Mtihani wa Kiswahili 1 Kidato cha Sita 2021 2
Maelekezo ya Kufanya Mtihani Ili Usahihishwe na Mwalimu:
1. Mtu yeyote na
popote alipo anaruhusiwa kufanya mtihani huu.
2. Fanya mtihani huu
kwa kutumia aina yoyote ya karatasi.
3. Ukimaliza, piga
picha karatasi hizo kisha zitume WhatsApp kwenye namba ya Mwalimu Makoba, 0653
250 566.
4. Subiri mtihani
wako usahihishwe, Urudishiwe na ufanyiwe masahihisho.
5. Gharama ya mtihani
huu ni shilingi 2,000/= (elfu mbili).
Namba za malipo ni: M
– Pesa 0754 895 321 (Daud Mhuli) na Tigo pesa 0653 250 566 (Daud Mhuli).
Pata Majibu ya
Mtihani Huu, Gusa Hapa Kuwasiliana Nami.
Muda: Saa 3
Maelekezo
1. karatasi hii ina sehemu A
na B zenye jumla ya maswali nane.
2. Jibu maswali yote katika
sehemu A na maswali matatu kutoka sehemu B. swali la tano ni la lazima.
3. Sehemu A in alama
arobaini na sehemu B ina alama sitini.
4. Zingatia maagizo ya kila
sehemu na kila swali.
5. Simu za mkononi na vitu
vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
6. Andika namba yako ya
mtihani au jina katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.
Sehemu A (Alama 40)
Jibu
maswali yote katika sehemu hii.
1. Soma kifungu cha habari
kifuatacho kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata:
Msiba mkuu wa Watanzania ni
ufisadi. Ufisadi unaofanywa na viongozi wao unawaumiza na kuwaacha watupu kabisa. Ama hakika, ufisadi
unapofanyika, haki ya wananchi hupotea na baada ya muda hupandishiwa kodi ili kufidia.
Watanzania
wanawaza ufisadi unaofanywa na viongozi watawezaje kuuondoa. Pengine suluhisho
ni kuchagua viongozi wema, lakini utawezaje kutambua kuwa huyu ni kiongozi mwema na huyu ni mbaya? Ni
ngumu.
Pengine suluhisho juu ya
ufisadi ni mahakama. Lakini mahakama
ya mafisadi ipo lakini ufisadi unaendelea. Basi kumbe suluhisho dhidi ya
ufisadi ni serikali kufanya mambo yake kwa uwazi, zikiingia pesa fulani,
serikali isema, akipewa bwana fulani serikali isema yaani kila linalotendekea,
wananchi wataarifiwe. Hii itasaidia kupunguza ufisadi, siyo kuumaliza.
Dawa kamili ya ufisadi ni uzalendo wa viongozi. Viongozi wakiipenda
nchi yao zaidi ya wanavyojipenda wao, ufisadi utakwisha.
Maswali:
a. Toa maana ya maneno
yafuatayo:
i. Watupu ii. Kodi iii.
Watanzania iv. Kiongozi v. Mahakama vi. Uzalendo
b. Fafanua wazo kuu la
mwandishi katika aya ya pili.
c. kwa kutumia aya moja,
eleza athari za ufisadi katika jamii.
d. Fupisha habari ifuatayo
kwa maneno yasiyopungua mia moja.
Kusoma ndiyo mwanzo wa
maarifa yote ulimwenguni. Mtu asiyejua kusoma huhesabika kuwa mjinga. Ajuaye
kusoma, huwezi kujipatia maarifa mapya yakamsaidia sana katika maisha yake.
Katika nchi yetu, watu
hujifunza kusoma wengine wakiwa shule ya msingi na wengine kabla ya elimu ya
msingi. Lakini wapo vichwa ngumu ambao humaliza la saba bila kujua kusoma.
Changamoto ya watu wetu ni
kwamba, baada ya kumaliza elimu, hukoma kabisa kusoma. Huona kama wamemalizana
na jambo la kusoma, lakini kumbe ukweli ni kwamba, mwanadamu safi ni yule
asomaye vitabu kila siku ili kujiongezea maarifa yake. Kusoma ni kama hewa,
huwezi kujua umuhimu wake mpaka uikose walau kwa dakika moja.
Huko katika mataifa
yaliyoendelea sana kwa teknolojia, watu wake husoma vitabu ili kupata maarifa
mbalimbali. Husoma vitabu vya fasihi, wakasoma vitabu vya biashara na hata
vitabu vya saikolojia. Sasa wayapatapo maarifa hayo, huijenga nchi yao.
2. Bainisha dhima nne za
kielezi katika lugha ya Kiswahili.
3. Kwa kutumia mifano, eleza
dhana za kisarufi zifuatazo:
a. Mzizi huru b. Fonolojia c.
Viambishi d. Sentensi changamano e. Alomofu
4. Toa maana mbili kwa kila
sentensi zifuatazo:
a. Mwalimu wetu wa Kichina
alitutembelea jana.
b. Bibi Mwanaheri
amewachezea jirani zangu.
c. Mtoto wake alimwibia
pikipiki.
d. Wizi wa silaha
umeongezeka sana siku hizi.
e. Huyu babu ni mpangaji
mzuri.
Sehemu B (Alama 60)
Jibu
maswali matatu kutoka sehemu hii. Swali la tano ni la lazima.
5. Endapo utaandika kitabu
chako na kikatakiwa kufasiriwa, ni sifa zipi utazizingatia kwa mfasiri
utakayemwajiri?
6. Andika insha yenye maneno
300 kuhusu muziki wa Tanzania.
7. Watu husema, “Waingereza
walikuwa wabaya, lakini walifanya jema moja la kukuza na kueneza lugha ya
Kiswahili.” Thibitisha kauli ya watu hao kwa kutumia hoja sita.
8. Taasisi ya Taaluma za
Kiswahili (TATAKI) iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imefanya mengi
katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili nchini Tanzania. Toa hoja sita
kuthibitisha madai haya.
Pata Majibu ya
Mtihani Huu, Gusa Hapa Kuwasiliana Nami.