Dhima za Kategoria za Virai katika Lugha Kisintaksia

Lugha ya Kiswahili inazo tungo nyingi na miongoni mwa tungo hizo ni tungo kirai. Tungo zingine ni tungo neno, kishazi na sentensi. Kategoria za virai ni sifa bainifu zinazoambikwa kwenye aina za virai. Kwa upande wa maana, tungo kirai ni kipashio kidogo cha kimuundo chenye neno moja au zaidi ambacho hakina muundo wa kiima (K) na kiarifu (A). Kirai huwa na neno kuu moja linalotawala. Neno hilo linalotawala ndilo huwa aina ya kirai. Kategoria ya virai inajumuisha kirai nomino, kirai kivumishi, kirai kitenzi, kirai kielezi na kirai kihusishi. Zifuataza ni dhima za kategoria za virai katika lugha ya Kiswahili Kisintaksia.

Kirai nomino kina dhima ya kuwa kiima, yambwa, yambiwa, kijalizo cha kirai kihusishi na kinaweza kukaa mahali pengine popote ambapo nomino inakaa. Kwa mfano: Askari waaminifu waliwakamata wahalifu wetu wote kwa siku moja. Askari imetumika kama kiima cha sentesi hiyo. Katika kirai nomino, neno kuu ni nomino.

Kirai kitenzi kina dhima ya kuwa kiarifu. Kwa mfano, mama anapika chakula cha baba yake na baba. Katika mfano huo wa sentensi neno Anapika ni kiarifu na neno mama ni kiima. Hivyo kirai kitenzi kimetimiza dhima yake ya kuwa kiarifu ama kirai kitenzi kimefanya kazi ya kuwa kiarifu. Kirai kitenzi ni kirai ambacho muundo wake hutawaliwa na kitenzi.

Kirai kivumishi kina dhima ya kuwa kikumushi cha kirai nomino. Kwa mfano, Kijana mzuri mshamba. Katika mfano huo, mzuri mshamba imetumika kukumusha nomino kijana. Pia, kirai kivumishi kina dhima ya kuwa kiima katika sentensi. Kwa mfano, wakubwa wale. Kirai kivumishi ni kirai ambacho neno lake kuu ni kivumishi.

Kirai kielezi kina dhima ya kuwa kikumushi cha kirai kitenzi. Kwa mfano, anaruka kichurachura. Katika mfano huo, neno kichurachura ni kikumushi cha kitenzi anaruka. Pia kina dhima ya kuwa kiima cha sentensi kwa mfano chumbani kwangu. Katika mfano huo, neno chumbani kwangu limetumika kama kiima. Kirai kielezi ni kirai ambacho neno lake kuu ni kirai.

Kirai kihusishi kina dhima ya kuwa kikumushi cha nomino kwa mfano, matawi ya miti. Pia, kikumushi cha kitenzi (Mwalimu amesimama kwa hofu kubwa). Pia, kirai kihusishi kinafanya kazi kama kiwakilishi. Kwa mfano, kwa mganga kumewekwa dawa nyingi. Kirai kihusishi ni aina ya kirai ambacho neno lake kuu ni kihisishi.

Hivyo basi, kategoria ya virai katika lugha ya Kiswahili ina dhima zake kama ilivyoelezwa hapo juu. Virai hufanya kazi kubwa ambayo imesaidia kuipa lugha maana. Uanishaji wa virai umejikita katika aina za maneno, yaani, aina za virai zinatokana na aina za maneno. Kwa kutumia kigezo hicho ndiyo tumepata kategoria hizo za virai zilizojadiliwa.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Vichekesho vya Kuchekesha na Kuvunja Mbavu 1