Tabia 11 za Usomaji Zitakazokupatia Matokeo Mazuri

Kilimo cha Kisasa.
Unaposoma, lengo huwa ni kupata alama nzuri zitakazokusaidia kutimiza yale uliyopanga. Inawezekana unataka kupata A, B, C na wapo wanafunzi wanaotaka kupata D. Ili uweze kupata alama nzuri unazohitaji wewe, zingatia tabia hizi za usomaji:

     1.   Tengeneza ratiba
Unapokuwa unasoma, kuwa na ratiba ya wiki nzima. Ratiba itakusaidia kuwa makini katika masomo na kuepuka kupoteza muda.

     2.   Soma kadri ya uwezo wako
Tumia muda wako mwingi kusoma. Hii haina maana kwamba hutakiwi kupumzika, ila kusoma kiwe kipaumbele.

     3.   Vuta pumzi ndefu kabla hujaanza kusoma
Kuvuta pumzi ndefu kabla hujaanza kusoma hukusaidia uwe makini katika unachokisoma na kuepusha mawazo mengine. Unapokaa kuanza kusoma, vuta pumzi ndani kwa pua, kisha itoe kwa njia ya mdomo. Wakati ukivuta pumzi, hesabu sekunde nne, na wakati unaitoa, hesabu sekunde nne. Itakusaidia ku’concentrate’ wakati wote utakaotumia kusoma.

     4.   Kuwa na sababu inayokufanya usome
Usisome kwa sababu watu wote wanasoma. Tafuta sababu ya kufanya hivyo: wengine husoma ili waweze kupata vyeti, kupanda vyeo, kupata kazi, kupata maarifa na sababu nyinginezo. Wewe pia, tafuta sababu inayokufanya usome.

     5.   Nukuu unapokuwa darasani
Usisikilize peke yake, nukuu yale yanayofundishwa na mwalimu. Huwezi kukumbuka mambo yote yanayosemwa na mwalimu, hivyo nukuu.

     6.   Yasome yote uliyofundishwa shuleni katika siku husika
Kama shuleni ulifundishwa Kiswahili, History na Physics au masomo yoyote, yapitie masomo hayo kabla hujaendelea na ratiba yako. Hii itakusaidia uelewe vizuri kwani bado utakuwa na kumbukumbu juu ya kile ulichofundishwa. Usisubiri mambo yawe mengi ndiyo uanze kusoma.

     7.   Soma ‘notes’ zako kabla hujafanya maswali uliyopewa
Kabla hujajibu maswali ya mwalimu, soma kwanza nukuu zako. Itaifanya akili yako iwe tayari kujibu maswali hayo.

     8.   Lala kwa muda wa kutosha
Ni vizuri zaidi kama utapata saa nane za kulala kila siku. Hata hivyo, kama mambo ni mengi, hakikisha angalau unalala kwa saa saba au sita.

     9.   Pata mazingira mazuri ya kusoma
Sehemu ambayo haina kelele wala usumbufu wa aina yoyote, ni nzuri kwa kusoma. Epuka sehemu zenye makelele na vikwazo vingine vitakavyokukatisha wakati ukisoma.

     10.               Pumzika
Usisome mfululizo, pumzika. Wakati unasoma, kuwa na saa pembeni. Kila baada ya dakika ishirini, pumzika kwa muda wa dakika moja: simama, tembea kidogo, jinyooshe, vuta pumzi ndefu kama nilivyoelekeza, kisha endelea tena kusoma.

     11.               Jipime mwenyewe
Usisubiri mtihani wa mwalimu ndiyo ujipime maarifa yako. Tafuta maswali katika vitabu au mtihani wowote wa online, kisha fanya ili uone uwezo ulionao katika somo husika. Hii itakusaidia kutambua mapema uwezo wako na kuchukua hatua zitakazokusaidia.

Anza leo kufanya mambo hayo, utaona mafanikio.

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kuandika CV | Mfano wa CV Wasifu

Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Mwaka 2024

Jinsi ya Kuandika Risala | Kiswahili Kidato Cha Nne