Swali la Ufahamu na Ufupisho Kuhusu Mtu Aliye Muungwana

Kijana anasoma kitabu.

1.   Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu kwa usahihi maswali yanayofuata.

Wazo la watu wengi juu ya muungwana ni kuwa mtanashati au labda kuwa mtu arifu mwenye cheo kwa watu. Lakini nguo nzuri hazimtukuzi mtu wala hazimfanyi kuwa muungwana. Fasihi ya hili ni kuwamba, nguo ni kama ngozi ya mtu au mnyama; au hasa ni duni sana kuliko ngozi au manyoya. Ngozi ya simba haiwezi kumfanya punda kuwa simba. Uungwana wa kufanywa na mshoni ni mzaha; si uungwana wa kweli. Neno muungwana lina maana kubwa zaidi kuliko nguo nzuri au adabu nzuri na elimu nzuri. Kwa hakika twatumia vibaya neno hili kwa mtu yeyote aendaye kwa miguu miwili.

Kwanza muungwana hawezi kumuudhi au kumdhuru mtu kwa maneno au matendo yake, hata kwa kumtazama. Ana moyo wa uvumilivu na anaweza kusikiliza kwa makini maoni ya watu wengine bila ya kujaribu kuwalazimisha wakubali maoni yake. Ni mkarimu, mnyofu na amini katika taiba yake kwa wengine. Hapendi kujionyesha alivyo tajiri a alivyoelimika. Hana makuu wala unafiki, yu mnyofu kwakila asemalo au atendalo. Hajitwezi kwa matendo yake wala hadunishi matendo ya watu wengine kwa sababu hana wivu. Haudhi wala hadhuru mtu yeyote kwa sababu ajua kwamba ushenzi kama o ni kinyume cha uungwana.

Siku zote muungwana ni mwema kama baba au mama, mwaminifu kama rafiki na msaidizi kama ndugu. Hutenda tena na kuendekesha kama raia mwadilifu ajuae kazi au madaraka yake kwa watu. Huchukuana na watumishi wake kwa mapenzi, huruma na upole. Hujiheshimu na kuwaheshimu wengine. Hivyo basi uungwana wake hautokana na malezi ya shule ila hutokana na uungwana wa kweli.

Maswali

a)   Andika kichwa cha habari hii.

b)   Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari hii.

     i.        Muungwana

    ii.        Arifu

   iii.        Hajitwezi

  iv.        Mwadilifu

c)   Eleza mawazo makuu mawili ya mwandishi.

d)   Kutokana na habari uliyosoma, taja tabia tatu za mtu muungwana.

Majibu

A.  MTU MUUNGWANA
B. i. Muungwana ni mtu mwenye adabu na tabia zinazokubalika katika jamii.
ii. Arifu ni mtu mwenye ujuzi mwingi.
iii. Hajitwezi ni kutokujivunjia heshima.
iv. Mwadilifu ni mtu mwenye maadili mema.
c. Mawazo makuu mawili ya mwandishi ni:
Uungwana, mwandishi anataka watu wawe waungwana na waishi vyema katika jamii.
Wazo la pili ni heshima, mwandishi anashauri heshima iwepo kwa watu wote, wakubwa kwa wadogo.
d. Tabia tatu za mtu muungwana ni:
- Mkarimu.
- Hapendi kujionyesha.

- Siyo mnafiki.

2.   Fupisha habari ulisoma kwa maneno tisini.

Jibu

Maana ya muungwana ipo tofauti zaidi ya watu wanavyodhani. Mtu hawi muungwana kwa sababu ya mavazi yake. Kutazama mavazi kumewapoteza watu wengi na kujikuta mikononi mwa watu wabaya.

Muungwana hatendi mambo mabaya kama: kujikweza, kusema watu vibaya, kusema uongo, unafiki wizi na mambo yote yasiyofaa. Kwa muungwana, kutenda mambo yasiyofaa ni mwiko.

Muungwana ni mwema, rafiki na ndugu. Muungwana hujiheshimu mwenyewe na kuwaheshimu watu wengine. Uungwana ni matokeo ya malezi anayopata mtu nyumbani na shuleni.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Uhakiki wa Tamthiliya ya Kilio Chetu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024