mtihani Huu ili Usahihishwe, Wasiliana na Mwalimu Hapa
Muda:
Saa 3
Maelekezo
1. Karatasi hii ina sehemu
A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
2. Jibu maswali yote katika
sehemu A na B na maswali matatu kutoka sehemu C.
3. Sehemu A ina alama 15,
sehemu B alama 40 na sehemu C alama 45.
4. Zingatia maelekezo ya
kila sehemu na ya kila swali.
5. Simu za mkononi na vitu
vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
Sehemu A (Alama 15)
Jibu
maswali yote katika sehemu hii.
1.
Chagua herufi ya jibu sahihi katika Vipengele
(i) hadi (x), kisha andika herufi ya jibu hilo kwenye kijitabu chako cha
kujibia.
i.
Ipi ni seti sahihi ya vipera vya fasihi
simulizi?
A. hadithi, semi na mizungu B. hadithi, semi na vitendawili C. hadithi, semi na mafumbo D. mafumbo, ngomezi na bembea E. Hadithi,
semi na ushairi
ii.
Dhima kuu ya rejesta katika lugha ni ipi?
A. kutangaza lugha duniani
kote B. Kutambulisha watumiaji wa lugha
ya Kiswahili C. Kuongeza maneno
mengi katika kamusi D. kuwapa pumziko
watumiaji wa lugha E. kukuza utamaduni wa
lugha ya Kiswahili
iii.
Bainisha sentensi yenye muundo wa nomino,
kitenzi na nomino:
A. Chakula kimeliwa shuleni.
B. Baba amelala darasani. C. wamepigwa kwa sababu ya ujinga wao. D. mtoto
anapika ugali. E. Kila kitabu na nabii wake.
iv.
Njia ipi ya uhifadhi wa kazi za fasihi
simulizi haipokei mabadiliko ya haraka kati ya hizi?
A. Kichwa B. Maandishi C.
kompyuta D. kanda za kunasa sauti E. B C na D ni sawa
v.
“Yooo… yooo… leo nimekuja kutoa nyimbo yangu
mpya.” Yapi ni masahihisho ya sentensi hii?
A. Nimekuja kutoa wimbo
zangu mpya. B. Nimekuja na nyimbo mpya C. Nimekuja kutoa wimbo wangu mpya D. Nimekuja
kuachia nyimbo mpya. E. Nimekuja.
vi.
“Wazee, nahamisha majeshi.” Ni ipi dhima ya
mazungumzo haya?
A. Kupunguza ukali wa
mazungumzo B. kupunguza hadhira C. kupamba lugha D. kusisitiza mazungumzo E.
kufikisha ujumbe barabara
vii.
“Mpishi anapika chakula chake polepole.”
Kiima cha sentensi hii kimejengwa na aina gani ya neno?
A. kielezi B. kihisishi C.
kitenzi D. kivumishi E. nomino
viii.
Idadi ya silabi nane kati na nane mwisho
ambazo hutengeneza jumla ya silabi kumi na sita katika ushairi huitwaje?
A. Vina B. Mizani C. Vituo
D. Mistari E. Bahari
ix.
Mambo muhimu ya kuzingatiwa katika uandishi
wa kadi ya mwaliko ni yapi kati ya haya?
A. Jina la mwalikaji na jina
la ndugu wa mwalikwa B. Mahali pa kukutana na kiasi cha mchango C. Cheo cha
anayealikwa na cheo cha anayealika D. Siku ya tukio na jina la anayealika E.
Majibu kwa wasiofika na namba ya kukusanya michango
x.
Ni kauli ipi iliyotumika katika uundaji wa
neno ‘piga’?
A. kutendama B. kutendesha
C. kutendeana D. kutenda E. kutendwa
2.
Oanisha maana za dhana za uundaji wa maneno
katika orodha A na dhana husika katika orodha B, kisha andika herufi ya jibu
sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
Orodha A |
Orodha B |
i. bibo ii. pikipiki iii. mwananchi iv. msomi v. lima |
A kutohoa B miambatano C mpangilio tofauti wa mofimu D kufananisha sauti, umbo au sura E kufupisha maneno F Urudufishaji G kuambisha |
Sehemu B (Alama 40)
Jibu
maswali yote katika sehemu hii.
3.
Tunga sentensi moja kwa kila njeo
iliyobainishwa katika vipengele hapo chini:
i. Wakati uliopo mtimilifu
ii. Wakati uliopita
iii. Wakati ujao
iv. wakati uliopo
unaoendelea
4.
Kwa kutumia hoja nne, fafanua mambo manne
yanayohatarisha kutoweka kwa lugha ya Kiswahili.
5.
Taja mambo manne yanayosababisha utata katika
sentensi.
6.
Eleza mambo manne yanayopatikana katika
kamusi.
7.
Soma beti zifuatazo kisha jibu maswali
yanayofuata:
Tanzania, Tanzania,
Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania,
Jina lako ni tamu sana.
Nilalapo nakuota wewe,
Niamkapo ni heri mama we,
Tanzania Tanzania,
Nakupenda kwa moyo wote.
a. Taja faida mbili za wimbo
huu kwa jamii ya Tanzania.
b. Unadhani ni nani
anastahili kuimba wimbo huu? Toa sababu ya jibu lako.
c. Toa mfano wa takriri moja
iliyotumika.
d. Unadhani hili ni aina
gani ya shairi? Toa sababu moja.
8. Andika barua kwa mtendaji
wa kata ya Kishapu S.L.P 123, kuomba kazi ya muda mfupi ya kuhesabu watu-SENSA.
Jina lako liwe Jiwe Sanane wa S.L.P 256 Kasulu Kigoma. Barua yako ipitie kwa
balozi wa mtaa unaoishi.
Sehemu C (Alama 45)
Jibu
maswali matatu kutoka katika sehemu hii.
9. Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari, umeitwa kwenye usaili wa nafasi ya kazi katika Chuo Kikuu
Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam. Katika uthaili umetakiwa kuthibitisha
iwapo mhakiki wa kazi za fasihi ana umuhimu wowote katika jamii. Kwa kutumia
hoja tano na mifano ya kazi mbalimbali za kifasihi, thibitisha hoja hiyo ili
kukidhi haja ya usaili wako.
10. Chagua mashairi matatu
kwa kila diwani kutoka katika diwani mbili ulizosoma kisha onyesha jinsi
washairi walivyo wakosoaji wa jamii ya leo.
11. Waandishi wa riwaya za
Watoto wa Mama Ntilie na Joka la Mdimu wameonyesha kuwa umasikini ni miongoni
mwa matatizo yanayozikabili jamii nyingi. Kwa kutumia mifano, eleza mambo
matatu yaliyopendekezwa na waandishi kwa kila riwaya yenye lengo la kuzuia
umasikini katika jamii.
12. Eleza jinsi uteuzi wa
wahusika ulivyoibua dhana ya gonjwa la UKIMWI kwa kutoa hoja tatu kwa kila
kitabu kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.
Endapo Unahitaji Majibu ya Mtihani Huu, Gusa Hapa Kuwasiliana Nami.