Mchango wa Tipu, Bloomfield, Krapf Katika Kueneza Kiswahili
Swali lote linasema, “Onesha
mchango wa watu wafuatao katika kukuza na kueneza kiswahili nchini: Tippu Tipu,
D.k Ludwig krapf, Broomfield na Askofu Edward steer.”
Watu wengi wamesaidia katika
kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania. Leo tutajadili mchango wa TippuTipu, Krapf, Broomfield na Askofu Edward Steer.
Mchango wa Tippu Tipu katika kueneza Kiswahili
Jina halisi la bwana huyu ni
Hamad bin Muhammad bin Juma bin Rajab el Murjeb. Alikuwa mwarabu mfanyabiashara
wa watumwa.
Tippu Tipu alisaidia kukua
na kuenea kwa Kiswahili kwa sababu, alitumia Kiswahili katika biashara zake.
Hivyo, kote alikopita, alieneza lugha ya Kiswahili na ikafahamika kwa watu
wengi Zaidi.
Mchango wa D.k Ludwig Krapf katika kueneza Kiswahili
Krapf alisaidia kukua na
kuenea kwa Kiswahili kwa sababu alitunga kamusi ya kwanza ya lugha ya
Kiswahili. Kamusi hii ilisaidia kuuweka msamiati wa lugha ya Kiswahili katika
kitabu kimoja.
Mchango wa Broomfield katika kueneza Kiswahili
Mtaalamu Broomfield naye
hayuko nyuma katika kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili kwani yeye
alijihusisha katika usanifishaji wa lugha ya Kiswahili.
Mchango wa Askofu Edward Steere katika kukuza na kueneza Kiswahili
Askofu Edward Steere
alitafsiri biblia katika lugha ya Kiswahili. Pia aliandika vitabu vingi vya
sarufi ya Kiswahili, miongoni mwavyo ni kile kinachoitwa, ‘A Handbook of the
Swahili Language as Spoken at Zanzibar.’
Lugha ya Kiswahili imefika hapo
ilipo kwa sababu ya mchango wa watu wengi ambao hawakuchoka katika kuipeleka
mbele lugha hii. Wengine walikuza na kukieneza Kiswahili kwa maslahi yao
binafsi, na wengine walikuza lugha ya Kiswahili kwa mapenzi yao katika lugha
hii. Ni jukumu la watumiaji wote wa lugha ya Kiswahili, kuhakikisha wanaikuza
lugha yao na kufika mbali Zaidi.
Mpaka hivi sasa, Kiswahili
kinazidi kujizolea umaarufu ikiwemo kutumika katika mikutano mikubwa ya
kimataifa, kuimbwa na wanamuziki wengi wa kimataifa, kuandikwa vitabu vingi,
kuwa na mitandao mingi inayotumia lugha ya Kiswahili na kingine ni kutumika
katika matangazo ya redio nyingi za kimataifa.