SABABU YA MWIZI KUWAPONGEZA POLISI YAJULIKANA
Leo kumeibuka kituko na gumzo
baada ya mwizi mmoja kuwapongeza polisi waliomkamata baada ya kuiba fedha
katika duka la simu.
Jamaa huyo anayefahamika kwa jina
la Boubacar Diallo na ambaye pia ni mwanafunzi katika chuo cha ufundi cha Mamu
huko nchini Guinea amezua gumzo kwa kitendo chake cha kulimwagia sifa jeshi la
polisi kwa kumkamata.
Baada ya uchunguzi wa masaa
kadhaa, hatimaye sababu iliyomfanya jamaa huyo kumwaga kongole kwa jeshi la
polisi tofauti na walivyo wahalifu wengine ikajulikana.
SABABU ZAJULIKANA
Jamaa huyo imefahamika kuwa ni
mwizi kupindukia na hajawahi kukamatwa kutokana na kuwa na mbinu mbalimbali za
kukwepa mkono wa sheria. Hata hivyo, kitendo cha yeye kukamatwa mapema kuliko
alivyotarajia ndiko kumemshitua na kumfanya awapongeze polisi kwa ufanisi
mkubwa walioonyesha.
AWAOMBEA MSAADA ASKARI
Akihojiwa na waandishi wa habari,
jamaa huyo, alisema polisi wanahitaji vifaa vya kisasa zaidi vitakavyowasaidia
kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Diallo kwa sasa yuko mikononi mwa
polisi na amesema anajuta sana kuwa mwizi. Pia, ameahidi kuacha tabia hiyo.